Msaada: Mmewezaje kupona maumivu ya kufiwa na mtu wa karibu?

Pole sana mkuu. Ndio maisha. Sometimes inabidi kuishi na maumivu...With atime utakua sawa
 
Najuta kusoma huu uzi nikiwa kwenye daladala,nmelia sana ,kufiwa kuacheni nyie.pole ndugu
 
Katika umri wangu huu, unafikiri nimepitia mapito yaliyonyooka tu!! Kwa taarifa yako, nimepitia mapito mengi tu ya kimaisha! Na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, nimeweza kuyashinda.
 
Pole sana
Maumivu huwa hayaishi,ila huwa yanapumzika tu.

Amini amepumzika,Kuishi kwetu ni Kristo,Kufa ni faida.
 
sometimes huwa nawaza kheri nianze kuondoka mie ndo wafate wazazi wng..maana wakianza wao..sijui itkuaje..
Yarabbi tujaalie mwisho mwema na wazazi wetu.
 


Hii kitu ni changamoto sana na inaweza kukusababishia depression. Kitu cha kwanza kubali kuwa ni kweli si ndoto. Kitu cha pili badilisha namna ya maisha uliyokuwa nayo wakati akiwepo. Fanya marafiki wapya, anza kuishi upya. Usipende kukaa peke yako, kaa na watu wengi na ambao hasa hawajui lililotokea ili wasikupe pole au kukusikitikia na kukuonea huruma... Kama ni mtu wa kanisani nenda kanisani, imba kwaya, imba kwa sauti. Kama ni mtu wa dunia, nenda club kwenye kelele sana, cheza muziki, kidogo kidogo maisha yatachukua mkondo wake kadiri muda unavyoenda.
Nina ushuhuda na hili, mwaka 2011 nilifiwa na mwenza ambaye ilikuwa bado miezi miwili nifunge naye ndoa. Nilijikuta kama nataka kuwa chizi, shukrani kwa bosi wangu alivyogundua hili alinifanya kuwa busy kazini, kazi nyingi, kufoka mpaka nikaanza kuona nina changamoto kubwa sana ya kazi, na akawa hanipi pumzi. Baadaye akaja kuniambia sababu ya hayo na akaniambia sasa unatakiwa uanze upya na usipende kukaa peke yako. Leo 2023 ninaishi.

Mwisho nakupa pole sana mkuu.
 
Katika umri wangu huu, unafikiri nimepitia mapito yaliyonyooka tu!! Kwa taarifa yako, nimepitia mapito mengi tu ya kimaisha! Na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, nimeweza kuyashinda.
Sawa. Hongera, so kila mtu anajuwa ataponea wapi sio kila mtu afate ulipo uponyaji wa mwingine dunia pana sana hii mkuu. Nadhani hatuwezi kufanana.
 
Yaani pole sana nimelia kama vile nakujua [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Kwa kweli inasikitisha lakini hakuna kitu kinacho itwa coincidence, mambo yote yanafanyika kwa sababu, sasa my dear hao wapendwa wako wametangulia ili wewe uishi maisha mazuri kwenye hii Dunia yetu, jichanganye na watu smart, kama ni mfanya biashara au kazini au shuleni na ukumbuke your love ones wapo na wanakusaidia katika kila kitu!
Hata huu uzi pia umeanzisha ili upate namna ya kuishi, huu ni msukumo wao!
Kaa mbali na walevi na mijitu yenye tabia mbovu! Jaribu sana kutenda mema hata kama wakati mwingine una hasira, lakini kumbuka vitu vikishindikana nenda hospital na mwone psychologist ata kusaidia na wala usione aibu!
Kuna watu wengine wana shida katika hii Dunia na sio lazima kufiawa tu, kwenye mambo mengine!
Nakuombea kwa Mwenye Enzi Mungu mwenye wingi wa hekima asimame na asikie kilio chako,
Remain blessed in safe hands of The Almighty One [emoji3516]
 
Pole sana ndugu yangu kwa msiba huu mzito uliokupata! Kusahau siyo rahisi sana itachukua muda mrefu. La msingi ni kupambana na zile hisia ( maumivu, huzuni n.k) unazosikia wakati unapomkumbuka hizi ndizo zinazosababisha matatizo. Kulingana na imani yako lazima ujue mambo yafuatayo; Mwenyenzi Mungu afanyi makosa inatakiwa ukubali kwamba ni amri yake na kwenye hii dunia tunapita tu ni suala la muda. Ongeza sala za usiku kwa hakiki utapata faraja na matumaini mapya Inshallah!
 

Ni jambo gumu, ila jionee Huruma, and do your best kuwa na ukaribu na watu hasa Kanisani au msikitini, na kama ni Mkristo, kuna mistari mingi sana ya biblia ya kukupa tumaini.

The only way to change namna unavgofikiri ni kubadili fikra zako na maneno ya Mungu yenye kuleta tumaini, ukila hayo maneno mda mrefu hubadilika na kuwa hai na halisi.

Exchangw your sad mawazo na maneno na ahadi za faraja za Mungu, with time nakuhakikishia utapata faraja ya ajabu sana sana na utasahau shida.

Usikubali kuijaza hiyo hali na faraja zisizo faa za mahusiano na wanaume ambao wanaweza itumia hiyo nafasi kukutumia na kukucheze.

Mungu akusaidie dogo.
 
Pole sana Mkanaani
 
Kufiwa ni kitu Cha kawaida sana ila maumivu utayapata ila DUNIANI ni njia tu
 
Pole sana rafiki, najua ni ngumu ila Mungu wetu mkuu akupe faraja ya roho Insh Allah.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…