Msaada: Namna ya kumfundisha au kuishi na dada wa kazi kwa muda mrefu

Msaada: Namna ya kumfundisha au kuishi na dada wa kazi kwa muda mrefu

Kwanza ukimpokea dada mfanyie interview namaanisha muulize malengo ya yeye kuja kufanya kazi ni yapi? Ukiona mtu ana babaika kujibu jua huyo hakai maana hajielewi amekuja kufanya nini hata majukumu hawezi kufanya.
Mpe taratibu za nyumbani kwako ratiba nzima kuanzia kuamka saa ngapi, chakula kinaliwa saa ngapi kama una watoto mpe ratiba za watoto kula.
Kama ni mfanyakazi omba ruhusa hata wiki amka fanya naye kazi msichana anayejielewa ukifanyanaye kazi utamuona ni wa aina gani.
Mpe orientation ya mwezi mmoja haja cop mazingira rudusha.
Muhimu kabla hujaagiza msichana muombe Mungu akuletee mtu sahihi
Msichana usimnyanyase ila usiruhusu akuzoee sana. Ili ukitoa maagizo yanafuatwa

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Ahsante
 
Mtoa mada kama kazi anafanya kwa mda na ufanisi muache achezee simu
Muda mwingi anautumia kwa simu kuliko kazi, kuna siku muda wa kuandaa chakula cha mchana alikuwa kajilaza anachat bahati nzuri kuna mmoja aliwahi kurudi nyumbani ikawa nafuu nafuu akapika.. ila hata mtu mwingine akiwa jikoni wala hajishughulishi zaidi ya kuwa bize na simu
 
Tatizo Wanawake mnataka house girl afanye kila kitu nyie mbaki kuagiza kama wahindi. Mpe kazi kiasi na nyingine fanya wewe la sivyo ukiendelea kumshurutisha utalia wewe.
Kuna mgawanyo wa majukumu isipokuwa siku za kazi kuna wa kwenda shule.. yeye dada + anayemuangalia mgonjwa ndio wanabaki nyumbani muda mwingi mchana.
 
Kuna kipengere umekiruka,mtume kariakoo na mwenyeji huku nyuma kagua begi lake kuona kama kuna hirizi,huyu alieenda nae kariakoo akifika mtaa wa congo amchenge apotee,jioni wamtangaze ITV akitoka hapo akili zitamkaa sawa
Kwanink ukague begi lake?
 
Naona unapitia ninayopitia kwa sasa yani huyu hana simu hajui chochote nasubiri mwezi huu uishe nimrudishe maana unajikuta muda mwingi unatoa maelekezo yale yale yasiyoeleweka. Huyu wangu hadi kuoga ni lazima umwambie hadi.mswaki lazima umwambie achana na kazi kama kufua na kuosha vyombo lazima uje uvirudie na ana wiki tatu sasa
 
Habari ya jumapili wadau.

Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu, ninaomba msaada wenu tafadhali.

Nina dada ambaye ana umri wa miaka 19(lakini kimuonekano anaonekana ni mkubwa), lakini dada huyu hajui kazi za ndani iwe kuosha vyombo, kupiga deki au kupika.. Alipofika alielekezwa majukumu yake na akasema anayaweza.

Changamoto nyingine kubwa ni kuwa yuko bize mno na simu, kuchat na kuongea.. Mahali alipo kuna mabinti wengine lakini wana soma na mmoja anashughuli binafsi hali inayopelekea kukosekana msaada nyumbani kwani kuna mgonjwa anayehudumiwa na mtu mwingine na anahitaji uangalizi wa karibu.

Naomba mniwie radhi kwa uandishi ila ninahitaji sana msaada wenu.. Natanguliza shukrani.
Hakuna mfanyakazi hapo timua
 
Muda mwingi anautumia kwa simu kuliko kazi, kuna siku muda wa kuandaa chakula cha mchana alikuwa kajilaza anachat bahati nzuri kuna mmoja aliwahi kurudi nyumbani ikawa nafuu nafuu akapika.. ila hata mtu mwingine akiwa jikoni wala hajishughulishi zaidi ya kuwa bize na simu
Rudisha kwao tena bila taarifa. Hajitambui. Utapata mwingine tu hadi utashangaa
 
Huyo si mfanyakazi amekuja kutembea tu na kuona mji.

Tena muweke tahadhari kubwa na vitu vyenu hasa kama mapambo ya mama maana anaweza kuruka navyo.

Siku ya siku mumeamka yeye amemwaga manyanga na ameondoka na vifaa muhimu.
 
Kupata mdada ni kazi ngumu au labda mazingira niliyopo
Wadada wa kazi kupata imekuwa ngumu sana na kupata anayejitambua ni ngumu zaidi. Maana siku hizi wadada ndio wanga, wauaji, wasambaza magonjwa yaani mtihani tu. Pole sana, sometimes naelewa kwa nini wazazi wanapeleka watoto wadogo boarding
 
Rudisha kwao tena bila taarifa. Hajitambui. Utapata mwingine tu hadi utashangaa
Siku inayofuata aliniomba mwenyewe kuondoka kwa sababu eti mama yake anaumwa ilhali dada yake alisema ni muongo
 
Back
Top Bottom