Msaada: Namna ya kumfundisha au kuishi na dada wa kazi kwa muda mrefu

Huyo mrudishe hafai. Anayekuja kufanya kazi huwa anajipangia muda wa simu na muda kazi. Sasa huyo hajui kazi yoyote ni mzigo tu na hauwezi kumbadilisha
Ahsante kwa maoni.
 
Ahsante
 
Mtoa mada kama kazi anafanya kwa mda na ufanisi muache achezee simu
Muda mwingi anautumia kwa simu kuliko kazi, kuna siku muda wa kuandaa chakula cha mchana alikuwa kajilaza anachat bahati nzuri kuna mmoja aliwahi kurudi nyumbani ikawa nafuu nafuu akapika.. ila hata mtu mwingine akiwa jikoni wala hajishughulishi zaidi ya kuwa bize na simu
 
Tatizo Wanawake mnataka house girl afanye kila kitu nyie mbaki kuagiza kama wahindi. Mpe kazi kiasi na nyingine fanya wewe la sivyo ukiendelea kumshurutisha utalia wewe.
Kuna mgawanyo wa majukumu isipokuwa siku za kazi kuna wa kwenda shule.. yeye dada + anayemuangalia mgonjwa ndio wanabaki nyumbani muda mwingi mchana.
 
Kuna kipengere umekiruka,mtume kariakoo na mwenyeji huku nyuma kagua begi lake kuona kama kuna hirizi,huyu alieenda nae kariakoo akifika mtaa wa congo amchenge apotee,jioni wamtangaze ITV akitoka hapo akili zitamkaa sawa
Kwanink ukague begi lake?
 
Naona unapitia ninayopitia kwa sasa yani huyu hana simu hajui chochote nasubiri mwezi huu uishe nimrudishe maana unajikuta muda mwingi unatoa maelekezo yale yale yasiyoeleweka. Huyu wangu hadi kuoga ni lazima umwambie hadi.mswaki lazima umwambie achana na kazi kama kufua na kuosha vyombo lazima uje uvirudie na ana wiki tatu sasa
 
Hakuna mfanyakazi hapo timua
 
Rudisha kwao tena bila taarifa. Hajitambui. Utapata mwingine tu hadi utashangaa
 
Huyo si mfanyakazi amekuja kutembea tu na kuona mji.

Tena muweke tahadhari kubwa na vitu vyenu hasa kama mapambo ya mama maana anaweza kuruka navyo.

Siku ya siku mumeamka yeye amemwaga manyanga na ameondoka na vifaa muhimu.
 
Kupata mdada ni kazi ngumu au labda mazingira niliyopo
Wadada wa kazi kupata imekuwa ngumu sana na kupata anayejitambua ni ngumu zaidi. Maana siku hizi wadada ndio wanga, wauaji, wasambaza magonjwa yaani mtihani tu. Pole sana, sometimes naelewa kwa nini wazazi wanapeleka watoto wadogo boarding
 
Rudisha kwao tena bila taarifa. Hajitambui. Utapata mwingine tu hadi utashangaa
Siku inayofuata aliniomba mwenyewe kuondoka kwa sababu eti mama yake anaumwa ilhali dada yake alisema ni muongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…