Msaada: Nimewapa ujauzito wanawake wawili, nawapenda ila dini yangu hairuhusu kuwa na wake wawili

Kwahio leo ndo unajifanya unawaza dini?

We si hukuweza tulia na mmoja?
Oa wote kanisani
Serikali haijakukataza

Afu tulie ufurahie vita ya wake wenza na miji miwili
 
Labda niendelee kumuhudumia na huko kwao huyo mzee wa boma ntamdamganya vipi huyu binti S
Unamdanganya wa nini ss
Waeleze wote ukweli kuwa unaoa wote na kila mtu atakua na mji wake , upange zamu na utende haki sio kunyanyasa watu
 
Na haya majibu ya " braza tafuta ela"
Nikipata ela nisije sikia lawama kokote pale mana nitazaa na wanawake 10+ tena ikibidi kwa mpigo
 
Wanaume ni viumbe wa ajabu sana

[mention]Lovelovie [/mention] Mi sioni chakushangaa kabisa, maandiko ya dini zote yamekataza kuzini kabla ya ndoa na wote kumtanguliza mungu ndani ya ndoa kwaiyo lazima ue muumini kwanza wa dini husika ndo ufunge ndoa.

Kimsingi binadamu tushajiamulia system zetu wenyewe katika mahusiano zinazotupa raha matokeo yake ndo kuzalisha masingo mom wengi ambao washavurugwa na wanahate na kitu kinachoitwa mapenzi &wanaume, note HAYA NI MAKOSA YENU WENYEWE WANAWAKE MSIMLAUMU MTU., apo kwanza kakosewa mungu then wanaona wamekosewa wao, naamini sio muda mrefu dada ambaye atazaaa mtoto wakike na hasipopata nafasi yakuolewa ni atachukia Mapenzi&Wanaume then atapandikiza chuki kwa watoto wake, wengi huwaaminisha watoto wao pesa ndo kilakitu na wachache hutulia ila wengi kwa hasira huanza kutafuta pesa kwa namna yoyote na ni kazi kuwatuliza nahata kuwashauri maana washaumizwa so hawataki kusikia uongo mwingine, watoto wao pia watasikia ila hawatoelewa ya mama zao(maranyingi hua ivo) kwa maana hajawahusiwa ya dini ila wamehusiwa kwa chuki za mama zao binafsi then na watoto watapata mimba either kwakupenda au kudanganywakama mama zao na watateswa na mapenzi na wengi wataishia kuona KAZI & KUDANGA ni bora kuliko kuolewa na wanaume, Pia wanaume tutasema HAWA WANAWAKE SIO WATU
maana hatutaelewa akili za wanawake wetu (KUTOKANA NA UZINIFU KUTAWALA HATUTOJUA KOSA LIMEANZIA WAPI) na tutaona ni bora kununua dada poa kuliko kuoa maana wanawake wasaivi ni wahuni tuuu kwanza wanapenda ela!!! End of the day SHETANI ANAZIDI KUCHUKUA POINT ZAKE TARATIIIBU UKU AKISUKUMIZIA NA KAMZIKI KA HARMONISE[emoji344]AMELOWA.

#Mwanaume sio kiumbe cha achabu binadamu ndo kiumbe cha ajabu.

#TUELIMISHANE.

#KUNIKOSOARUKSA.
 
Dini yako inaruhusu kumpa ujauzito ambaye sio mkeo?
 
Ni kweli, kwa kuwa tumeamua kuchagua njia ya maisha ambayo iko kinyume na aliyoamrisha Mwenyezi Mungu, basi tusilaumu ila nafsi zetu wenyewe. Haya yote yanatutokea katika dhiki, visirani miongoni mwetu, mara huyu kazalishwa na kutupwa, mara panya road na kukosekana amani, mara mauaji yasiyo na kichwa wala miguu huyu kamuua mama yake yule kamuua mkewe, mara baba kambaka binti yake na mengineyo. Uharibifu huu unatokana na yale yanayochumwa na mikono yetu. Na kwa Imani yangu ninafundishwa kuwa Mwenyezi Mungu habadilishi yale yaliyoko kwa watu mpaka wao wabadilishe yale yaliyoko katika nafsi zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…