Msaada: Nataka kwenda Ustawi wa Jamii, baba wa watoto ananisumbua huduma

Msaada: Nataka kwenda Ustawi wa Jamii, baba wa watoto ananisumbua huduma

Yaàni ni maboss kwelikweli,mtu anapanga masharti Utasema yeye ndio mwenye hiyo nyumba,ukipika maharage anasema sitaki nataka nyama,ukipika nyama anasema nataka Chipsi,ukipika Chipsi anasema nataka samaki aaaaaah hakika hutu tuviumbe ni tusumbufu Sana....Nina kamoja hako kananimbiaga "mama,hii juice sijaipenda"yaàni hapo mie nimejipinda najua katafurahi ,naishia kuchokaa😁😁😁
Watoto wapo real sana na wanakuaga na honest opinion. Anasema kitu kwa ukweli na si kwa lengo la kumfurahisha au kumkera mtu.

Hapo kwenye kutokupenda juisi amenikumbusha chuo DIT kunakuaga na mwanafunzi ambaye kazi yake ni kukagua vyakula vya cafeteria na canteen zote, akisema viko poa ndio vinauzwa kwa wanafunzi, akisema haviko poa, haviuzwi. Jamaa utasikia ameonja supu halafu anasema, hiki kiwango cha chumvi sijakipenda, ipo mbali sana ongeza😀😀
 
Nenda kwa bosi wake ongea nae
Kisha nenda ustawi
Sheria zetu hazimlindi mwanamke na mtoto asa huko ustawi waseme 50 inatosha nin?? Na watoto wanakula kama mchwa

Hapo hesabu itakuwa mtoto anakula kiwis gani Kwa Siku, kisha Kwa mwezi,
Kama ni 100,000/= basi Mama atatoa 50k na Baba 50k na sio zaidi ya hapo.
Ishu ya shule au matibabu mtoto alipiwe bima na wote Baba na mama wachangie hiyo bima, halikadhalika na Ada.
Mambo ya 50/50 ni magumu na Mabaya Sana ni vile Watu hawajui.
Ni magumu Kwa Wanawake wenye vipato vya Chini.
 
iko hivi mimi nmeolewa na tuna miaka 4 na nusu ya ndoa now nina miaka 24 ex husband ako na 31 ...ye ni engneer tanesco kipindi tunaowana sikukaa sana naona ni saba ile nikabeba mimba nikajifungua mtoto wa kwanza ..nikaja beba mimba nikajifungua wa pili siwezi sema mimi ndo nina matatizo au yeye maan nitakuwa nakosea pengine mimi nilikosea au yeye pia alinikosea maan nikisema alinifanya hivi sijui vile ntakuwa pengine namponda yeye kumbe shida ninayo mm ila mimi ndiye nikawa naumia kila nikijitahid kurekebisha ilishindikana basi tukawa tunaishi ndan kama watu hawajuani chuki yule baba kwangu ndo ilizidi maan nahis alinichoka zaidi kutokana na kuwa kinyume nae baadhi ya mambo yake ambayo sikuona sahihi au kutokana na tofaut zetu ukimwambia hiki tunaishia kulumbana kutokana na pengine tuliyopitia tulichokana ila mimi kama mm nilivumilia sababu ya mtoto apo nina mimba miez 7 ikafikia hatua mbaya mpaka napigiwa simu na manzi za nje zinanitukana nilipata pressure ya mimba nikajifungua siku ambazo sio makadirio nilijifungua week 29 mtoto njiti na siku najifungua hakuwa nyumban alilala kwa manzi zake alipigiwa simu na nesi alete vifaa hosptal kwa maan kabla ya kuingia theatre niliandika namba za wadhamin wawili na sikwenda kwa nia ya kujifungua ila nilikwenda kama clinic ndo pressure ikanishika ikabidi nikimbizwe op fasta basi nilipozinduka nilimuona hosp na mama yang na baadhu ya ndug zake apo mtoto alikuwa yupo kwenye incubeta ile ya kupumulia tulikaa sana hosp bas baada ya kuruhusiwa nilikaa week mbili alinipa talaka kwamba hanitaki ye anataka kuoa niende kwetu nikawasiliana na kwao tulikaa kikao ila alionekana mkorofi sana bas mpaka hivi navoongea mamaangu kajitoa kabisa kwenye maswala ya kesi yetu nipo napambana mwenyew ila kinachonifanya nipambane naye kwa sasa hali yangu haijaimarika sana kutokana na op nilifanyiwa mbili ya mtoto na ya hernia ya kitovu ambapo huko nyuma nilipata op ya nje ya kizazi na ya mtoto wa kwanza jumla ninayo mishono 4 kwa muda mfupi kwahiy sikukava sana hivo mamaangu analalamika anaelemewa sababu mamaangu ni kibarua tu hana biashara ya ajira ila yeye tulivyoachana alinitamkia sitapata chochote sikuhangaika maan tulijenga tukifanya maendeleo tukiwa wote sikutak kusumbuana nae kwenye mali maan niliamini ipo siku ningepata mali zangu na mimi je (nyie mnaosema nimefwata mali je ningeshindwa enda bakwata kudai mali zang?? msipende mtukan mtu hamjui nachopitia maan cheti ninacho na kuhus msharah alikuwa ananambia mpk siku anapandishwa cheo alinionyesha karatas kabisa ya ofisi mmenitukana san



cha mwisho nilitak kupambania haki za watoto tu ndo naan niliomba msaad wapi nipitie niwez pata haki yangu
Me ndio nimesoma hapa muda huu so kama nilikutukana juu huko niwie radhi. Ila bado nina maswali. Huyu bwana mlikutana mazingira gani?!

Na je , ulijiridhisha vipi kuwa mwenendo wake kimaisha atatoshea kuwa mume wako?
 
mnanikejeli sana mimi kuomba msaada basi naombeni mnisamehe nina roho ndogo sana naumia kwa kunidhihaki nisameheni pengine sikupaswa kuomba ushauri samahanini ilanjueni sijazaa bila ndoa nmezaa kwa ndoa kabisa
Jikaze usiwe mlaini hivi. Vikao vya kifamilia huwa vinakuwaga na mikiki mikiki ya namna hii kwa hivyo jikaze tutafute suluhu.
 
Me ndio nimesoma hapa muda huu so kama nilikutukana juu huko niwie radhi. Ila bado nina maswali. Huyu bwana mlikutana mazingira gani?!

Na je , ulijiridhisha vipi kuwa mwenendo wake kimaisha atatoshea kuwa mume wako?
swali sijalielewa
 
Usijibu kwa jazba bali boresha ubishani wako kwa hoja.Mliandikiana kwa ushahidi alichokuambia?Kama anakutunza vema haina shida.
NINACHOTAKA KUWAKUMBUSHA:Jitambueni na muwafundishe wenzenu/mabinti wanaochipuka wawe makini,wawe na uhakika na wanaume watakaopata nao watoto/familia.Kama ambavyo mnaitaka hamsini kwa hamsini kwa nguvu na haraka,ndivyo mpanue akili zenu na mjifungulie nguvu za uwezo wa kuzikabili changamoto zenu bila kulialia,kushtaki na kutaka kuonewa huruma muda wote.Sheria zilizopitwa na mabadiliko ya maisha isiwe egemeo batili la kujibanzabanza kimaisha.Vilevile,acheni kuzaa na wanaume kwa mategemeo ya kuvuna utajiri/mali,kumsumbua tu au kumkosesha amani ili kufurahisha,kulipisha gharama na kujirahisishia maisha.Jifunzeni kuchukua majukumu kwa akili na kuzitafuta huduma.
Umenena vema sana bamdogo. Huyu dada bado anaonyesha kuna elements za uzembe kwenye story yake.

Story yake ina red flags nyingi sana.
 
Kuna wakati huwa nashindwa kuwaelewa Wanaume wenzangu, hivi inakuwaje unashindwa kulea damu yako?

Imagine huyo Dada yupo tayari kupokea hata shilingi 50,000 kwa mwezi. Hiyo elfu 50 inatosha Kula, mavazi au mtoto akiugua kweli? Kwa hiyo elfu 50 huyo Mtoto atapata Sare za shule au hata Kalamu na Daftari akianza shule?

Tuweni na huruma wakati mwingine, wewe usingehudumiwa na Baba yako ungefika hapo ulipo kweli?

Kama hauko tayari kulea Mtoto, niwasihi Wanaume wenzangu ni bora kutumia Kondomu au mtumie uzazi wa mpango. Tutakuja kupata dhambi na laana za Uzeeni kwa kutelekeza damu zetu.

Umeshauri vizuri lakini Huko Chini umeharibu.
Hakuna mambo ya laana na Dhambi kwenye uhalisia wa Maisha.
Wapo Watu wanatenda wajibu na Majukumu Yao na bado uzeeni wanapasuka, na wapo Watu wanatelekeza Watoto na kufanya Matendo ya hovyo na uzeeni wanaishi vizuri au Watoto waliowatelekeza wanawakumbuka na kuwatunza.
Ulichofanya ni kutishia Watu ili waogope.

Muhimu ni kusema, Watu wabebe majukumu yao, ukizaa tunza wanaokuhusu, lakini hiyo sio Guarantee ya kutopasuka uzeeni. Kuna wazee wamelea Watoto Kwa Hali na Mali na bado wametelekezwa na Wake na watoto wao.
 
Umenena vema sana bamdogo. Huyu dada bado anaonyesha kuna elements za uzembe kwenye story yake.

Story yake ina red flags nyingi sana.
red flag kama zipi na nmeelza history kwa ufupi ila nyue ndo mmekazana nimempanulia mara nimezaa na mume wa mtu
 
Hitimisho lako ndiyo limeharibu kila kitu. Bado ninajiuliza, je, umeleta uzi wa kuwasema wanaodai kuwa ulifuata mali au unaomba msaada?!!🤔
 
Hitimisho lako ndiyo limeharibu kila kitu. Bado ninajiuliza, je, umeleta uzi wa kuwasema wanaodai kuwa ulifuata mali au unaomba msaada?!!🤔
wengi humu mmenitusi sijuu nmezaa kwa sabab ya mali mara nilifwata hela kwel?? serious mkuu?
 
Ujinga ni upi hapo?Mueleze mtu ukweli na ajitambue.Mnakaa mnawadanganya hovyo,kuwasomea vijisheria vya kipuuzi bila kuwafundisha kujisimamia na kuyakabili majukumu.Mnawarembea mwandiko habari za huzuni?Mnawazubaisha na kuwafanya wasiwe responsibles kwa mambo yaliyowakuta,wanayoyaishi na hamuwapi positive options!
Huyo anaomba utelezi kwa njia nyingine
 
Labda anawatoto wengine sehemu zingine.
Hoja hapo yaangaliwe mahitaji ya mtoto ya lazima, kisha gharama alafu yagawanywe Kwa Mbili yaani Baba na Mama. Full stop.
mim sina kazi mkuu kumbuka nmezaa mtoto njiti najiuguza na alinioa alisema hatak mwanamke afanye kaz asa nimeachwa sina pa kuanza nifanyaje?
 
Kwa hiyo ulivyojua huo mshahara ukaona mkubwaa ,

Wanawake mna mambo nyie?! [emoji4]

Ukaona uitege ?

Kupata majaliwa Na kisichoriziki hakiliki.
Kaitegaje na kasema wameoana?
 
Hakuna anaekukejeli unaambiwa ukwel hata ukiolewa tena usitoe mapembe juuu na kutomsikiliza mme wako hadi ndoa inakufa..

Ukipata mume tena ukae Kwa kutulia acha mapepe ,msikilize mmeo na sio kusikiliza mashangazi na wanaharakat wa haki sawa watakuponza tena..mtii mume wako mtarajiwa mchukulie kama Mungu wako ha ha haa..[emoji23][emoji23][emoji23]
Singel maza hawaolewi
 
siwezi mchukulia mwanaume kama Mungu na huku nmeomba jinsi ya kufanya asa kejeli matusi ya nini?? nikaomba basi na ajira mnisaidie nilee hawa watoto ni sabbau hujui behind ya haya mambo....kamwe siwez mfananaisha Mungu wangu na kitu chochote afu sahivi ndoa sio priority yangu kaka so usinikejeli kwa kuona nataka mume sijui kulalamika hapana
Ukisema Ndoa sio priority yako mbona unataka benefits za ndoa sasa?

Ukipata watoto malezi sahihi ni ndani ya Ndoa, ukiwa nje ya Ndoa hapo ni wewe na nafsi yako na sio wewe watoto na mume wako.

Dada nahisi unachangamoto zako. Huyu mwanaume anaweza kuwa mkorofi ila wewe una part yako kubwa katika kuvunja hii ndoa. Huwa nakutana na visa vya namna hii, ukitumia hisia utajikuta umetetea mwanamke na kumbe yeye ndie mkorofi.

Mimi nadhani fanya kujitathimini kwa kina hili eneo.
 
Back
Top Bottom