Msaada mwenye connection ya ajira nchi za Kiarabu

Msaada mwenye connection ya ajira nchi za Kiarabu

Wanakuwaga wagumu sana maana wa bongo wengi wazinguaji, unakuta mtu hana hata passport halafu anaenda agent wa Kenya ..kwa hiyo wanawakataa..halafu pia wanaweka bei juu sana kwa watz, unakuta hadi USD 1000 uko wakati kwa mkenya mwenzake ni 100 tu.
Wa Kenya wana roho mbaya sana! na wana wivu mkubwa kwa Wa Tanzania.

Kwa nini tuwe wepesi wepesi kuwakubalia yao? Na sisi tukatae!
 
nadhani sio wakati wa kuisikilizia Tanzania inaruhusu au hairuhusu. tunazidi kudumaa ndani ya hii inchi, ni muda wa kutoka na kupambana na kesho yetu.
Wanakuzuia airport. Bongo wana mambo ya ajabu sana. Wanataka wote tufie hapa hapa na njaa.

Kenya na Uganda hawana huu ujinga. Kila mtu yupo huru kufanya kazi popote.
 
Kijana tafuta fursa nje ya nchi acha uoga ..leo una miaka 28 kesho haitakuwa hivyo. Uoga wetu unatukosesha pesa huko nje ..wakenya wanapiga sana pesa.
Kuna mkenya juz alikua anaomba msaada, ni graduate wa univerisity, alienda kufanya kaz saudi arabia, aliua halali, anafanya kaz 24 hours, yaan analala 11:30pm na kuamka saa 4:00AM daily. Hiz nchi za kiarabu sio poa

Ameombaomba wakamleta nyumban, ubaya zaidi alikua anafanyishwa kaz na malipo hapati au akipata yamechelewa

Kingine pia, alikua haruhusiwi kutoka ndani, anafungiwa na cctv kamera juu.
 
Baada ya kufatilia sana, kuna kitu nimegundua. Makampuni mengi nchi za kiarabu wanaprefer zaidi wakenya kuliko watz.

Kuna agent wa Kenya ananishughulikia issue yangu, siku ya kwanza tu aliniuliza kuhusu passport yangu ni ya nchi gani, baada ya kumwambia ni ya bongo akasema nimtumie. Ni miezi sasa imepita but kila nikiongea nae anasema bado hajafanikisha kwani passport ndio kikwazo japo kanihakikishia kuwa ni 100% kupatikana kwa kazi.


Kwahiyo ndugu zangu, kama bado hujapata passport fanya mchakato upate ya Kenya. Kuna watu nikisema passport ya bongo au ya kenya hawaelewi, paasport ni ile ile but ombea kenya uwe kama mkenya. Ni rahisi sana kupata mchongo uarabuni ukiwa raia wa kenya
Kuna rafiki yangu wa Facebook.ni raia wa Kenya Sasa hivi yupo saudia ni mwalimu.anasema yeye alitumia wakala.
Nikamuuliza huyo wakala anaweza kumfanyia mpango mtanzania akasema HAWARUHUSIWI.
nikamuuliza kuhusu masuala ya ubaguzi.akasema umejaa tele.
 
Nimependa huu mjadala. Mimi pia mmoja wa watafuta ajira hasa Dubai. Dubai kwa sababu girlfriend yupo huko. Nimeanza kutafuta connection 2019. Agent wengi Bongo nishaongea nao. Hela watataja ni kubwa sana 1000 USD. Kuna mmoja nilimpata akapunguza ikawa 800 USD. Nilikubali akaanza process matokeo yake aliniibia Tsh 50,000/= aliniomba kwa ajili ya kuombea vibali Zanzibar sababu aliniambia lazima upitie Zanzibar kwa urahisi zaidi.
Yupo pia urgent wa Kenya huyo sio tapeli nimekuwa nikiwasiliane naye tangu 2019 kipindi Corona imepamba moto. Akawa anasema kwa sasa hakuna kazi. 2021 akapata urgent akasema nilipie 150k +15k kitu kama hicho msg ninazo.
Nimekuwa nijifunza sana kwa namna gani naweza kupata kazi na kufanya kazi huko Dubai hasa ya security sababu nilipata habari toka kwa girlfriend wangu kuwa kazi ya security dubai haitesi sana kama kazi zingine za helps.
Sasa kuna rafiki yangu kaniunganisha kwa rafiki yake ambaye atanipokea huko Dubai. Natafuta nauli mpaka Aprili nitakuwa dubai.
Vitu alivyoniambia muhimu kupata kazi ya security dubai
1. Passport travel
2. Passport size
3. cv one page
4. SIRA hii ni leseni unasoma huko Drm 1730
5. Uzoefu muhimu pia
6. Police clearance report utoke nayo huku
7. Medical clearance report utoke nayo
8. Hela ya mtumizi
Niongea kifupi kidogo. Ahsante
 
Back
Top Bottom