Punguza hasira kidogo, warembo Kama wewe hapaswi kukasirika sana.
Mkuu hakuna mtu namchukia hadharani kama mtu mchoyo wa chakula😡😡😡
Ngoja nikupe hiki kisa kinanihusu mimi Chakorii.
mwaka
1999 nakumbuka kabisa mtoto wa babangu mdogo alikuwa amefikish 40 tangu kuzaliwa kwake...so kulikuwa kuna tafrija kidogo lakni shughuli ilikuwa ni kumbwa tu..watu wengi walikuwepo.
Nakumbuka watu walikuwa wameshaanza kula(kuna kitu mama alinituma nakumbuka)so wakati wameanza kula sikuwepo.
Niliporudi eneo la tukio njaa ilikuwa inauma nakumbuka..nilimkuta binamu yangu mtoto wa Dadake na baba(yeye alikuwa upande wa chakula).nikamfuata nikamwambia binamu njaa inauma sijakula bado...akaniangalia hakunijibu(kuku kuwa kuna watoto wengine wa mtaani na wenyewe walikuw hawajala..so ni kama walikuwa wananisikilizia)
Nikamuona binamu anachukua ungo(kuu kuu kidogo)akatupakulia makoko (chakula kingine kizuri kilikuwepo.nilikiona) tulikula lkni hakuna siku nilikuwa mnyonge kama siku ile😢😢😢niliumia mnooooo..hapo ndipo siku niliyogundua kuwa ninakuwa yangu ni mchoyo wa chakula.
Sikuwahi kusema Kwa yeyote zaidi ya leo hapa JF na hakuwahi kujua kamwe.
Miaka ikapita.mwaka jana tulikuwa tunaenda mkoa fulani kwenye msiba ni mbali kabisa mkoani huko..hakuna na nauli na anataka kwenda kuzika,akaniomba nimkopeshe kiasi fulani cha pesa ni kidogo tu ☹️☹️☹️Ghafla nikakumbuka mwa
1999
Nikajawa namajonzi sijui kwa nini.😩😩
Sikumkopesha ile hela bali nilimpa.nilimwambia nitakulipia nauli usijali mpka tutakakofika msibani.
Sikuwahi kuwa na furaha nae..
So kila nikimuona mtu mchoyo wa chakula ninakasirika na kumuona ni fukara wa nafsi.
Kwahiyo,mtu akileta uchoyo wa chakula na kama nammudu namchana au ninamziria chakula chake ale mwenyewe mpka ashibe au nitoe niwape mbwa wale😒😒😒.
Siwezi ficha hasira kwa mtu mchoyo...niko hivyo.