Regent
JF-Expert Member
- Oct 9, 2020
- 2,306
- 3,576
Miezi mitatu ya chumba kipya 90K + ya deni la chumba cha mwanzo 90K jumla 180,000 Tzs...So bodaboda uliuza kwa 180,000 ausio.Unamaanisha nini?! Au unadhani nilipata mkwanja wa kuanzia maisha?! Mkuu, dunia ya Mchina bila shaka unafahamu mtu anapozungumzia pikipiki wala hamaanishi Yamaha ambayo anaweza kuuza 3M+! Hiyo pikipiki ilinipatia tu visent vya kumlipa baba mwenye nyumba ili nihame kwa amani, na visenti vingine viliniwezesha kulipa kodi ya miezi 3 TU kwenye makazi mapya, ingawaje Baba Mwenye Nyumba mpya alikuwa anataka kodi ya miezi 6 lakini sikuwa nayo!!