Baada ya kufatilia sana, kuna kitu nimegundua. Makampuni mengi nchi za kiarabu wanaprefer zaidi wakenya kuliko watz.
Kuna agent wa Kenya ananishughulikia issue yangu, siku ya kwanza tu aliniuliza kuhusu passport yangu ni ya nchi gani, baada ya kumwambia ni ya bongo akasema nimtumie. Ni miezi sasa imepita but kila nikiongea nae anasema bado hajafanikisha kwani passport ndio kikwazo japo kanihakikishia kuwa ni 100% kupatikana kwa kazi.
Kwahiyo ndugu zangu, kama bado hujapata passport fanya mchakato upate ya Kenya. Kuna watu nikisema passport ya bongo au ya kenya hawaelewi, paasport ni ile ile but ombea kenya uwe kama mkenya. Ni rahisi sana kupata mchongo uarabuni ukiwa raia wa kenya