Msaada: Nataka kwenda Ustawi wa Jamii, baba wa watoto ananisumbua huduma

Msaada: Nataka kwenda Ustawi wa Jamii, baba wa watoto ananisumbua huduma

Pambana lea mwanao, achana nae.

Ushawahi ona jogoo analea vifaranga? Wanaume hawaleagi, its nature....atahudumia mtoto Kama na wewe unamuhudumia, Kama uko tayari kufata matumizi ya mtoto guest endelea kumsumbua, Kama unajali utu wako pambana mwenyewe.....mlezi mkuu ni Mungu, mtoto atakua tu bila yeye.

Angalizo, akileta matumizi usikatae na usimlishe mtoto sumu kumuhusu.
Hawezi kuelewa huyo mwanamke anaonekana kabisa tamaa mbele. Amefatilia mpk mshahara wake anajua kwaio anataka afaidike kupitoa mshahara wa jamaa,
Wewe dada acha tamaa
 
Jaribu kutafuta maelewano na mzazi mwenzio, sidhani kma kuna mwanaume anakataa kuhudumia damu yake kirahisi unless kama kuna sababu ambazo hatuzijui zinazomfanya asitoe huduma, either kauli au visa, wanawake tuna visa na maneno makali sana kwa hawa ambao tunataka wahudumie watoto, hatuwapi heshima wala nafasi ya kuwaona watoto na wakati mwingine tunajaribu kuwaharibia hata maisha yao kwa sababu ya ugomvi usio na sababu

Trust me, ukienda huko ustawi unaweza pata msaada lakini mwanaume akasema uwezo wake ni.kutoa elfu kumi kila mwezi na ustawi hawawezi kumlazimisha kutoa pesa zaidi ya hiyo kwa sababu nae ana majukumu yake mengine nje ya hao watoto kwa hiyo ni bora ukatumia hekima na husara kuweka mambo sawa na huyo mwenzio kwa faida ya watoto wenu. ustake maisha ya kukommoana eti kisa anapokea 2.8
Njoo hapa karibu na kwako nikununulie nyama choma na bia bardiiiii!!!!
 
Bro unapomtukana mtu usiyemjua huwa unafaidika nini.. ? nimeshare experience niliyopitia na wengi wanapitia hayo kwenye jamii hasa za waafrika labda kama unazibaga masikio na macho.. Nakupa tu angalizo usimtukane mtu usiyemjua.. karibu sana canada napoishi ila nazurura nchi nyingi duniani.. 🤣
Nmekutukana wapi ? Ungetukanwa ungesema wewe
 
Weee mim nnae hapa muda wote mdomo unatafuna unataka kula
Yaan huwa na kaz ya kujipilikisha maandaz au kalimati tofauti na msosi ili apate na vya kula kula wakija wengine hataree
Halaf unapangiwa vya kupika na aina ya juice unapangiwa na kukosolewa juu
Akiii inabidi ukiwa na hamu na juice fulan utengeneze yako na yake utengeneze anavyopenda huwa nachoka mie
Wewe ulishaambiwa masharti uliyokuwa ukimpa mama yako au mlezi wako kuhusu vyakula?
Hayo malezi unayompa yanamfaa yeye ama wewe?
 
Jaribu bi mdogo miye binti yangu kampeleka huko na amishia kupewa barua za wito kumi na mbili jamaa haji na hawamfanyi kitu.
Ushauri nenda kituo cha msaada wa kisheria kwa wanawake WILAD wamburuze mahakamani.
Ama kweli wazee wa siku hizi wanapaka piko ili mvi zisionekane na hivyo kukosa hekima.
Unajua walimzaa mzaa mtoto wao ktk mazingira na makubaliano gani?
 
Ulizaa mtoto Kwa kuhitaji uwe na mtoto au kumridhisha huyo mwanaume?

Lea mwanao! Angekufa ungeenda kulishtaki kaburi?

Fanya kama hayupo, Lea bila huzuni, ona mwanao ni baraka kuu.

Sali na mtegemee Mungu, atakupa riziki ya mtoto wako.

Ukianza habari za ustawi wa jamii, utapauka Kwa stress, huo muda angalia shughuli ya kufanya.

Mwanaume wa kweli na mtu mzima, hakumbushwi kulea damu yake.
Umemaliza yote niliyotaka kusema🙏isitoshe asiishi akiuwaza mshahara wa mwanaume atakufa kwa stress,Mimi mwanzoni nilizinguana na baba watoto kuhusu mahitaj ya watoto,yeye Yuko private firm,akasema wewe uko serikalini unanizid kipato,nikaona isiwe kesi nikaacha kumwuliza lolote kuhusu mahitaji ya watoto.

Miaka ikasonga nikapata challenge kazini tukakubaliana watoto wakachukuliwa na wazazi wake,wanaishi vyema tu,wanakula watakacho,wanasoma, kifupi they're happy,hakuna grudge kati yetu,kifupi tunawalea kwa amani,nachopambana nacho ni upweke tu wa kutoishi nao🙏.

So apambane alee watoto na asiuwaze mshahara wa jamaa atakufa awaache wanae yatima.
 
Naombeni msaada nataka kwenda ustawi, baba wa watoto huduma ananisumbua maana ni mfanyakazi TANESCO Engineer Grade 1 anapokea 2.8. Sasa naombeni msaada - Je, kwa mshahara huo naweza pata elfu 50 ustawi au wanadanganya?
Usiskilize maneno ya watu hapa jf wewe nenda watamuuta na utasaidiwa . Hiyo inaitwa maintenance. Ipo kwenye sheria ya ndoa . Utapewa zaidi ya 5 cause jamaa ana uwezo
 
Weee mim nnae hapa muda wote mdomo unatafuna unataka kula
Yaan huwa na kaz ya kujipilikisha maandaz au kalimati tofauti na msosi ili apate na vya kula kula wakija wengine hataree
Halaf unapangiwa vya kupika na aina ya juice unapangiwa na kukosolewa juu
Akiii inabidi ukiwa na hamu na juice fulan utengeneze yako na yake utengeneze anavyopenda huwa nachoka mie
Mbona unamsema hivyo mwanao. Mtoto kupenda kula ni baraka.
 
Naombeni msaada nataka kwenda ustawi, baba wa watoto huduma ananisumbua maana ni mfanyakazi TANESCO Engineer Grade 1 anapokea 2.8. Sasa naombeni msaada - Je, kwa mshahara huo naweza pata elfu 50 ustawi au wanadanganya?
mtoto ni wako dada pambana nae tu hakuna namna, sawa elfu hamsini ni kubwa kama huna na ni ndogo sana ukizingatia mpaka umpeleke ustawi wa jamii kwa ajili ya elfu hamsini
 
Sasa mwembamba mrefuu acha ale anenepe tu siku hizi kaanza nenepa angalau ,acha ale tu halaf anapenda vitu vya kukaanga na kachumbari ananimalizia mafuta huyuuu 😂😂😂
Pole ila vitu vya kukaanga usimzoeshe sana, bado mtoto anakua jitahidi ale mboga za majani kwa wingi, vyakula jamii ya wanga vimpe nguvu na vya protini kwa wingi vimjengee kimwili na akili

Bites asizifanye ndio mlo, ale bites vetween meals

Nimeconnect dot tu 😃😃
 
Kuna wakati huwa nashindwa kuwaelewa Wanaume wenzangu, hivi inakuwaje unashindwa kulea damu yako?
Mkuu, haya mambo yana changamoto sana.

Sisemi kwamba muanzisha Uzi amesababisha Mwanaume kutelekeza Mtoto, lakini, nyakati nyingine unaweza kuta Mwanamke ndiye aliyesababisha hali hii kwa kumtenganisha Baba/Mwanaume na Mwanaye kwa sababu mbalimbali, ikiwemo kumkomoa Mwanaume, kiasi hata cha Mwanaume kuambiwa Mtoto siyo wake.!!!

Siyo mara zote Wanaume wasiolea damu zao, wamezitelekeza kwa kukimbia majukumu bali imewalazimu kufanya hivyo, ili nao, maisha yaweze kusonga mbele. Maana, kama wangeendelea kulazimisha, wangekufa kwa stress.

Ni jambo la kushangaza, lakini ndiyo hali halisi inayoendelea kwenye Jamii.
 
Kuna wakati huwa nashindwa kuwaelewa Wanaume wenzangu, hivi inakuwaje unashindwa kulea damu yako?

Imagine huyo Dada yupo tayari kupokea hata shilingi 50,000 kwa mwezi. Hiyo elfu 50 inatosha Kula, mavazi au mtoto akiugua kweli? Kwa hiyo elfu 50 huyo Mtoto atapata Sare za shule au hata Kalamu na Daftari akianza shule?

Tuweni na huruma wakati mwingine, wewe usingehudumiwa na Baba yako ungefika hapo ulipo kweli?

Kama hauko tayari kulea Mtoto, niwasihi Wanaume wenzangu ni bora kutumia Kondomu au mtumie uzazi wa mpango. Tutakuja kupata dhambi na laana za Uzeeni kwa kutelekeza damu zetu.
💯🤗🤗🤗
 
Back
Top Bottom