Big sis; hakiiiiiiii...........
I remember kuna siku ulisimulia kitu like mkiwa wadogo; mdogo wako alibanwa na pumu na mlikuwa mmefungiwa sijui pasipo msaada wowote; ikakubidi uvunje mlango kuhakikisha mdogo wako anatibiwa (kama nakumbuka vizuri ulimshikia panga mlezi wenu alipokuwa harespond chochote kuhusu kumpeleka mdogo wako hospital).......Ilinifanya nione how much ulikuwa unampenda mdogo ako; how exactly big sisters are.
Tunajikutaga sisi ndiyo kama mama wa wadogo zetu na sio madada tena. I know what she/he meant to you; she/he was the only thing left for you after you both lost your parents; you found strength and purpose to live just for her/him. I can imagine how her/her death has hit you. Daah yaani naona hata kutype "pole sana" ni kama daah. Mungu akutie nguvu dada mkubwa.
Please you need to do a closure. Hiyo hatia uliyonayo kwamba maybe hukumlinda ipasavyo ndiyo maana imefariki; inabidi iondoke sasa. Jisamehe kabisa
Kama unaweza kwenda alipozikwa; fika frequently. Mimina moyo wako; ongea yote ambayo unatamani umwambie hata kama hakusikii; I know utalia vya kutosha na kwa kiasi fulani utapata amani ya moyo.
Wakati wa mtu kufa ukifika; hakuna utakachoweza kufanya kuzuia mauti yasimpate. Amini tu wakati wake ulifika; na hata asingekufa kwa presha; angekuwa tu hata kwa ajali au malaria. His/her time was simply up.
Hata katika machozi na uchungu wako mkuu ulionao; usiache kumshukuru Mungu. Mshukuru Mungu hata alikupa Neema ya kuwa na mdogo wako kwa miaka yote hiyo aliyokupa; imagine asingekuwepo na huku wazazi hawakuwepo pia. Mshukuru Mungu amekuachia na mtoto wake wa pekee ambaye ndiyo kumbukumbu halisi ya mdogo wako. Mshukuru Mungu hata umepata nafasi ya kumuona kwa mara ya mwisho na kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele; at least unaweza kwenda kumtembelea kaburini kwake na ukafeel uwepo wake. Imagine wale ambao wapendwa wao wametoweka hawajulikani hata walipo; whether wapo hai au wamekufa; imagine familia zao zinaishi kwenye sintofahamu ya namna gani au unaambiwa tu ndugu yako wamepata ajali ya meli imezama, na miili yao haionekani. So ukija kuangalia; bado zipo sababu nyingi tu za kumshukuru Mungu katika hili pia. Take heart big sis; Mungu atakuvusha katika hili. Usiache kuomba, usiache kuongea na watu; toa yote yaliyo moyoni mwako. It shall be well with you big sis
Sent using
Jamii Forums mobile app
yAAAH!
Huyu was a son to me.
Watoto wangu walikuwa wanasema kabisa mama yani Uncle knows unampenda kiasi gani!
Mimi huwa napenda kuvaa raba na mashati ya draft over the weekend!
Ilikuwa tunavaliana na kununuliana.
Niliwahi kulazwa wakati fulani, nikawa naishi peke yangu.
Alihama nyumbani kwake na mkewe na mtoto wake, wakaja kukaa kwangu mwezi!
Ilikuwa anakuja hospitali anakaa hapo kitandani , mi nalala naamka namkuta!
Anafua nguo zangu, ananilisha na kuhakikisha nimeoga ndo anashuka chini anapiga story na walinziiii, ili wamruhusu awe anakuja kuniangalia usiku!
Mahala fulani nilidhulumiwa karibu 5m. Alipojua, alihakikishwa nalipwa na ya usumbufu , pesa niliyodai karibu miaka 3. Alihakikisha inalipwa ndani ya miezi 3.
Yani naomba nikwambie Oddo! Nashindwa hata kumlilia, sijui namliliaje!
Maisha yangu yamebadilika hasa.
Nimekuwa mtu mwingine sana!
Najikaza nacheka, natembea, nafanya projects zake aliachilia katikati!
Just kutamani kutimiza ndoto zake!
Bado najikuta nina ombwe.
Alikuwa ndo msiri wangu, kuna vitu nafkr nitavipoteza just because yeye hayupo!
Naomba sana niweze kuvuka hapa!
Ila Mungu wa Mbinguni anajua nimeondokewa na mtu wa aina gani!