MSAADA: Nimepata kazi Serikalini dereva ila mshahara mdogo kuliko wa Mwendokasi ninakofanya kazi sasa. Nimechanganyikiwa!

Hao WMA sii ni ajira za muda hizo. Mkataba wa mwaka mmoja,. Komaa na mwendokasi utakuja lia
Boss, hapa ndo wengi hawapajui, washikaji kibao wanasota kitaa baada ya mkataba kuisha na kutemwa na hao WMA. Ni kama Tanroads, operators wa mizani.

Hizo per diem zinaishia kwenye starehe tu, angalau wizi wa mafuta unafanya kila siku.
 
Kwanza Sina imani na huo mshahara unaosema. mnalipwa huko mwendokasi, acha Uongo. UDart hivi sasa inamilikiwa na serikali, wawalipe 800000 kwani nyie mna tofauti gani na madereva wa serikali?. Labda utuambie hiyo 8 ni pamoja na marupurupu mengine.

Serikalini kuna advantage kubwa ikiwepo posho za safari kwa usiku mmoja kwa dereva ni 80000.Pia kuna Mikopo ambapo kwa dereva utakopeshwa si chini ya milion 15,. Ajira ya serikali hata gari uliyokabidhiwa au uwe huna gari, bado mshahara utaingia.

Je Una habari hapo UDart ni mradi wa majaribio, kiasi kwamba serikali ikiona haulipi itaachana nao na kumtafuta Mwendeshaji ambaye atakuja na vigezo vyake vya kufanya apate faida, ikiwepo na kushusha mishahara.
 
Wanabodi mm ni dereva mzoefu wa daladala kisha nikaajiriwa na mwendokasi ambapo nakula 800,000/per month .
Wandugu kwa sasa nimevurugwa kwan baada ya interview iliyohusisha watu 760 ambao tuliomba kazi wakala wa vipimo tumepenya na kuajiriwa 57 tuu!!! Nimepewa barua Jana napaswa kuripoti kituon kuanzaia 2/7 sasa aisee mbona hii salary Jau!? Yan nipo kipindi kigumu wandugu hebu wenye uzoefu nisaidieni hill!?kiukweli napata wakati mgumu sana barua ninayo ila naipenda ajira za serikali tatizo hiyo salary!??naomba ushauri
Nenda wakala wa vipimo hutajuta ,kuna perdiem huko mpaka waajiriwa wanapaliwa ,
Nenda kapige Kazi mkuu,utatoboa Saa mbili asbh kabla jogoo hajawika
 
Acheni kumjaza mwenzenu ujinga...uache laki nane ukimbilie laki tatu..ukikatwa hiyo unabaki na laki mbili...ukienda huko utakula msongo wa mawazo to your entire life. Kuhusu ishu ya perdiem wasikudanganye..perdiem inaendana na levo ya mshahara..kwa mshahara huo perdiem yako haitazidi elfu sitini..sasa upate safari ya siku tatu singida utalipwa 240,000. Ukienda huko ulipie guest, msosi, utakutana na watoto wa kiburushi..utakula nao bata..siku ya kurudi mjini utaishia kubeba machungwa na viazi hautabaki na kitu.
Ushauri wangu endelea hapo hapo mwendokasi
Mi nakomea hapa kusoma maoni Umemaliza mkuu, huwezi kuacha laki 8 ukakimbilia laki 3 kisa Serikalini utazeeka ukiwa huna chochote zaidi ya sifa za mstaafu Serikalini
 
Dole gumba. Niliachana na mawazo ya kijinga ya security ya kazi zamani sana. Na wala sijawahi kujuta. Kuna sehemu ukifanya kazi miaka 5 unatapa hela yote ambayo ungeisotea serikalini kwa miaka 15-20. Sasa kwa nini ukae huko serikalini kwa miaka 20 wkt kuna nafasi ya kupata hiyo pesa ktk miaka 5? Siyo ujinga huo ni nini? Na wakati natoka serikalini, kaka yangu alitoa machozi akifikiri napotea njia! Yeye yuko serikalini kwenye security miaka nenda rudi lakini amechakaa sana. Hana msaada wowote kwenye familia yetu pamoja kuwa na security ya kazi. Karibu anastaafu sasa.
Security ya ajira ni ujinga ambao unawaponza wengi
 
Acheni kumjaza mwenzenu ujinga...uache laki nane ukimbilie laki tatu..ukikatwa hiyo unabaki na laki mbili...ukienda huko utakula msongo wa mawazo to your entire life. Kuhusu ishu ya perdiem wasikudanganye..perdiem inaendana na levo ya mshahara..kwa mshahara huo perdiem yako haitazidi elfu sitini..sasa upate safari ya siku tatu singida utalipwa 240,000. Ukienda huko ulipie guest, msosi, utakutana na watoto wa kiburushi..utakula nao bata..siku ya kurudi mjini utaishia kubeba machungwa na viazi hautabaki na kitu.
Ushauri wangu endelea hapo hapo mwendokasi

Mkuu una uhakika na unachokisema kuwa per diem inaendana na ngazi ya mshahara ndugu...?

Na pia unafahamu kuwa mwenye ajira serikalini anakopesheka mamilioni ya shilingi mkuu...?
 
Na uhakika 100% perdiem inaendana na cheo au ngazi ya mshahara. Perdiem ya dereva haiwezinkuwa sawa na perdiem ya Mkurugenzi au Ofisa labda kama ngazi zao za mshahara zinafanana.
Siyo kila sehemu kuna hiyo access...mm sijawahi pata huo mkopo unaousema licha ya kuwa kwenye taasisi za kiserikali.
 
NENDA HARAKA SERIKALINI, KUNA KITU KINAITWA JOB SECURITY KWA WATUMISH WA SERIKALI, AMBAPO ITAKULINDA HADI KU STAFF KWAKO.
Madereva wa serikal wana mishahara midogo ila wana malulupu mengi unaweza kufikisha hata posho ya Million Moja kwa mwezi...
Hao mwendokasi sio wakuwaamini kesho na kesho kutwa hawapo...
 
Fata ushauri wa huyu jamaa.
Nikupe mfano kuna ndg yng anafanya kazi serikalini analipwa 350k Ila anajenga na ana gar yake nzuri tuu. Na security ya kazi. Kama ni permanent kapige kazi kama ni ya muda acha acha acha
Kama ni mkataba achana nayo kama ni permanent nakuomba uende kiongozi...!

Unaongea na dereva mwenzako japo sipo serikalini direct nipo kwenye mradi chini ya Taasisi ya serikali kiongozi.

Karibu sana...!
 
Acheni kumjaza mwenzenu ujinga...uache laki nane ukimbilie laki tatu..ukikatwa hiyo unabaki na laki mbili...ukienda huko utakula msongo wa mawazo to your entire life. Kuhusu ishu ya perdiem wasikudanganye..perdiem inaendana na levo ya mshahara..kwa mshahara huo perdiem yako haitazidi elfu sitini..sasa upate safari ya siku tatu singida utalipwa 240,000. Ukienda huko ulipie guest, msosi, utakutana na watoto wa kiburushi..utakula nao bata..siku ya kurudi mjini utaishia kubeba machungwa na viazi hautabaki na kitu.
Ushauri wangu endelea hapo hapo mwendokasi
Aiseee Hongera kwa kupata akili mkuu ,hapo Kuna variation ya 500k Sasa sijui km hizo per diem zitafika hyo number labda uibe mafute na wizi mwingine..
Ukikomaa mwendokasi mwaka 1 tu ushapata mtaji...
Kama unataka kulala kwa waganga na kuwa mshirikina safi nenda huko ukatumikie wafaidi nchi ..Utakumbuka nyuma
 
Acheni kumjaza mwenzenu ujinga...uache laki nane ukimbilie laki tatu..ukikatwa hiyo unabaki na laki mbili...ukienda huko utakula msongo wa mawazo to your entire life. Kuhusu ishu ya perdiem wasikudanganye..perdiem inaendana na levo ya mshahara..kwa mshahara huo perdiem yako haitazidi elfu sitini..sasa upate safari ya siku tatu singida utalipwa 240,000. Ukienda huko ulipie guest, msosi, utakutana na watoto wa kiburushi..utakula nao bata..siku ya kurudi mjini utaishia kubeba machungwa na viazi hautabaki na kitu.
Ushauri wangu endelea hapo hapo mwendokasi
hongera umemusauri poa sana
 
Swali ni kwamba anajenga nini na anaendesha nini? Kwa hiyo huko aliko huyu mleta mada hakuna watu wenye magari na nyumba? Watu wengine wanajenga kwa vile ni wezi. Sasa na wewe unataka huyu naye akaibe huko?

Back
Top Bottom