Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shukrani sana mkuu [emoji1545] [emoji1545]Wala sikushangai, nipo hivyo pia mara nyingi tu huwa napiga stori mi mwenyewe na kujijibu mwenyewe na wala sioni kuwa nina tatizo la kiafya ya akili tena mimi huwa nakuja na majibu imara haswaa kwa maswali ambayo huwa nayatafutia majibu. Kuna watu wanaonizunguka huwa wakikwama kwenye majibu ya yanayowatatiza huwa wakinifuata ni dk 0 tu nimewapatia majibu wanasepa.
Kuna mdada mmoja kaja kunifanya mimi ni gud n close brother of hers, ananiheshimu mno na kunipenda sababu hiyo hiyo ya kumpa na kuresolve yanayomtatiza na wala hakuwahi kuniwazia hivyo. Ndugu, jiamini wewe huna tatizo la kiakili.
New hamza in the making Detective Cpl Detective JNashangaa watu wameleta utani na hakuna seriousness katika hili. Mimi mwenyewe naongea peke yangu hasa ni kwa kuwa nakosa watu sahihi wa kuongea mada zangu. Unakuta sebuleni wako wanatazama mkurugenzi kaagiza vyoo vifungwe mimi naona ni habari za kipuuzi nazama chumbani kutazama Taliban wamefanyaje. Alafu sasa unakuta nasema mwenyewe "hawa Taliban si ndio juzi hapa walikuwa wanashangaa gym na babywalkers za umeme, sasa wamewezaje kuendesha helicopter si wataanguka hawa?"
alafu nafikiria then najijibu "itakuwa wameteka marubani wa jeshi la serikali iliyopita au jeshini kulikuwa na mamluki wa Taliban". Simply ni kwamba nikikaa na watu tunaelewana siongei mwenyewe
Ahahaaaa.....!Sasa hapa ni bora uishi karibu na Dodoma ili usiwape kazi ngumu ndugu zako kukusogeza pale hospitali ya waheshimiwa [emoji16][emoji16]
Fanya liwezekanalo uishi mkoani Dodoma
Watu wanaweza wasikuelewe. Ila Mi naelewa.Binafsi ni mtu wa kujitenga sana, sio mtu wa kujichanganya kabisa na sijawahi kuwa bored .. ni simply because I have a tendency of talking alone, ninaweza kukaa peke yangu na kuanza kuongea kwa muda mrefu hata masaa mawili .. mtu akiniona huwa nashtuka sana na kuanza ku pretend kama naimba [emoji23][emoji23] .. nimejitahidi sana kuacha hii tabia lakini nashindwa .. kila nikifumwa huwa najiapia kwamba sirudii tena, lakini naishia kurudia kama awali .. je hii ni kawaida ? .. nawezaje kuacha hii tabia ?? ..
Hiki unachokisema nimekumbuka jambo.Niliwahi kusikia watu wanaoongea wenyewe ubongo wao unafanya kazi kuzidi normal, mara nyingi watu wa aina hii huwa wanatakiwa kutumika kwenye taaluma km za utafiti/ugunduzi maabara n.k ila kwa kuwa wabongo hatujawahi kuwa serious huu uzi utajaa replies za utani tu.
Mkuu sijajua unadili na mishe gani ila kwa ushauri ili kuupooza ubongo wako jaribu kuwa na watu ila pia siku hizi kuna mitandao km hivi so waweza kuitumia pia. Kumbuka kila ufanyalo linaratibiwa na ubongo.
Huwa Unaongea nini?? Tuanzie hapo kwanza.Binafsi ni mtu wa kujitenga sana, sio mtu wa kujichanganya kabisa na sijawahi kuwa bored .. ni simply because I have a tendency of talking alone, ninaweza kukaa peke yangu na kuanza kuongea kwa muda mrefu hata masaa mawili .. mtu akiniona huwa nashtuka sana na kuanza ku pretend kama naimba [emoji23][emoji23] .. nimejitahidi sana kuacha hii tabia lakini nashindwa .. kila nikifumwa huwa najiapia kwamba sirudii tena, lakini naishia kurudia kama awali .. je hii ni kawaida ? .. nawezaje kuacha hii tabia ?? ..
Nipo hivyo pia, naweza kujipa safari tu nikawa natembea tu bila kuwa na sehemu specific ninayokwenda ..Watu wanaweza wasikuelewe. Ila Mi naelewa.
Yaani mimi naweza jipa safari ya kutembea ili nifanye hiyo kitu, especially nikivaa earphones.
Yangu inaitwa Maladaptive Day Dreaming. Sema haina madhara so naitumia ku-cope na maisha.
Pole man. Haina side effects sana zaidi ya kupoteza muda na kuchoka kutokua productive.Nipo hivyo pia, naweza kujipa safari tu nikawa natembea tu bila kuwa na sehemu specific ninayokwenda ..
anza kwa kusoma vitabu kimya kimya.Utasinzisha speech centresNaongea vitu kwa kueleweka kabisa ..