Msaada: Nataka kwenda Ustawi wa Jamii, baba wa watoto ananisumbua huduma

Kuna wakati huwa nashindwa kuwaelewa Wanaume wenzangu, hivi inakuwaje unashindwa kulea damu yako?

Imagine huyo Dada yupo tayari kupokea hata shilingi 50,000 kwa mwezi. Hiyo elfu 50 inatosha Kula, mavazi au mtoto akiugua kweli? Kwa hiyo elfu 50 huyo Mtoto atapata Sare za shule au hata Kalamu na Daftari akianza shule?

Tuweni na huruma wakati mwingine, wewe usingehudumiwa na Baba yako ungefika hapo ulipo kweli?

Kama hauko tayari kulea Mtoto, niwasihi Wanaume wenzangu ni bora kutumia Kondomu au mtumie uzazi wa mpango. Tutakuja kupata dhambi na laana za Uzeeni kwa kutelekeza damu zetu.
 
Unapoamua kuzaa hakikisha na wewe una uwezo wa kutunza watoto peke yako incase linapotokea jambo lolote. Nenda Mahakamani kama unaona mzigo ni mzito.Nenda kashitaki ili awe anatoa child support.Binafsi ningekuwa wewe wala nisingehangaika nae ,yule ni Baba anajua wajibu wake.Mimi ningemuacha nikalea wanangu.Finali uzeeni .
 
Yaani hamu yako wewe unaona ni sawa kuwa nayo, lakini hamu ya mtoto ndo umwite mchwa..!! Sasa ujuwe mchwa anazaliwa na mchwa..!!
 
Angewaza kuwa kuna kufa, asingefanya hayo..!!
 
Bila shaka ni wa kiume maana wanatafuna haswa
 
Kwanza hakuna kitu kibaya kama kuzaa watoto tofauti tofauti na hovyo hovyoo inakuwaga tfran tupu
inaleta tatizo kubwa sana hii kitu.. watoto wengi tuliozaliwa kwa michanganyo iliyochochewa na tabia chafu za wazazi wetu kutoboa kwenye maisha inakuwaga ni shughuli pevu sana kuna baraka fulani zinavurugwa japo zipo ila kuzifikia mpaka upambane sanaa
 
Kwa hiyo ulivyojua huo mshahara ukaona mkubwaa ,

Wanawake mna mambo nyie?! [emoji4]

Ukaona uitege ?

Kupata majaliwa Na kisichoriziki hakiliki.
 
Umesema kweli kabisa watoto wanaozaliwa familia moja tu huwa wana baraka sana
Hawa wa mchanganyiko kwanza wanakuwa hawapendani maana kila mtu kalelewa kwingine Yaan inakera mno
 
Naombeni msaada nataka kwenda ustawi, baba wa watoto huduma ananisumbua maana ni mfanyakazi TANESCO Engineer Grade 1 anapokea 2.8. Sasa naombeni msaada - Je, kwa mshahara huo naweza pata elfu 50 ustawi au wanadanganya?
Mlikubaliana kuanzisha mahusiano kwa ajili ya kuzaa?
Kama hamkukubaliana nabidi akushitaki kwa kubeba mimba yake bila makubaliano.
Ili mambo yasiwe mengi na mengi yasiwe mambo bora uendelee kulea kivyako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…