Msaada: Niliingia mkataba wa bajaji kwa miaka miwili, baada ya miezi 20 nimepokonywa bajaji

Msaada: Niliingia mkataba wa bajaji kwa miaka miwili, baada ya miezi 20 nimepokonywa bajaji

Imekula kwake
Kutokuwa na mkataba siyo tatizo. Tatizo ni ushahidi kuwa alimpatia hizo elfu 20 kwa miezi hiyo. Kama alikuwa anatunza nyaraka kesi nyepesi hiyo ni either ataachiwa bajaj au atarudishiwa fedha ila kama mkataba hana, ushahidi wa malipo hana, huyo achukulie kama kalipia ada ya kujifunza umuhimu wa utunzaji kumbukumbu.
 
Kama hana mkataba imekula kwake.

Hata kama ana ushahidi wa miamala bosi atamkana tu, Akisema alimwajiri na haikuwa mkataba wa kuja kuachiana chombo atasemaje.

Mwenetu achukue kama somo tu, Kwenye kutafuta kuna hasara ndio hizo sasa, next time asifanye makosa kama hayo tena.
 
Ni haki kweli? Kuna mdau mmoja kanipa bajaj yake kwa mkataba wa miaka 2. Yaani kila siku nimpe 20,000/=.

Nimefanya kazi kwa muda wa miezi 20, huyo mdau kaninyang'anya chombo kwa Madai anamadeni benki hivyo inabidi aiuze ili apunguze deni.

Nimejaribu sana kufuatilia kwa watu mbali mbali kuona ntasaidiwaje ila kote bila bila.

Naombeni ushauri wenu kwa wenye uelewa zaidi.

N.B HILI BANDIKO NI LA MDAU AMBALO NIMESHARE NANYI.
Je kuna mpatano au makubaliano mliyowekeana kimaandishi? Kama hakuna pole
 
Kama hana mkataba bado ana haki ikiwa pesa alikua anamuwekea kupitia simu yake na sio kwa wakala,je kuna kidaftari alikua ana saini wakati wa kupokea pesa?
Je kuna shaidi wa mazungumzo yenu ?
 
Kabla ya kwenda popote, je hiyo 20k kwa siku ulikiwa unaitimza?? Na kama ulikuwa unaruka mara kwa mara je ulikuja oufidia bila kukosa?? Tuanzie hapo kwanza
Hapo kuna point mkuu. Vijana wengi wakiaminiwa huwa watiifu siku za mwanzo lakini baadaye wakishazoea wanaanza kuzingua. Je huyu si mmojawapo?
 
Kutokuwa na mkataba siyo tatizo. Tatizo ni ushahidi kuwa alimpatia hizo elfu 20 kwa miezi hiyo. Kama alikuwa anatunza nyaraka kesi nyepesi hiyo ni either ataachiwa bajaj au atarudishiwa fedha ila kama mkataba hana, ushahidi wa malipo hana, huyo achukulie kama kalipia ada ya kujifunza umuhimu wa utunzaji kumbukumbu.
Umenikumbusha: Mali bila daftari hupotea bila Taarifa.😁
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Kama hana mkataba imekula kwake.
Mikataba huwa inapotea, inaharibika, inaibiwa n.k Kwani hujui hili boss? Kama umri wako ni above 30 hili lazima umeshawahi kutana nalo na ushahidi mbadala ukatumika kutatua tatizo. Kwa huyu ushahidi mbadala ni slip za malipo.
Hata kama ana ushahidi wa miamala bosi atamkana tu, Akisema alimwajiri na haikuwa mkataba wa kuja kuachiana chombo atasemaje.
Alimwajiri kwa mkataba gani? Hakuna mikataba ndo msingi wa kesi. Mwenzake atakuwa na slip kama ushahidi kuwa nimempa huyu fedha kwa makubaliano kuwa nitamlipa kwa miezi 20 na nilitunza hili ili nitakapomaliza nimkabidhi, leo kanigeuka sasa jaji hapo ndo atasubiri ushahidi wa mwenye bajaji kuwa alimwajiri. Halafu kesi kama hizi mwongo anajulikanaga. Labda ahonge. Miez 20 ni mingi, unakuta walishatumiana ujumbe au walishaongea kwa simu kuwa apambane bado kidogo atamaliza yaani ukitrace back lazima kuna alama tu za ushahidi zitakuwa zimeachwa maana kila unapodeposit utawasiliana na mhusika kuwa umeweka sasa mara 20 zote lazima kuna sehemu mmezungumza jambo linalohusu sababu ya kuweka fedha. Hapo ni kuangalia tarehe ya slip na kurudi kwenye rekodi za mawasiliano kuangalia mlizungumza nini. Kesi inaweza chukua hata miaka.
Mwenetu achukue kama somo tu, Kwenye kutafuta kuna hasara ndio hizo sasa, next time asifanye makosa kama hayo tena.
Somo ni kwa sababu hana ushahidi wowote.
 
1- hawakuandikishana popote Bali walipeana Ile ya kuaminiana.
2- kwanini hawakuandikishana, nikwasababu aliwahi kufanya kazi ya kuuza duka la mdau la spare.
3- Hilo swala lilifikishwa kwa mtendaji na mpaka polisi, ambapo mdau alikana kumpa dog chombo chake na hafahamu makubaliano ya aina yote baina Yao.
4- mdau ni askari hivo ni kama anamkandamiza dog kupata haki yake. Na ukizingatia chombo kilitunzwa na bado Kiko vizuri.
5-mpaka bandiko hili linakuja huku, dog alikuwa amewekwa lockup kwa kesi ya kumtusi huyo mdau. Ila tulifanikiwa kumtoa swala limebaki kwenye haki za huyo dogo kwenye hio bajaj. Mdau kasema labda afe na chombo kashakiuza jana jioni 4.3ml. Inaumiza kwakweli.
Kosa la kufanya kazi kimazoea ndio uleta haya..,,unakubali vipi kuingia mkataba bila maandishi? Amesha kushinda hadi happ
 
Siku hizi watu wana roho mbaya. You need to be very careful in every step of your life.
Una bahati, wenzako wakibakisha wiki wanauwawa na kunyang'anywa bajaji au pikipiki kisha upepo ukitulia inauzwa mtaa wa 4
 
PACTA SUNT SERVANDA

Hiyo bajaji ni Mali yako, kopa marejesho ya miezi 4 iliyobakia muwekee kwenye akaunti. Fungus kesi mahakamani, mahakama imlazimishe AKUPE Mali yako
Mkuu hata kama mlalamikaji ha-kuandikiana mkataba na mshtakiwa?
 
1- hawakuandikishana popote Bali walipeana Ile ya kuaminiana.
2- kwanini hawakuandikishana, nikwasababu aliwahi kufanya kazi ya kuuza duka la mdau la spare.
3- Hilo swala lilifikishwa kwa mtendaji na mpaka polisi, ambapo mdau alikana kumpa dog chombo chake na hafahamu makubaliano ya aina yote baina Yao.
4- mdau ni askari hivo ni kama anamkandamiza dog kupata haki yake. Na ukizingatia chombo kilitunzwa na bado Kiko vizuri.
5-mpaka bandiko hili linakuja huku, dog alikuwa amewekwa lockup kwa kesi ya kumtusi huyo mdau. Ila tulifanikiwa kumtoa swala limebaki kwenye haki za huyo dogo kwenye hio bajaj. Mdau kasema labda afe na chombo kashakiuza jana jioni 4.3ml. Inaumiza kwakweli.
Vitu kama hivi vinaumiza kwakweli mtu una struggle tena kwa uaminifu then mwisho wa siku mtu anakufanyia unyama huu ila hata kama dogo hatopata haki yake kwasababu ya mamlaka aliyonayo askari bc haki yake ipo kwa mwenyezi Mungu atalipwa kwa anachostahili na uyo askari naye atalipwa pia kwa anachostahili na wala asihuzunike sana japokua inaumiza ila mbaya
 
Back
Top Bottom