Msaada: Niliingia mkataba wa bajaji kwa miaka miwili, baada ya miezi 20 nimepokonywa bajaji

Msaada: Niliingia mkataba wa bajaji kwa miaka miwili, baada ya miezi 20 nimepokonywa bajaji

Siku hizi watu wana roho mbaya. You need to be very careful in every step of your life.
Una bahati, wenzako wakibakisha wiki wanauwawa na kunyang'anywa bajaji au pikipiki kisha upepo ukitulia inauzwa mtaa wa 4
Kisheria kuna ushahidi wa kimazingira unaweza kukusaidia nitafute inbox nikushauri
 
Kama kuna namna ya kumsaidia huyu mtu asaidiwe kosa la uaminifu...
 
1- hawakuandikishana popote Bali walipeana Ile ya kuaminiana.
2- kwanini hawakuandikishana, nikwasababu aliwahi kufanya kazi ya kuuza duka la mdau la spare.
3- Hilo swala lilifikishwa kwa mtendaji na mpaka polisi, ambapo mdau alikana kumpa dog chombo chake na hafahamu makubaliano ya aina yote baina Yao.
4- mdau ni askari hivo ni kama anamkandamiza dog kupata haki yake. Na ukizingatia chombo kilitunzwa na bado Kiko vizuri.
5-mpaka bandiko hili linakuja huku, dog alikuwa amewekwa lockup kwa kesi ya kumtusi huyo mdau. Ila tulifanikiwa kumtoa swala limebaki kwenye haki za huyo dogo kwenye hio bajaj. Mdau kasema labda afe na chombo kashakiuza jana jioni 4.3ml. Inaumiza kwakweli.
Aisee..
Kama huyo bosi wake ni askari polisi, akamuone kwanza iGP, anaweza kusaidiwa chap
 
Kama anamkataba hiyo bajaji niyake, ila kama waliongea kishikaji hapo imeshakula kwake.
 
Karipoti ofisi ya PCCB karibu yako utasaidiwa kwa kiasi chake
 
Kwa kifupi hapo amevunja mkataba na anatakiwa kukulipa pesa yote uliyomuingizia kipindi hiki chote cha miezi 20.

Kama mlikubaliana Bajaji ilete hesabu kila siku ina maana ni ( siku 365 × Tshs 20,000/=) jibu ni Tshs 7,300,000/= mara mbili ni Tshs 14,600,000/=.

Hii maana yake ni kuwa ulishatimiza ths 12,200,000/= katika mkataba wako ilibakia 2,400,000/=

Ulishatekeleza sehemu kubwa sana ya mkataba na hiyo inakupa ushindi hata kabla ya kesi kutolewa hukumu.

Kwa kifupi huyo muhusika amekiuka masharti na anatakiwa kukulipa stahiki yako ambacho ni bajaji mpya tena ambayo haijatumika. Ama kwa shinikizo la mahakama akulipe hiyo milioni 14.6 Cash.
 
Hakuwa na mkataba wa kisheria ila walikabidhiana kwa kuaminiana.
Na ndio maana jamaa amechukua bajaji yake kwa jeuri maana anajua hakuna mkataba kati yao kimsingi alimkodisha tu bajaji ili aendeshe maisha yake.
 
1- hawakuandikishana popote Bali walipeana Ile ya kuaminiana.
2- kwanini hawakuandikishana, nikwasababu aliwahi kufanya kazi ya kuuza duka la mdau la spare.
3- Hilo swala lilifikishwa kwa mtendaji na mpaka polisi, ambapo mdau alikana kumpa dog chombo chake na hafahamu makubaliano ya aina yote baina Yao.
4- mdau ni askari hivo ni kama anamkandamiza dog kupata haki yake. Na ukizingatia chombo kilitunzwa na bado Kiko vizuri.
5-mpaka bandiko hili linakuja huku, dog alikuwa amewekwa lockup kwa kesi ya kumtusi huyo mdau. Ila tulifanikiwa kumtoa swala limebaki kwenye haki za huyo dogo kwenye hio bajaj. Mdau kasema labda afe na chombo kashakiuza jana jioni 4.3ml. Inaumiza kwakweli.
Askari sio watu wa kufanya nao biashara yoyote wana upumbavu mwingi sana. Na wanahisi kazi yao ni kichaka cha kuficha maovu yao.
 
Back
Top Bottom