Msaada: Naomba kupewa gharama za hatua hizi za ujenzi

Habari za kwenu wanajamvi,

Nakuja hapa nikiomba ushauri/msaada wa dhati kabisa juu ya ujenzi nina 15million ya kumalizia vitu vichache je itatosha? Na kwa sasa najua wengi wenu humu mna uzoefu na mafundi mpo humu, kwa mtu anaejua naomba kujuzwa nyumba yangu ina ukubwa wa 14.6*12.3 Squaremita na vyumba vinne, sasa nipo kwenye hatua ya finishing, naomba msaada wa kujua nyumba ya namna hii yenye vyumba vinne je gharama zikoje katika hatua hizi hapo chini;

Blundering
Kupiga plasta
Kufanya plumbing
Kuweka tiles
Wiringi
Kupiga rangi
Madirisha ya aluminium

Naomba usaidizi gharama za mafundi na materials zikoje?
Mkuu huo mzigo unahamia kabisa.
 
hapa wengi watakuchanganya kutokana na bei utakazoambiwa,binafsi nimeinua jengo la floor 1 wakati huo fedha niliyokua nayo cash ni m10 tu lakini nafanya vitu kwa awamu.nnachokushauri fanya vitu kwa awamu na kumbuka maneno ni tofauti na vitendo,
 
Unachosema ni kweli, awali nilianza mdogo mdogo kuanzia msingi mpaka kwenye kuezeka kwa kuwa nilikua makini, sasa hii stage kwangu mimi ni stage yenye kuhitaji umakini wa hali ya juu, nafanya data collection kulingana na ubora wa kitu nachotaka kufanya ni ngumu kuchanganyikiwa kupokea mawazo mbalimbali bali nachuja nipate mawazo mazuri
 
Tiles inategemea unataka Spanish au Mchina.
Mchina grade 1 sitting room 50*50 ndio zinapendeza box moja 30,000-35,000/- box moja sqm 1.5. Sitting room yako 20sqm utahitaji 14boxes ambayo ni 490,000/-.
Fundi anachaji sqm moja 5,000/-
Hapo kwenye tylis namshauri anunue spanish mi nilinunua mchina rangi crem ilopauka kadri kunavyodekiwa zinazidi kuwa nyeupe saa hivi nina mpango wa kung'oa zile za siting room na kordo
 
Habari za kwenu wanajamvi,

Nakuja hapa nikiomba ushauri/msaada wa dhati kabisa juu ya ujenzi nina 15million ya kumalizia vitu vichache je itatosha? Na kwa sasa najua wengi wenu humu mna uzoefu na mafundi mpo humu, kwa mtu anaejua naomba kujuzwa nyumba yangu ina ukubwa wa 14.6*12.3 Squaremita na vyumba vinne, sasa nipo kwenye hatua ya finishing, naomba msaada wa kujua nyumba ya namna hii yenye vyumba vinne je gharama zikoje katika hatua hizi hapo chini;

Blundering
Kupiga plasta
Kufanya plumbing
Kuweka tiles
Wiringi
Kupiga rangi
Madirisha ya aluminium

Naomba usaidizi gharama za mafundi na materials zikoje?
Mkuu nakushauri anza na blandering na plumbing na plaster na tylis na wirering hizo aluminium fanya mwisho maana zinakula sana hela na vile vile kwa upamde wa madirisha inategemea ni ukubwa gani maana didisha la aluminium 5×6 mi walinitengenezea kwa 2800000 sasa kama yako yana ukubwa zaidi ya hapo ujue ni laki 3 na point hivi. Hivu vingine sio gharama kiviile ni uoga wako hela yaki ni nyingi sana kama ukiipangilia vizuri
 
Hapo kwenye tylis namshauri anunue spanish mi nilinunua mchina rangi crem ilopauka kadri kunavyodekiwa zinazidi kuwa nyeupe saa hivi nina mpango wa kung'oa zile za siting room na kordo
Tatizo ni kwenye kupoteza mng'aro na hasa hizi za kichina ndiyo zina shida, spanish sio mbaya, ila kuna mdau humu alinishauri za india anasema ni nzuri sana na zinabaki na ubora wake kwa muda mrefu sana
 
Mkuu nakushauri anza na blandering na plumbing na plaster na tylis na wirering hizo aluminium fanya mwisho maana zinakula sana hela na vile vile kwa upamde wa madirisha inategemea ni ukubwa gani maana didisha la aluminium 5×6 mi walinitengenezea kwa 2800000 sasa kama yako yana ukubwa zaidi ya hapo ujue ni laki 3 na point hivi. Hivu vingine sio gharama kiviile ni uoga wako hela yaki ni nyingi sana kama ukiipangilia vizuri
Mkuu madirisha yangu yana ukuwabwa wa 5*5 kasoro master room tu ndiyo 6*6 grill kijana anataka 150 grill peke yake, vipi wewe kwa hiyo pesa ni complete grillna aluminium?
IMG-20180510-WA0002.jpeg
 
Hapo kwenye tylis namshauri anunue spanish mi nilinunua mchina rangi crem ilopauka kadri kunavyodekiwa zinazidi kuwa nyeupe saa hivi nina mpango wa kung'oa zile za siting room na kordo
Mimi niliweka Mchina grade one, 50*50 mwaka wa pili huu zipo vile vile.
 
Weka vipaumbele muhimu kwanza;
1. Grill za milango na madirisha, @120,000/- dirisha na @180,000/- mlango wa mbele.
Hivyo, 120,000x11=1,320,000/- + 180,000/- =.....
2. Wiring materials inaweza cost 1,500,000-2,000,000/- kila kitu kutegemeana na quality ya wiring unayotaka.
3. Plumbing pia ni relative, andaa 1,000,000/-
4. Floor, mchanga gari moja @120,000/-, cement 15-20bags @14,000/-(sijui maeneo yako bei ikoje)
5. Blundering, unaweza kupiga nyumba nzima ili usije kugonga manyundo baadae, inaweza kufika 1,500,000/- kwa nyumba yote.
6. Plastering ndani na nje, gari mbili za mchanga @120,000/-, cement 30-35bags @14,000/-.

Fanya mahesabu, ukifika hapo unaweza kutimba ndani, the rest utamaliza taratibu coz hiyo 15m hauitatosha gypsum boards, skimming, rangi, tiles, PVC board na aluminium windows.

Hongera kwa hatua hiyo mkuu.
 
Tatizo ni kwenye kupoteza mng'aro na hasa hizi za kichina ndiyo zina shida, spanish sio mbaya, ila kuna mdau humu alinisahauri za india anasema ni nzuri sana na zinabaki na ubora wake kwa muda mrefu sana
Nakushauri usifikirie tiles wala aluminium windows kwa sasa, fanya yale muhimu kwanza as umesema unataka kuingia ndani.
Grills za madirisha na milango, wiring, plumbing, floor, blundering, plastering, then kama pesa ipo bado weka gypsum boards, skim ndani na nje, weka milango ya mbele na nyuma....
Kwa mtiririko huo, Ila kama unataka umalize chumba kimoja kimoja hapo sawa.
 
Hivyo vyote ulivyomtajia hapo juu approximately ni 8m, yeye ana 15m. Atabaki na 7m anaweza kuweka aluminium na gypsum kwa hela inayobaki.

Kwa nyumba ya kawaida ambayo ishaezekwa 15m finishing inatosha sana.
 
Nyumba yake sio ndogo, almost 180sqm lazima materials na ufundi vitamkosti. Ingekuwa mimi ningeweka tiles kabla ya aluminium, aisee lile vumbi la rough floor noma sana.
 
Mkuu madirisha yangu yana ukuwabwa wa 5*5 kasoro master room tu ndiyo 6*6 grill kijana anataka 150 grill peke yake, vipi wewe kwa hiyo pesa ni complete grillna aluminium? View attachment 778796
Kwa size ya dirisha lako kwa upande wa grill huyo fundi anakupiga bei hiyo ghali sana mafundi wapo kibao unapata mpaka kwa 120000 tena flat bar ya 4mm '1' kwa upande wa aluminium size ya dirisha hilo fundi ni 250000 mkishushana ni 235000 mafundi kipindi hichi wana njaa sana lia nao
 
Weka vipaumbele muhimu kwanza;
1. Grill za milango na madirisha, @120,000/- dirisha na @180,000/- mlango wa mbele.
Hivyo, 120,000x11=1,320,000/- + 180,000/- =.....
2. Wiring materials inaweza cost 1,500,000-2,000,000/- kila kitu kutegemeana na quality ya wiring unayotaka.
3. Plumbing pia ni relative, andaa 1,000,000/-
4. Floor, mchanga gari moja @120,000/-, cement 15-20bags @14,000/-(sijui maeneo yako bei ikoje)
5. Blundering, unaweza kupiga nyumba nzima ili usije kugonga manyundo baadae, inaweza kufika 1,500,000/- kwa nyumba yote.
6. Plastering ndani na nje, gari mbili za mchanga @120,000/-, cement 30-35bags @14,000/-.

Fanya mahesabu, ukifika hapo unaweza kutimba ndani, the rest utamaliza taratibu coz hiyo 15m hauitatosha gypsum boards, skimming, rangi, tiles, PVC board na aluminium windows.

Hongera kwa hatua hiyo mkuu.
Ufafanuzi mzuri na bora kabisa hivi ndiyo nilikua nataka mkuu yani umetembea ndani ya mstari umejaribu kugusa hitaji langu, maana lengo ni kupata mwanga kwa kile ninacho tarajia kukifanya kulingana na bajet, ahsante mkuu, hivi hapo kwenye blundering hiyo ni bei ya material tu na fundi je? Pia kawa ukubwa wa nyumba yangu plasta ndani na nje kwa material na gharama za ufundi.....
 
Back
Top Bottom