Sijui nimekuelewa, Nilichoelewa ni kwamba mumeo hana muda wa kukushirikisha/kujadiliana chochote hata kama kuna uwezekano wa kutokea hatari/madhara.
Nakumbuka hii hali nikiwa nakuwa mama alikuwa akilalama kutoshirikishwa au kutokuongea as family na mzee. Madhara yalionekana kwa baadhi ya mambo ambayo yalikuwa ndani ya uwezo wa mama ila kutokana na hali hiyo ilikuwa ngumu kwake kufanya chochote. Mzee kaja kuchange jua lishazama na mambo mengi yameshavurugika. Hata taarifa tu kumshirikisha mwenzie ilikuwa changamoto, ye ni kufoka tu baada ya madhara. Hii kitu mpaka nakuwa najitambua niliona mwenyewe mzee alikuwa anazingua kwanza hakubali kushaurika mpaka kesho hii tabia anayo, atatafuta solution baada ya mambo kuharibika ndio ataanza kusema sasa hapa tunafanyaje. Mambo mengi yamefeli kwa sababu hiyo.
Sio kila kitu ni cha kushirikishana/kuongea ila kuna mambo ambayo ni vizuri kushirikiana na mwenza wako kama familia.