ERoni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2013
- 48,052
- 104,677
Ufafanuzi mzuri na bora kabisa hivi ndiyo nilikua nataka mkuu yani umetembea ndani ya mstari umejaribu kugusa hitaji langu, maana lengo ni kupata mwanga kwa kile ninacho tarajia kukifanya kulingana na bajet, ahsante mkuu, hivi hapo kwenye blundering hiyo ni bei ya material tu na fundi je? Pia kawa ukubwa wa nyumba yangu plasta ndani na nje kwa material na gharama za ufundi.....
Mkuu, hizi bei ni za kitaa, ukitaka kuumia tumia mafundi wa masaki huko, utaumia sana. Blundering kwa vile umesema haina madoido makubwa sebleni, possibility ya 2x2 za 700,000-800,000 kutosha ni kubwa, then ukikutana na fundi wa kitaa akikupiga 400,000-500,000 kazi inaisha, tena hadi blundering ya nje.
Kwa uzoefu wangu, kwenye plaster nyumba hiyo ufundi tu inaweza kufika 1,200,000(nje -ndani) au zaidi kutegemeana na maelewano. Weka 40-50bags za cement, gari mbili za mchanga(fuso) coz moja hatotosha. Hivyo 50x14,000/-=700,000+240,000+1,200,000= ....hapo bado maji, mbao za kench ili fundi afikie juu.