Msaada: Nimepewa siku 30 niondoke nyumbani kwa Baba mkubwa

Msaada: Nimepewa siku 30 niondoke nyumbani kwa Baba mkubwa

Sorry ,kwan una umri gani??? Ulimkosea nn??? Mwambie akupe muda kidogo aiseee mtaani taiti sana yaani!!! Kafuta ya kula lita - 5000/, mchele mzuri kg 2000/ ,chumba 50000/ bado umeme maji nk !!! Nimeuliza mkate asubuhi nikaambiwa 1200/ !??? Ongea na msua alegeze aisee
 
Unafikiri uko peke yako. Hata hao unawasikia wanafukuza au kushabikia mtu kafukuzwa wamepitia huko huko.
Mi sikukulia kwa watu nilikulia home kwetu kukawa daraja kwa ndugu zetu, tulilala chini kupisha wageni, kwanza umnyanyase mgeni utaanzia wapi, mzee kauli yake wageni baraka, alafu usimzarau usiye mjua.
 
Baba mkubwa ana upendo na wewe, anataka uwe mwanaume wa kweli, ukapambane huko duniani.
Kabebe zege, kashushe mizigo kwenye malori, kajitegemee.
Hakuna kitu kibaya kama mtoto wa kiume, kula, kulala bure, huku mkinyang'anyana remote na beki3.
Miezi mi4, inaonekana hujawahi hata kufagia uwanja, au hata kunyanyua sahani uliyolia ukaosha. Upo unaishi ka mfalme.
Si ajabu mpaka nguo zako unampa dada akufulie.

Binafsi ndugu wa kuja kwangu anakaribishwa siku 2,3, la sivyo akae kwao, kama msaada ataupatia huko.
Beki 3, akisumbuliwa ina maana wife naye kasumbuka, na mie nasumbuka.

Everyday is Saturday................................😎
 
Kukaa
Acha kugombania nyama saa ya Kula na vitafunio vya chai asubuhi na watoto wake......atakuwa Tu kapata maelezo kutoka Kwa mama yako mkubwa.....akiwaekea cartoon akina junior kwenye DStv wewe unatoa na unasema unataka mpira kama huwa unalipia king'amuzi Chao.....
Kwa watu unatakiwakujishusha hasa, siyo kujifanya wewe ndo wewe.
 
Duuuh, pambana mkuu hama hapo, mbn inawezekana
 
Duh
Niliwahi kuishi kwa dadangu damu 1 alikua ameolewa...hahaa...jaman maisha haya ..walikua wakipika wenyewe wanaenda kulia chumban na mumewe...nilikua nachota maji najaza pipa 2 ..lakini hom kwetu ni kila kona wafanyakazi..nilikonda kwakweli.inahitaji wito mno!sipend hayo maisha tena
Huyo Dada kiboko shost,
 
Acha kugombania nyama saa ya Kula na vitafunio vya chai asubuhi na watoto wake......atakuwa Tu kapata maelezo kutoka Kwa mama yako mkubwa.....akiwaekea cartoon akina junior kwenye DStv wewe unatoa na unasema unataka mpira kama huwa unalipia king'amuzi Chao.....
🤣🤣
 
Angalau ulikuwa na pakuanzia mkuu vipi kama yeye hana chochote cha kuuza? Afanye nini?
Bila shaka unazungumzia hiyo pikipiki! Mkuu, unajua changamoto haziibuki ghafla, kwahiyo pesa ya hiyo pikipiki zilisaidia kulipa kodi ya miezi 3 TU, na iliyobaki yote, ingawaje haikuwa kubwa, ilitumika kulipa kodi ya nilipokuwa naishi ili hatimae nihame nitafute sehemu nafuu!!! Shukrani zangu kubwa ni kwa Baba Mwenye Nyumba mpya ambae alinipokea nikiwa na kodi pungufu manake alitaka ya miezi 6! Na hata ilipoisha ile miezi 3, sikuwa na ya kulipa, lakini Bwana Yule, Mungu amzidishie, akanivumilia kwa miezi mingine kadhaa! Yaani nilikuwa completely broke! Sasa kama mshikaji alikuwa anafanya kazi, ina maana hakuwa na chochote hata cha kumpatia 100K?
 
Kaka mkubwa BonT kwanini ulikuwa unakataa msaada wa ndugu zako wa karibu katika story yako fupi hapo juu?
Kwa sababu nilihofia kutokea hiki hapa👇👇
Mkuu umekumbusha kipindi kimoja nilikaa kwa father wangu mkubwa ki ukwel nilibweteka sana
Just imagine, nipo home, nakula bure, nalala bure; unadhani ningepambana kiume?! Sana sana ningebaki kutembea na bahasha mkononi kutafuta kazi ya kuajiriwa huku nikiwa sina presha kwa sababu najua, nikirudi home nakuta hotpot la ugali! Kinyume chake ndugu yangu Infantry, kama mwana alivyoeleza kwenye post yake, alifikia hadi kutembeza bidhaa barabarani wakati yupo kwa mshua wake, ali-relax!
 
Mwaka fulani, nilipoteza kazi nikiwa sina chochote! Nyumbani kwetu kuna nyumba kubwa sana, na kwavile watoto wote ni wakubwa (the youngest is now 26), karibu, except huyu dogo, wana "kwako"! Hata huyu dogo bado yupo home kwavile, as a big brother, nilimwambia asitoke lakini uwezo wa kupanga anao! Ninachotaka kusema ni kwamba, ingawaje nyumba ni kubwa sana lakini ilikuwa inaishi baba, mama, mfanyakazi wa ndani, na huyu dogo huku chumba kimoja na sebule (uani) kukiwa hakuna mtu, na chumba kimoja wakaamua kuweka kuku kwavile na chenyewe kilikuwa hakina kitu! Aidha, kulikuwa na banda lingine kubwa la uani (upande mwingine wa nyumba) ambako walikuwa wanaishi wapangaji ambao ni MMOJA TU ndie alikuwa analipa kodi kwa wakati! Wengine wote walikuwa na sifa ya kutimuliwa!!!

Unaona jinsi ambavyo nilikuwa na "utajiri" wa makazi?! Lakini pamoja na yote hayo, nikagoma katakata kurudi home kwenye nyumba ya bure! Nilichofanya ni kuuza pikipiki yangu na kwenda kupanda sehemu iliyokuwa nafuu zaidi! Usidhani ilikuwa rahisi! Niliishi kwa shida SANA! Mlo mmoja ilikuwa kawaida! Nikipika chai, majani nilikuwa simwagi! Amini usiamini, sufuria ya chai ilibadilika rangi kutokana na kutoisafisha kwa hofu ya kumwaga majani! Mboga yangu ilikuwa maharage, na wala sikuwa na uhakika wa kuyapata! Niliachana na jiko la gesi na kuanza kutumia mafuta ya taa sababu ilikuwa ni rahisi kupata buku 2 ya mafuta ya taa kuliko 15K hadi 18K ya gesi! Si mara moja wala mara mbili kukaa na njaa lakini nikakomaa ingawaje wazazi wapo hai Dar, Sister wangu (hana mume) yupo hai Dar na ana nyumba yake, uncle wangu, yupo hai Dar na ana nyumba yake, Bro wangu akanipatia banda la uani pale kwake Charambe! Lakini kote huko NILIGOMA kwenda!

Leo sina cha kujivunia lakini naweza kulipa kodi ya mwaka mzima! Najua unajua huwezi kulipa kodi mwaka mzima wakati hauna uhakika wa kula!!!

Ninachotaka kusema ni kwamba, ONDOKA hapo unapotimuliwa! kapambane mtaani uingie akili! Huwezi kuwa kula kulala bure halafu ukapata akili ya ku-fight!!
Asipokuelewa basii
 
“Niliuza pikipiki”
Unamaanisha nini?! Au unadhani nilipata mkwanja wa kuanzia maisha?! Mkuu, dunia ya Mchina bila shaka unafahamu mtu anapozungumzia pikipiki wala hamaanishi Yamaha ambayo anaweza kuuza 3M+! Hiyo pikipiki ilinipatia tu visent vya kumlipa baba mwenye nyumba ili nihame kwa amani, na visenti vingine viliniwezesha kulipa kodi ya miezi 3 TU kwenye makazi mapya, ingawaje Baba Mwenye Nyumba mpya alikuwa anataka kodi ya miezi 6 lakini sikuwa nayo!!
 
Mwaka fulani, nilipoteza kazi nikiwa sina chochote! Nyumbani kwetu kuna nyumba kubwa sana, na kwavile watoto wote ni wakubwa (the youngest is now 26), karibu, except huyu dogo, wana "kwako"! Hata huyu dogo bado yupo home kwavile, as a big brother, nilimwambia asitoke lakini uwezo wa kupanga anao! Ninachotaka kusema ni kwamba, ingawaje nyumba ni kubwa sana lakini ilikuwa inaishi baba, mama, mfanyakazi wa ndani, na huyu dogo huku chumba kimoja na sebule (uani) kukiwa hakuna mtu, na chumba kimoja wakaamua kuweka kuku kwavile na chenyewe kilikuwa hakina kitu! Aidha, kulikuwa na banda lingine kubwa la uani (upande mwingine wa nyumba) ambako walikuwa wanaishi wapangaji ambao ni MMOJA TU ndie alikuwa analipa kodi kwa wakati! Wengine wote walikuwa na sifa ya kutimuliwa!!!

Unaona jinsi ambavyo nilikuwa na "utajiri" wa makazi?! Lakini pamoja na yote hayo, nikagoma katakata kurudi home kwenye nyumba ya bure! Nilichofanya ni kuuza pikipiki yangu na kwenda kupanda sehemu iliyokuwa nafuu zaidi! Usidhani ilikuwa rahisi! Niliishi kwa shida SANA! Mlo mmoja ilikuwa kawaida! Nikipika chai, majani nilikuwa simwagi! Amini usiamini, sufuria ya chai ilibadilika rangi kutokana na kutoisafisha kwa hofu ya kumwaga majani! Mboga yangu ilikuwa maharage, na wala sikuwa na uhakika wa kuyapata! Niliachana na jiko la gesi na kuanza kutumia mafuta ya taa sababu ilikuwa ni rahisi kupata buku 2 ya mafuta ya taa kuliko 15K hadi 18K ya gesi! Si mara moja wala mara mbili kukaa na njaa lakini nikakomaa ingawaje wazazi wapo hai Dar, Sister wangu (hana mume) yupo hai Dar na ana nyumba yake, uncle wangu, yupo hai Dar na ana nyumba yake, Bro wangu akanipatia banda la uani pale kwake Charambe! Lakini kote huko NILIGOMA kwenda!

Leo sina cha kujivunia lakini naweza kulipa kodi ya mwaka mzima! Najua unajua huwezi kulipa kodi mwaka mzima wakati hauna uhakika wa kula!!!

Ninachotaka kusema ni kwamba, ONDOKA hapo unapotimuliwa! kapambane mtaani uingie akili! Huwezi kuwa kula kulala bure halafu ukapata akili ya ku-fight!!
Ulikua ushapata familia wakati huo?
 
Wana JF wenzangu, nilikuwa nimepanga maeneo ya Kimara miaka kadhaa iliyopita. Kutokana na changamoto ya maisha, kazi nilikuwa sina nikaenda kuishi kwa bamkubwa ili nijipange upya.

Kwa sasa nimekaa miezi minne kwake leo asubuhi kaniambia “nimekupa siku 30 uondoke kwangu”.

Wakuu naombeni msaada wapi pakuanzia? Nifanye nini? Nianzie wapi?
Ushaharibu tayari.....kwanza ungemshukuru huyo Baba yako mkubwa badala ya kuja humu kwa panic. Una umri gani?
 
Back
Top Bottom