Hello JF Members,
I'm madam Agnes, leo tena humu Jukwaani. Nisiwachoshe, niko na 30k kwenye kipochi, nahitaji kuanza biashara yoyote ile itakayowezekana sasa hivi
Mazingira ni Dar es salaam. Siko na aibu, naeza fanya yoyote ile. Ilimradi tu itoshe kunipatia mlo pamoja na saving kidogo kwa ajili ya masuala ya baadae
Sihitaji kuajiliwa, maake naondoka hivyo kwenye nyumba ya watu nilipokuwa naishi as house girl, watu hawana shukhrani jamani
Mwenye wazo lolote lile ambalo limemsaidia kuendesha maisha, ama ameona limemsaidia somebody ku run his/her own life anipatie basi. Hata kama ni idea ya kiume, I'm ready
I'm waiting...
una nia na malengo mazuri sana hata kama si wewe...
Nimeona apo juu, kwa uchache, ushauri mzuri sana wangwana wa JF wameuporomosha....
A serious human being akiaamua kuuchukua ushauri huo na kuufanyia kazi, anatoboa vizuri sana within short, middle and long period of time...
Hiyo hela sio kidogo, ukiamua ukanunua na ukafungasha mathalani karanga za mia1, mia2 na mia5, ukaongeza na peremende, pipi, sigara na bigG kwa kuanzia, mbona umejipatia ajira yako mwenyewe tayari..
Lakini pia ukafungasha maji ya mia mia, maarufu maji ya kandoro, tunayabwia sana humu kwenye vijiwe vya boda daladala, kahawa na sokoni. Wateja wapo, soko lipo kwa uwekezaji mtaji kama huo ulonao.
Lakini mwingine ameshauri wekeza kwenye nguo za ndani za kike na kiume mathalani chupi, socks , boxer, singland, tyty, sidiria n.k .Aise huku maofisini maofsaa wanapitanazo mbaya sana. Hawana muda kwenda madukani. Lakini pia mtaani zinauzika sana na haziozi...
So,
kwa uwekezaji wa mtaji huo, unaweza kufanya dogo likawa kubwa. Likakufurahisha na kukunufaisha wewe na wengine pia.
Cha muhimu zaidi ni kua na nia thabiti na uthubutu wa kuamua na kutenda.
Nakutakia kila la Kheri.
Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi...