Msaada: Mmewezaje kupona maumivu ya kufiwa na mtu wa karibu?

wacha nijikusanye akili na mwili!
 
Ni watu waliopitia mazingira kama yako pekee ndiyo watakuelewa.
Kwa ufupi tu, kifo ni fumbo la kikatili sana. Na ndiyo hivyo tena; hakikwepeki. Waliofariki wametangulia! Na sisi zamu yetu ikifika, tutafuata.
 
Thank u love. Aliacha mbwa wake mmoja,ana mtoto sasa. nimebaki nao nawatunza! Ni kweli wanagive back huo upendo! Nakaa pia na mtoto wake. I hope vitanisaidia
Wow! Umeona sasa alihisi Dada ake atakua mpweke akiondoka akakuachia Mtoto aendelee kukupa kampani, basi muangalie Mtoto kama ulivyomuangalia ndugu yetu, be strong muda unaponyesha,

Nimefurahi amekuachia na Mbwa darling just know you are blessed 😘

I send my hugs and if you need someone to talk i'm in.
 
Atakuwa ni mwanasaikolojia bila shaka. Hivyo anatengeneza mazingira ya kazi kupitia matatizo ya mtu.
 
Upendo unazidi mauti, ukisoma muhubiri,
Tunatakiwa kumpenda Mungu tu upendo usio na kipimo, ila Hawa ndugu tunawapenda upendo usio tuumiza sisi ,
Kwanza nakushauli acha kumuombea kwa sababu hakuna mstari kwenye biblia unao utumia kumuombea,
Pili omba msaada kwa Mungu, Petro alivokua anazama kwenye maji aliomba msaada,
Muombe Mungu msaada, mwambie Mungu ninazama , mwambie Mungu nisaidie nikupende Sana wewe na si. Mwingine,
Wapo watu Wanafiwa na waume zao au watoto wao nao wanakufa pia kwa sababu upendo wao waliweka mwingi kwa mtu kuliko kwa Mungu,
It looks like ulimpenda Sana ndugu yako kuliko Mungu,
So muombe Mungu umpende Sana yeye kuliko kaka yako
 

Mie mpaka leo huwa naomba hata aje ndotoni tu nimuone lakini hajawahi kuja! Huwa haipiti wiki mbili naingia fcbk page yake namtumia meseji bas natulia!
 
Kwanza pole sana kwa msiba,

Nachoamini ni muda unaponya, msiba wa baba yangu uliniuma sana na ilikuwa ghafla pia,, niliteseka kwa miaka takribani 6 hivi,,ikawa kama namuona, namuwaza sana nililia sana, nilimuota sana pia,, ikafikia hatua nikiwa peke yangu kama namuona napiga kelele, mama mmoja nikamsimulia akanipa majani flani hivi niyafikiche nipake machoni na mengine niweke chini ya mto,, kwenye miezi 6 hali ilipotea nikawa kawaida mpaka leo namkumbuka lakini sipati hiyo hali,
 
Big sis; hakiiiiiiii...........

I remember kuna siku ulisimulia kitu like mkiwa wadogo; mdogo wako alibanwa na pumu na mlikuwa mmefungiwa sijui pasipo msaada wowote; ikakubidi uvunje mlango kuhakikisha mdogo wako anatibiwa (kama nakumbuka vizuri ulimshikia panga mlezi wenu alipokuwa harespond chochote kuhusu kumpeleka mdogo wako hospital).......Ilinifanya nione how much ulikuwa unampenda mdogo ako; how exactly big sisters are.

Tunajikutaga sisi ndiyo kama mama wa wadogo zetu na sio madada tena. I know what she/he meant to you; she/he was the only thing left for you after you both lost your parents; you found strength and purpose to live just for her/him. I can imagine how her/her death has hit you. Daah yaani naona hata kutype "pole sana" ni kama daah. Mungu akutie nguvu dada mkubwa.

Please you need to do a closure. Hiyo hatia uliyonayo kwamba maybe hukumlinda ipasavyo ndiyo maana imefariki; inabidi iondoke sasa. Jisamehe kabisa
Kama unaweza kwenda alipozikwa; fika frequently. Mimina moyo wako; ongea yote ambayo unatamani umwambie hata kama hakusikii; I know utalia vya kutosha na kwa kiasi fulani utapata amani ya moyo.

Wakati wa mtu kufa ukifika; hakuna utakachoweza kufanya kuzuia mauti yasimpate. Amini tu wakati wake ulifika; na hata asingekufa kwa presha; angekuwa tu hata kwa ajali au malaria. His/her time was simply up.

Hata katika machozi na uchungu wako mkuu ulionao; usiache kumshukuru Mungu. Mshukuru Mungu hata alikupa Neema ya kuwa na mdogo wako kwa miaka yote hiyo aliyokupa; imagine asingekuwepo na huku wazazi hawakuwepo pia. Mshukuru Mungu amekuachia na mtoto wake wa pekee ambaye ndiyo kumbukumbu halisi ya mdogo wako. Mshukuru Mungu hata umepata nafasi ya kumuona kwa mara ya mwisho na kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele; at least unaweza kwenda kumtembelea kaburini kwake na ukafeel uwepo wake. Imagine wale ambao wapendwa wao wametoweka hawajulikani hata walipo; whether wapo hai au wamekufa; imagine familia zao zinaishi kwenye sintofahamu ya namna gani au unaambiwa tu ndugu yako wamepata ajali ya meli imezama, na miili yao haionekani. So ukija kuangalia; bado zipo sababu nyingi tu za kumshukuru Mungu katika hili pia. Take heart big sis; Mungu atakuvusha katika hili. Usiache kuomba, usiache kuongea na watu; toa yote yaliyo moyoni mwako. It shall be well with you big sis

Sent using Jamii Forums mobile app
 
snowhite Mungu ni mwaminifu, mshukuru Mungu. Yaliyotokoe kwako hayarudi nyuma( kufiwa ), ila yatupasa kumhsukuru Mungu njia pekee ya kukubali kilichotoea na kuruhusu faraja ya Mungu ( mapenzi ya Mungu moyoni mwako ). Tumia mda mwingi kumshukuru Mungu , tumia mda Mungu kuweka moyo wako kwa mtoa faraja wako ambae ni Mungu. Kuna nyakati tunajikuta katika hii dunia kama tupo peka yetu, ila usama wetu huja pale tunapokimbilia miguuni pa Mungu
 
Unahitaji greaf counselling ambayo itakusaidia kuondokana na ilo welcom pm
 
Pole ndugu yangu, ni kweli maumivu ya kuondokewa na mtu wa karibu hayazoeleki! Nilifiwa na baba yangu mzazi miaka ya nyuma, hakika ilichukua muda mrefu sana akili kukubaliana na tukio hilo. Kwanza, unaona kama ameonewa kuchukuliwa na unataka umrudishe, na unahisi kinachoendelea ni kama ndoto tu, ambayo muda mfupi baadaye inaisha na hivyo kuendelea na hali ya kawaida, lakini kumbe ni tukio la kweli! Jipe moyo, kila jaribu analokupa Mungu lina kipimo chake, Mungu hawezi kukupa jaribu litakalokushinda!
 
dawa ya kusahau mpendwa wako kama umefiwa na mke ao haraka kama umefiwa namume olewa kama umefiwa na mzazi ndugu nawe kumbuka kuwa kunasiku utakufa
 
Mkuu snowhite kwanza utambue hapa duniani sio kwetu na ndio maana inabidi tufikwe na mauti turudi tulikotoka, hakuna namna na sisi tutafuata tu chukua muda wako kujiandaa na kifo chako na usiendelee kupoteza afya yako kwa maumivu makali kwani yeye tayari ameshakusahau yuko busy na aliyokutana nayo huko.

Mwisho kubali kuwa ameshafariki na hawezi kurudi tena sasa tumebaki mimi na wewe na yule tumeandaa nini? pole kwa msiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…