Msaada: Mke wangu anataka tuwe tunaishi na mtoto wa dada yake kila wikiendi na likizo

Pole Sana kwa yalio kupata, binadamu ndivyo tulivyo wengine wanakosa Imani kwa vitu vidogo tu Ila sababu kubwa tunaweza kusema ni hulka ya mtu, tabia inayo tokana na malezi tu ya kwao ama roho mbaya tu ambayo mtu huumbwa nayo.

Cha muhimu ni kuwasamehe tu watu wa namna hiyo wasikupe mzigo nafsini mwako.
 
Nilikuwa-ga najiuliza sana ni kwanini wazazi huwapa watoto majina kama vile Sinandugu, baada ya kudadisi sana moja ya majibu niliyopewa ni kama hii hoja
 
Usiwasikilize wanaokuambia habari za mala mchoyo mala gubu wewe ongea na nafsi yako utachoamua fanya ,imeandikwa kila punda abebe mzigo wake mwenyewe ( watz 4: 16)
 
Mbona umekazania tu hapohapo kwamba mtoto ameambukizwa tabia za jike?,kwani huyo mtoto ana umri gani?,ni utoto tu akikua ataacha Tania za kike
 
Usikute mkeo ni mama wa huyo mtoto
Hili watu hawalioni. Kwanza sidhani kama huyo shemeji yake angekubali hili. Mtoto wake ateseke kisa, au huyo mkewe angelishaachana na hilo wazo maana anajua mumewe hapendi. Jamaa anauziwa mbuzi kwenye gunia na yeye anakubali
 
Hio tabia ya kipuuzi alitakiwa awe nayo mkeo ila inashangaza sana kama kidume cha mbegu ndio kinakuwa na tabia ya hovyo namna hio!

Choyo ni tabia ya kike mkuu!
 
Kwani hao wageni wanakaa kwako milele?
 
Sasa aslong as hulipishwi ada swala la mtoto kukatazwa kwenda kwa babaake si swala la maamuzi ya mama yake! Kama hataki kumpeleka mwache mtoto akikua na kujitambua atamtafuta baba yake. Kwanini unakuwa kama unataka kuwalazimisha watu wazima wenzio kitu ambacho wao binafsi hawakiafiki?

Power yako inaishia kwenye ushauri tu, kama wameopt kutokumpeleka kaa kimya fata mambo yako. Kama unaona mtoto wa shemeji yako ni kero mfukuze na uvunje ushemeji na dada wa mkeo usilalamike kama mtu ambaye hana maamuzi.
 
Mamii huyu jamaa anataka kutufanya wote tuonekane vituko ila trust me wanaume wenye choyo ni 1% tu ya population na hawa huchangiwa na malezi mabovu.
 
Mkuu hapo sijaona kosa zaidi nahisi utakuwa una viashilia vya uchoyo,
Nakushauri mwambie mkeo ili amwambie dada yake achangie pesa kidogo ya uji na ubwabwa ili roho yako iridhike,
Maana sijaona hapo hoja ya msingi kwa upande wako zaidi ya uchoyo,,
2021 uchoyo haulipi!!
 
. Hapo wewe kinachokuuma Ni kuwa kwanini unamsaidia mwanaume mwenzio?
Haswaa, ila kama jamaa hataki kuwajibika afanyeje sasa 😁😁😁? Shemejie amemsogeza mtoto ili apate ile moral support ya baba ila lenyewe halielewi limetanguliza kijiba cha roho na choyo mbele.
 
Yeah huenda ndio chanzo akamtema huyo mwanamke. Maana hawa wanawake wengine sio kabisa.
 
Mambo kama haya hukaribisha umaskini sana ktk familia zetu za kimaskini, hii tabia imenikosti sana.
Kuna watu hapa watasema kwani sh ngapi lkn hawajui chochote kile ni gharama hata kama ni sh 100. Mjue tu bajeti ya familia haiwezi kua ileile

Mkuu nakuelewa sana
 
Mkuu acha ukimya mpige marufuku mbona simpo tu, sioni haja ya kuja kuomba ushauri huku maamuzi unayo wewe
 
Du mkuu una roho ngumu Sana ,mtoto mdogo tu unamuanzishia uzi humu?. Wengine tunakaa na wakubwa zaidi ya hao 3. Akili inatanuka ya utafutaji ,maisha yanaenda .Mwisho wa siku wananisaidia kwenye shughuli nyingi na zinaenda poa.Nawaona moja ya familia yangu ,maisha yanaendelea.Unapowafanyia mazuri ,wanaposhukuru Mungu nawe anakuongezea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…