kolelosi
JF-Expert Member
- Jun 16, 2015
- 814
- 1,940
(@)Mama D ni kweli kabisa kwa ugonjwa aliokuwa nao alihitaji faraja sana hasa kuanzia watu wa karibu anaoishi nao (wauguzi) pia na watu wenye kufatilia kila hali anayoipata hasa wakati analalamika kuhusu kero za dawa.Unaweza ukawa na shida ya ugonjwa lakini shida ya upweke ikawa kubwa zaidi kuliko ugonjwa.
Huyu kijana ni kama faraja yake alikua anaitafuta jamiiforum, huko alipokua alikosa watu wa karibu wa kushare nao anayopitia, wangekuepo wangempa faraja, wangemshauri na wangemwonyesha upendo
Pumzika kwa amani
Alionekana hakuwa na watu makini wanao mzunguka zaidi ya kupata ushauri hapa JF ila kama kawaida baadhi ya member humu wameweka utoto na utani kwenye matatizo ya watu.
Wengi wao utakuta hawajawahi kukumbana na matatizo ya kuugua au kuuguza wakaona hali halisi ya muombaji ushauri (msaada). Tabia hii ya ku beza matatizo ya watu ife waungwana ni bora kukaa kmya kuliko kujimwambafai.
Sent using Jamii Forums mobile app