Msaada: Nawezaje kuacha tabia ya kuongea peke yangu?

Niliwahi kusikia watu wanaoongea wenyewe ubongo wao unafanya kazi kuzidi normal, mara nyingi watu wa aina hii huwa wanatakiwa kutumika kwenye taaluma km za utafiti/ugunduzi maabara n.k ila kwa kuwa wabongo hatujawahi kuwa serious huu uzi utajaa replies za utani tu.
Mkuu sijajua unadili na mishe gani ila kwa ushauri ili kuupooza ubongo wako jaribu kuwa na watu ila pia siku hizi kuna mitandao km hivi so waweza kuitumia pia. Kumbuka kila ufanyalo linaratibiwa na ubongo.
 
Shukrani Sana mkuu ..
 
Wewe ni introvert
 
Endelea mkuu, unapunguza stress, unacontrol emotion. Lakini pia ni dalili ya kuwa wewe unaouwezo mkubwa mno wa akili.



Sio kila mtu anao uwezo wa kuongea mwenyewe kwa mpangilio maalum wa kueleweka ni watu wachache mno wenye uwezo huo ila sijamaanisha ila kuongea hovyohovyo ya watu wenye matatizo ya akili. Naamanisha ile hali ya kuweza kutengeneza kikao au kijiwe wewe mwenyewe na story zikanoga hiyo ni dalili ya uwezo mkubwa wa akili.





 
Nipo hivyo mkuu, naweza kukaa na kuanza kuchanganua jambo kwa kina mno na pia naweza kuwa labda nipo na watu naangalia Tv ikatokea nimeona kitu cha kufikirisha nitajikuta tu nimeinuka natoka nje na kuanza kuzunguka nje huku nikiwa najadili like jambo .. hapo naweza chukua hata saa nzima mpaka kuja kushtuka tena ..
 
Kama unaouwezo wa kutengeneza kikao kwenye akili yako. Na kichwani mwako hicho kikao kikawa kama kikao kwelikweli mpaka mnabishana na kukubaliana kwa hoja kiufupi Mungu amekupa akili nyingi sana (sijamaanisha za darasani). Wazungu wameshafanya utafiti wanasema watu wenye akili za aina hiyo wana ubunifu wa hali ya juu mno na wengine ni majiniasi kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…