Msaada: Nimepewa siku 30 niondoke nyumbani kwa Baba mkubwa

Wana JF wenzangu, nilikuwa nimepanga maeneo ya Kimara miaka kadhaa iliyopita. Kutokana na changamoto ya maisha, kazi nilikuwa sina nikaenda kuishi kwa bamkubwa ili nijipange upya.

Kwa sasa nimekaa miezi minne kwake leo asubuhi kaniambia “nimekupa siku 30 uondoke kwangu”.

Wakuu naombeni msaada wapi pakuanzia? Nifanye nini? Nianzie wapi?
Rudi kijijini
 
Mwaka fulani, nilipoteza kazi nikiwa sina chochote! Nyumbani kwetu kuna nyumba kubwa sana, na kwavile watoto wote ni wakubwa (the youngest is now 26), karibu, except huyu dogo, wana "kwako"! Hata huyu dogo bado yupo home kwavile, as a big brother, nilimwambia asitoke lakini uwezo wa kupanga anao! Ninachotaka kusema ni kwamba, ingawaje nyumba ni kubwa sana lakini ilikuwa inaishi baba, mama, mfanyakazi wa ndani, na huyu dogo huku chumba kimoja na sebule (uani) kukiwa hakuna mtu, na chumba kimoja wakaamua kuweka kuku kwavile na chenyewe kilikuwa hakina kitu! Aidha, kulikuwa na banda lingine kubwa la uani (upande mwingine wa nyumba) ambako walikuwa wanaishi wapangaji ambao ni MMOJA TU ndie alikuwa analipa kodi kwa wakati! Wengine wote walikuwa na sifa ya kutimuliwa!!!

Unaona jinsi ambavyo nilikuwa na "utajiri" wa makazi?! Lakini pamoja na yote hayo, nikagoma katakata kurudi home kwenye nyumba ya bure! Nilichofanya ni kuuza pikipiki yangu na kwenda kupanda sehemu iliyokuwa nafuu zaidi! Usidhani ilikuwa rahisi! Niliishi kwa shida SANA! Mlo mmoja ilikuwa kawaida! Nikipika chai, majani nilikuwa simwagi! Amini usiamini, sufuria ya chai ilibadilika rangi kutokana na kutoisafisha kwa hofu ya kumwaga majani! Mboga yangu ilikuwa maharage, na wala sikuwa na uhakika wa kuyapata! Niliachana na jiko la gesi na kuanza kutumia mafuta ya taa sababu ilikuwa ni rahisi kupata buku 2 ya mafuta ya taa kuliko 15K hadi 18K ya gesi! Si mara moja wala mara mbili kukaa na njaa lakini nikakomaa ingawaje wazazi wapo hai Dar, Sister wangu (hana mume) yupo hai Dar na ana nyumba yake, uncle wangu, yupo hai Dar na ana nyumba yake, Bro wangu akanipatia banda la uani pale kwake Charambe! Lakini kote huko NILIGOMA kwenda!

Leo sina cha kujivunia lakini naweza kulipa kodi ya mwaka mzima! Najua unajua huwezi kulipa kodi mwaka mzima wakati hauna uhakika wa kula!!!

Ninachotaka kusema ni kwamba, ONDOKA hapo unapotimuliwa! kapambane mtaani uingie akili! Huwezi kuwa kula kulala bure halafu ukapata akili ya ku-fight!!
Chai......
 
Wewe ndo umekazana kupiga mahesabu, kiasi cha kutaja bei ya pikipiki, kodi ya nyumba ya zamani na mpya wakati hakuna popote nilipotaja gharama wala bei ya chochote! Sasa kwavile umekomalia hilo suala la pesa unayodhani niliingiza na kutumia, ndipo nakuuliza unajaribu ku-prove nini ikiwa mimi sija-specify chochote kati ya hivyo unavyotaja?! Seems lakini hujiamini kwa kile unachojaribu kueleza!
siasa
 
Mwaka fulani, nilipoteza kazi nikiwa sina chochote! Nyumbani kwetu kuna nyumba kubwa sana, na kwavile watoto wote ni wakubwa (the youngest is now 26), karibu, except huyu dogo, wana "kwako"! Hata huyu dogo bado yupo home kwavile, as a big brother, nilimwambia asitoke lakini uwezo wa kupanga anao! Ninachotaka kusema ni kwamba, ingawaje nyumba ni kubwa sana lakini ilikuwa inaishi baba, mama, mfanyakazi wa ndani, na huyu dogo huku chumba kimoja na sebule (uani) kukiwa hakuna mtu, na chumba kimoja wakaamua kuweka kuku kwavile na chenyewe kilikuwa hakina kitu! Aidha, kulikuwa na banda lingine kubwa la uani (upande mwingine wa nyumba) ambako walikuwa wanaishi wapangaji ambao ni MMOJA TU ndie alikuwa analipa kodi kwa wakati! Wengine wote walikuwa na sifa ya kutimuliwa!!!

Unaona jinsi ambavyo nilikuwa na "utajiri" wa makazi?! Lakini pamoja na yote hayo, nikagoma katakata kurudi home kwenye nyumba ya bure! Nilichofanya ni kuuza pikipiki yangu na kwenda kupanda sehemu iliyokuwa nafuu zaidi! Usidhani ilikuwa rahisi! Niliishi kwa shida SANA! Mlo mmoja ilikuwa kawaida! Nikipika chai, majani nilikuwa simwagi! Amini usiamini, sufuria ya chai ilibadilika rangi kutokana na kutoisafisha kwa hofu ya kumwaga majani! Mboga yangu ilikuwa maharage, na wala sikuwa na uhakika wa kuyapata! Niliachana na jiko la gesi na kuanza kutumia mafuta ya taa sababu ilikuwa ni rahisi kupata buku 2 ya mafuta ya taa kuliko 15K hadi 18K ya gesi! Si mara moja wala mara mbili kukaa na njaa lakini nikakomaa ingawaje wazazi wapo hai Dar, Sister wangu (hana mume) yupo hai Dar na ana nyumba yake, uncle wangu, yupo hai Dar na ana nyumba yake, Bro wangu akanipatia banda la uani pale kwake Charambe! Lakini kote huko NILIGOMA kwenda!

Leo sina cha kujivunia lakini naweza kulipa kodi ya mwaka mzima! Najua unajua huwezi kulipa kodi mwaka mzima wakati hauna uhakika wa kula!!!

Ninachotaka kusema ni kwamba, ONDOKA hapo unapotimuliwa! kapambane mtaani uingie akili! Huwezi kuwa kula kulala bure halafu ukapata akili ya ku-fight!!
Mkuu niunganishe na huyo sista wako
 
Mimi Kama sitaki uje kwangu nitakuwekea kila sababu usikarbie hata geti langu
Ila once nikikubali uje kwangu utakula utakunywa mpka ufanikishe michongo yako ..kua na Tabia nzuri Ni mhumu ukikaa kwa watu
 
sijawahi kukaa kwa ndugu zaid ya siku3,,, hata nipigike vipi siwezi kwenda kuishi kwa ndugu ni bora ninyongwe tu
 
Unamaanisha nini?! Au unadhani nilipata mkwanja wa kuanzia maisha?! Mkuu, dunia ya Mchina bila shaka unafahamu mtu anapozungumzia pikipiki wala hamaanishi Yamaha ambayo anaweza kuuza 3M+! Hiyo pikipiki ilinipatia tu visent vya kumlipa baba mwenye nyumba ili nihame kwa amani, na visenti vingine viliniwezesha kulipa kodi ya miezi 3 TU kwenye makazi mapya, ingawaje Baba Mwenye Nyumba mpya alikuwa anataka kodi ya miezi 6 lakini sikuwa nayo!!
Kwanini hukufanya bodaboda mambo yalipo anza kwenda mrama ??
 
Bodaboda ni 10K isiyo na uhakika kwa siku, wakati nilikuwa nahitajika kulipa deni la kodi ya nyumba niliyokuwa naishi wakati huo huo nilikuwa nahitajika kuhamia makazi mapya yenye nafuu ya kodi!
 
Nilimaanisha wewe mwenyewe kuwa dereva wa hiyo pikipiki yako kwa kufanya kazi ya bodaboda wakati mambo yameanza kwenda kombo. Maana umesema ulikuwa na deni la kodi maana yake mambo yalianza kuharibika kwa myda flani kabla ya kuuza bodaboda na kutakiwa kuhama, haikuwa ghafla, sasa kwanini yukufanya kazi ya bodaboda wewe mwenyewe ??
 
Njoo ukae kwangu ila uje na girl friend wako masharti uwe unaondoka asubuhi unamuacha yeye. Kula bili ya maji na umeme ni juu yangu
 
Back
Top Bottom