Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pole. Rafikiyo anagawa password so badilisha pass word na usimpe huyo ndio mchawi. Wahuni washa piga picha. Hapo pakuscan so wana enjoy tu wifiHabari wakuu,
Nimenunua Router ya airtel 5G (smart box), nimejiunga kifurushi cha unlimited cha 110,000/- kwa mwezi, nimepata changamoto ambayo hata airtel wenyewe wameshindwa kunisaidia.
Nimeona kuna tatizo kwenye kifaa chao mfano nilimuunga rafiki yangu kwenye simu yake ya Samsung s20, chakushangaza kwenye simu yake kuna QR code inayomruhusu kushare wifi yangu kwa mtu mwingine bila kutumia password, naomba msaada jinsi ya kuzuia mtu kushare wifi.
Kila nikiangalia kwenye connect list naona kuna users zaidi ya 10, mimi binafsi natumia simu na laptop pekee, nahisi rafiki yangu ame share kwa watu mwengine.
naomba msaada wakuu ili niweze kuwaondoa au kuzuia hili tatizo, nimajaribu kubadilisha password lakini kila nikimpa password rafiki yangu nashangaa baada ya muda users wanaongezeka, binafsi huyu rafiki tunafanya nae biashara ni lazima akija ofisini kwangu atumie wifi yangu.
Ikiwezekana muuzie vifurushi kimya kimya.Mwondoe huyo rafiki yako kwenye mtandao wako na kila kitu kitakaa sawa. Wewe ndio admin wa hicho kifaa chako, hivyo kumpa Access huyo rafiki yako kupitia password yako mwenyewe unampa mamlaka ya kuwa admin wa vifaa vingine ambavyo wewe hutaweza kuvidhibiti. 🤓