Msaada mwenye connection ya ajira nchi za Kiarabu

Nimemaniisha hiyo biashara ya laki 5

Sijazungumzia laki tano, bali dola 1000=shilingi milioni mbili na laki tatu kumi na tano themanini na nane....ni mtaji tosha haswaa, na itakuingizia kipato kikubwa kuliko huo mshahara utakaopewa....ni kutuliza akili tu.
 
Miili 12 za Wakenya zililetwa na Ndege kutoka Saudi,Saudi wanatesa Waafrika Sana
 
Nimekaa nikafikilia maisha yamenipiga, kazi niliyokuwa nayo haikidhi kabisa mahitaji yangu ya kila siku, nina mke, nina mtoto, ninao ndugu wanao nitegemea, baba, mama na wadogo zangu mbaya zaidi mimi ndie kaka mkubwa wa familia, najiona kabisa nimeanguka, najiona napoteza uelekeo kila kukicha, nimekuja humu najua kuna watu wa hadhi na kariba tofauti tofauti, maana waswahili husema "mficha maradhi kifo humuumbua"

Nimehangaika kutafuta kazi, ni kweli nipo kwenye kazi ambayo mshahala ni 250k baada ya makato, huo mshahala unanifanya niishi kwa madeni hata kabla sijaupokea unakuwa teyari umeshaisha, sasa ndugu zangu kwa umri wangu huu 25+ najiona kabisa ndoto zangu hazitotimia, nikiwa na akili timamu ninaomba kwa yeyote mwenye connection ya ajira, ata ya ULinzi, na nyinginezo kwenye nchi za kiarabu haswa Doha, Qatar anisaidie pengine huko maslahi yanaweza kuongezeka.

Nimejaribu kufuatilia kwenye mitandao nakutana na maagency ambao wapo nchi za jirani inakuwa ngumu kwangu kuwafikia kwani wengi wao wapo Kenya ama Uganda.

Ndugu zanguni ni matumaini yangu kilio changu kiapatiwa ufumbuzi.

Elimu yangu ni ya kidato cha nne, sijasoma kihivyo ila ujinga wa kuelewa kingereza kidogo nimeuondoa hivyo ninaweza kingereza japo si sana.

Register then apply izo nafasi ukipata, thank me later. Salesman – Addify
 
Ok unatakiwa uwe na passport ya kusafiria
Passport size mbili zenye back ground nyeupe
Na yellow fever card ukikamilisha hapo kazi imeisha hyo mwezi mmoja upo Dubai
baada ya kuvipata hivyo...kazi nitaitoa wapi sasa maana lengo la kwenda huko ni kujitafutia maisha sio kutembea...
 
Kazi zipo we tafuta passport ila yule agent anataka hela kama laki 6 hivi utaangalia kama mtawezana nae kuna za sheli cashier na KFC store
 
unampa cash...ama atakukata kidogo kidogo...?
 
Anataka cash ila gharama zilizobaki zote anabeba mwajiri wako including flight tickets and accommodation kulala na usafiri wa kwenda kazini na kurudi
hapo itakuwa ngumu kidogo kwa upande wangu wallah ningekuwa ninauwezo wa kuimiliki hiyo laki 6 nisingehangaika kutaka kwenda nje...ningeitumia hiyo hiyo kama mtaji
 
Ok sawa mkuu ila mi nime kupa hints tu unaweza kupambana kivingine nadhani humu kuna wadau wengi sana watakupa mwangaza zaidi kikubwa uwe na passport tu
 
Nimekaa nikafikilia maisha yamenipiga, kazi niliyokuwa nayo haikidhi kabisa mahitaji yangu ya kila siku, nina mke, nina mtoto, ninao ndugu wanao nitegemea, baba, mama na wadogo zangu mbaya zaidi mimi ndie kaka mkubwa wa familia, najiona kabisa nimeanguka, najiona napoteza uelekeo kila kukicha, nimekuja humu najua kuna watu wa hadhi na kariba tofauti tofauti, maana waswahili husema "mficha maradhi kifo humuumbua"

Nimehangaika kutafuta kazi, ni kweli nipo kwenye kazi ambayo mshahala ni 250k baada ya makato, huo mshahala unanifanya niishi kwa madeni hata kabla sijaupokea unakuwa teyari umeshaisha, sasa ndugu zangu kwa umri wangu huu 25+ najiona kabisa ndoto zangu hazitotimia, nikiwa na akili timamu ninaomba kwa yeyote mwenye connection ya ajira, ata ya ULinzi, na nyinginezo kwenye nchi za kiarabu haswa Doha, Qatar anisaidie pengine huko maslahi yanaweza kuongezeka.

Nimejaribu kufuatilia kwenye mitandao nakutana na maagency ambao wapo nchi za jirani inakuwa ngumu kwangu kuwafikia kwani wengi wao wapo Kenya ama Uganda.

Ndugu zanguni ni matumaini yangu kilio changu kiapatiwa ufumbuzi.

Elimu yangu ni ya kidato cha nne, sijasoma kihivyo ila ujinga wa kuelewa kingereza kidogo nimeuondoa hivyo ninaweza kingereza japo si sana.

VILE VILE mimi ni dereva wa magari...mwenye leseni yenye daraja A, A2, B, C1, C2, C3, D, E

pole sana. lakini kuwa makini, kuna mijitu inawapeleka watu kwa njia zisizo rasmi na matokeo yake unageuka mtumwa kule uarabuni. utateseka mpaka ujute kuwaza kwenda uarabuni. ninasisitiza, nenda kwa njia halali. usikubali ule mtindo wa kushikiwa passport. usiingie ule mkataba eti ulipiwe nauli na boss kule arabuni, kisha passport unashikiwa,ukitaka kuacha kazi ulipe nauli. usikubali haya ndugu. bora ufe kwa shida hapa bongo. tazama hizi clips kupata uzoefu. Mungu akujaalie

Back
Top Bottom