Msaada: Ndugu yangu (22) kaanza ubabe kwangu (31), kisa karefuka na anabeba vyuma

Msaada: Ndugu yangu (22) kaanza ubabe kwangu (31), kisa karefuka na anabeba vyuma

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
copy paste fb 😂😂

JE NICHUKUE UAMUZI UPI KAMA MTU MZIMA.

Ni mtoto wa ndugu yangu, mara ya mwisho kuonana nae ilikuwa kama miaka 7 iliyopita, kipindi hicho tulitokea kuwa na mazoea sana, kahamia mkoani kwangu huku kiukweli dogo kapanda hewani yupo kama futi 6 .3,,,mimi nipo 5.9

Sasa kahamia mkoa wangu huku anafanya shughuli zake, kwahio huwa tunakutana mara kwa mara.

Tatizo linakuja tukikutana huwa ni kama anatania flani hivi ila inakuwa style ya kuniona mimi mfupi kuzidi yeye so huwa ni kama analeta kaubabe flani hivi.

Jana nilikuwa sehem flani nimepumzika nimechoka baada ya kutoka kazini, nikashangaa mtu kanipiga vidole kwenye mbavu kama ule mchezo wa sekondari, niliamka na hasira sana, nikaona ni huyu dogo, sasa wakati nimefura akawa kama ananiangalia chini kudhiirisha urefu wake na misuli yake hio ya mazoezi, nilimuonya ila alibaki anacheka tu.

Nichukue uamizu gani
 
Potea miaka miwili au mitatu nenda china kakutane na jetri, jackchain, na wale kina drunken master ukajifunze style mbalimbali za kupigana.

Hakikisha unatia juhudi baada ya hapo rudi bongo af kaa kindezindezi ukisubri akufanyie hivyo tena hapo ndipo atakapostukia tu umepaa hewani na kumpiga utosini anatahamaki anajikuta chini.

Nahisi nauli sio kubwa siku hizi baada ya ujio wa bombadier zetu.
 
Watu wazima nyie, pengine wewe ndio unajishtukia, yeye hana dharau. Na kama mna ukaribu, kwa nini usimwambie?
 
Labda hukusoma hapa

Mimi mwenyewe nina dogo mtoto wa kaka yangu nimemlea yani nmemzidi sana zaidi ya miaka 12 sema kapanda anaenda gym naona hata shikamoo kila kukicha zinapungua ukali
 
Dawa yake wewe tafuta hela, uwe unamtuma kubeba mizigo.
 
Akikukipiga kidole cha trako ndio akili jtakukaa sawa
 
Nenda kwa warussi ukirudi atakaa mbali na wewe
 
copy paste fb 😂😂

JE NICHUKUE UAMUZI UPI KAMA MTU MZIMA.

Ni mtoto wa ndugu yangu, mara ya mwisho kuonana nae ilikuwa kama miaka 7 iliyopita, kipindi hicho tulitokea kuwa na mazoea sana, kahamia mkoani kwangu huku kiukweli dogo kapanda hewani yupo kama futi 6 .3,,,mimi nipo 5.9

Sasa kahamia mkoa wangu huku anafanya shughuli zake, kwahio huwa tunakutana mara kwa mara.

Tatizo linakuja tukikutana huwa ni kama anatania flani hivi ila inakuwa style ya kuniona mimi mfupi kuzidi yeye so huwa ni kama analeta kaubabe flani hivi.

Jana nilikuwa sehem flani nimepumzika nimechoka baada ya kutoka kazini, nikashangaa mtu kanipiga vidole kwenye mbavu kama ule mchezo wa sekondari, niliamka na hasira sana, nikaona ni huyu dogo, sasa wakati nimefura akawa kama ananiangalia chini kudhiirisha urefu wake na misuli yake hio ya mazoezi, nilimuonya ila alibaki anacheka tu.

Nichukue uamizu gani
Nikaribishe kwako nimshilishe adabu
 
Nina dogo langu anamwili mkubwa ila namshona vizuri mikanda na mianzi ya mgongo mpaka akili inamkaa sawa, uyo ukidhihirisha anakupima we mpe kipimo halisi
 
Back
Top Bottom