Msaada: Naomba nijue stahiki za watoto wangu

Unastahili Pole mkuu.....
Chochote kile kilichotokea pole.
Jiulize kipi bora Watoto wako walelewe na mumeo au wewe? Wapi unaona watapata mahitaji yote muhimu?
Afya, chakula, malazi, mavazi n.k
Kwanini muwaweke kwenye tabu ambayo hawakuistahili wala kuichagua.
Wapeleke kwa baba yao, wawe wanakuja kukutembelea weekends au wewe kwenda.
Endelea na biashara zako ukuze kipato chako, siku moja na wewe utakuwa mtu.

Kuwapenda watoto sio kuwakumbatia uonekane mpambanaji, kuwapenda ni kuwachagulia kilicho bora kwa manufaa yao.
Unavyoendelea kuwakazania inaonesha unataka pesa ya matumizi ya watoto uipige ( hata kama sio hivyo).
 
Pole sana
na umesema mtoto wa engeneer hawez kulelewa na mama mpika vitumbua?? HII KAULI YAKO ULOVYOIANDIKA ULIIONA IPO SAHIHI MKUU??
Naomba unisamehe sana!.
KWAN WANGAPI WAMESOMESHWA KATIKA MAZINGIRA MAGUMU NA WAKAFANYA VIZUR?
Ni kweli samahani sana
Kitendo cha kutoa matumizi ni kujali na kujali ni kupenda.
NAPAMBANA KWAAJILI YA WANANGU SIJASOMA NMEISHIA FORM FOUR ULITAKA NIIJIUZE NILEE WANANGU???
Pole na samahani tena
NILIJUA UNGEPONGEZA JUHUDI YA KUHANGAIKA WANANGU WALE UNAKUJA KUSEMA MTOTO WA ENGNEER HALELEW NA MAMA MPIKA VITUMBUA REALLY??
Pole na samahani sana
KAUL YAKO IMENIUMIZA SANA .
Pole sana sana sana, mimi ni mwanaume niliotendwa hivyo nikaside na mumeo nikijua ulimtenda, kumbe umeolewa na mtoto wa mama!. Pole!
..ANGEWAPENDA WANAE ANGEWAJALI SIO KUNISUSIA MIMI WATOTO ..
Pole tena na pambana.
P
 
Ndoa ni upendo, kama hakuna upendo basi hakuna ndoa.
Shida yetu sisi binadamu hatujui kuwa ndoa ni ya mke na mume (ya watu wawili).
Ukianza kuweka mawazo ya watu wengine ndoa lazima ivunjike.
Mama mkwe, baba mkwe (wa pande zote mbili) na wengine hawana amri kwenye ndoa.
Huko kujipendekeza ni jambo zuri ila ni baya sana kwasababu mama mkwe hana amri yoyote kwenye ndoa ya mwanae.
 
😳😳😳😳😳😳😳
Duuuuh!! Kazi mnazo!!
 
Hao ndio hufia ndoani kisa kujipendekeza wasikotakiwa.
 
Hee mkuu shida yote hiyo ya nini?? Huo muda wa kufanya yote hayo kwa watu wasiokupenda si bora akawekeza nguvu kufanya kazi ajikwamuw kiuchumi???
 
Amwachie mtoto wa mwaka mmoja na miaka 3?? Hao wote si bado wanahitaji malezi ya mama mwingine ananyonya kabisa?? Sema aangalie namna ya kutatua shida hiyo ili isiwaathiri watoto
Ndio
Si jamaa anasema ana hela na anawataka watoto wake?amwachie tu,hata akiwatesa si wanae?
Yani uishi kwa mateso,mume hakutaki,ndugu wazazi wake hawakutaki,halafu unaendelea kukomaa👁️atakufa kwa stress awaache hao watoto yatima
Awaache waende,akipata nafasi ya kuwatembelea,sense,full stop🙏
 
Unasemaje amewasusa watoto wakati ameomba awalee yeye kiasi cha kwenda kufungua shauri ustawi wa jamii?
Kuna kitu kimejificha katika maelezo yako. Something fishy ...

Yaonekana wewe 'umewang'ang'ania' watoto ili hali huwezi kuwahudumia.
Unatufanya tutamani kuhoji kwanini ndugu wa mume wakukatae hivyo?
Ulimtenda nini huyo mdau? Au ulikuwa na tabia gani kwa mumeo na nduguze?

Samahani kama nimekukwaza.
 
Hee mkuu shida yote hiyo ya nini?? Huo muda wa kufanya yote hayo kwa watu wasiokupenda si bora akawekeza nguvu kufanya kazi ajikwamuw kiuchumi???
This attitude!!!
Kuna wakati inabidi ujitoe (sacrifice) kwa ajili ya wanao kama kweli unawapenda.
Huo muda wa kwenda kuwekeza usiwe wakutesa wanao. Waache waende kwa baba yao jitafutie wewe na ukifanikiwa ziada utakuwa na uwezo wakuhudumia wanao baadae.
 
Shida iko wapi baba kuchukua wanae?
Kaeni chini muongee, jishushe maana nawe inaonyesha una mdimo mrefu kama walivyo akina mama ntilie
 
Pole sana aisee ,wanawake saa nyingine tunapitia mambo magumu sana hasa ukishakuwa na wattoto.Mimi nilijisemeaga mwenyewe kabla sijapata mwenza naomba Mungu unipe uwezo wa kusimama na miguu yangu miwili na alinisikia ingawa sijawahi kutendwa na mwenza wangu.Huwa nawafundisha watu jinene unachotaka kuwa ,fanya kazi kwa bidii ,focus mshirikishe Mungu muumba wa yote.Kwa sheria za Tanzania ,naona umeshapewa ushauri wa namna ya kukabiliana na hiyo hali.Angalia sasa usiongeze mwingine maana wanawake bana tukibembelezwa kidogo tu tunajisahau sana tunaanza kuwasingizia wanaume na maisha.Pole mwaya
 
Hapa nakupa 95% majibu ya busara sana

Japo kwenye siasa hutumii hizi akili bwana paschal Mayalla
 
Kwani tabu nini bibi eeh
Leo watoto wote peke yako acha kelele na mtu

Kama huwezi kulea
Mwachie awalee kwa ustawi wa maisha yao ya leo na kesho

Kama unawatumia kama sehemu ya kupata hela za kuendesha maisha yako hakika hutowasaidia zaid watapitia ugumu ambao si stahiki yao.

Ushauri chanya na wa mwisho.
Ka chin na mme wako wa zamani myajenge pasipo mashindano na pasipo kutaka kujikweza. Hakika hakuna litakaloshindikana.
Ukafanikiwe kwa ustawi wa maisha bora ya watoto hao

MAHAKAMANI KUNA HAKI
MTAANI KUNA BUSARA
 
 
Wanawake wajuaji kama wewe hiyo ndio dawa yenu, na hapa unajifanya kutafuta huruma kwa kumsemea baba wa watoto wako.
Ni dhahir umewaingiza watoto wako kwenye mgogoro wenu na mwanaume wako, then mlipo tofautiana na kuachana ulijifanya kung'ang'ania watoto wakati kama kinga ili uweze kuendelea kuhudumiwa (wakati hauna uwezo wa kuwahudumia).
Na inaonyesha unavyo tafuta huruma kwa kutuambia kwamba baba watoto wako ni Engineer alafu wewe unapika vitafunwa. Inaonekana ulishauriwa na wajinga wenzako na leo unapitia magumu na wamekaa pembeni.
Minasemaga hivi.....
Ukimuona mtu analeta simulizi za mgogoro wake kwa kisingizio cha watoto kukosa haki, basi huyo mtu mtazame sana... maana inaelekea hata wazazi pamoja na ndugu wamemshindwa huyo mtu anar tafuta huruma sasa mtandaoni.
Haya mpigie Doroth Gwajima kwa 0734124191 / 0765345777 ili upate msaada kabla ya kwenda huko unapo jidanganya utapata msaada (mahakamani), kwani nao watakurudisha ustawi wa jamii.
 
Not attitude mkuu, kusacrifise kwa ajili ya watoto wake sio kwa kujishusha mpaka udharaulike sasa. Kweli kujipendekeza kwa mama mkwe ambae hakupendi ili mwanae atoe matunzo kwa damu yake does it sound right?? Kwanini upendo uwe wa upande mmoja??
Hapo cha msingi baba na mama should grow up wajue majukumu yao trust me hakuna maisha magumu kama kuolewa/ kuzaa na mtoto wa mama yaani ni kama umeengage na mama yake.
 
Na sio kila baba anaweza kulea mkuu, wengine anataka kuchukua mtoto simply sababu ya visasi vya ugomvi wao.

Nina mfano wa rafiki yangu baba mtoto alichukua mtoto yeye hawezi kumlea akampeleka kwa mama yake ( bibi) huko mtoto alikuwa anafungiwa ndani na funguo bibi anaenda kwenye shughuli zake na mtoto ni mdogo bado vipigo visivyoendana na umri wa mtoto. Hadi siku mtoto akapiga simu kwa mama njoo unichukue sitaki kukaa huku.
Kuacha mtoto akakae kwa baba yao ninsawa lakini jee watoto watapata malezi stahiki??
 
Hee mkuu shida yote hiyo ya nini?? Huo muda wa kufanya yote hayo kwa watu wasiokupenda si bora akawekeza nguvu kufanya kazi ajikwamuw kiuchumi???
For me and my kids sake I would do that bila shida kabisa.

Ni bora nionekane mjinga kuliko watoto wangu kulelewa na mama wa kambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…