Msaada: Nina 30,000 hapa, nahitaji kuanza biashara yoyote ile sasa hivi. Niko DSM

Ha ha we jamaa una kitu, itabidi nije pm!
 
Kha! Marafiki zangu wote wakiokimbilia huko wameharibikiwa, hata yule Nasra mtoto wa Ostadhi sasa hivi ukimuona huezi dhania. Nina mashaka keshautwaa. Uko sio pazuri kaka yangu
 
Hongera kwa uthubutu Mkuu, ni Wanawake wachache wa kizazi hiki cha Instagram kinaweza kuthubutu kufanya hicho unachojaribu kukifanya.

Nenda Soko la Mabibo ama Sterio ununue Matunda Mchanganyiko ya shilingi 15,000.

Tumia elfu 8 ununue deli pamoja vifungashio pamoja na Kisu.

Baada ya hapo anza biashara yako ya matunda kwa kuyapitisha kwenye maofisi hapo Posta.

Kama utatia bidii, utakuwa na miezi 6 hivi utakuwa na mabinti zako 3 ambao utakuwa umewaajiri kwa biashara hiyo hiyo huku mtaji ukikua mara dufu.

Zingatia usafi na unadhifu wa mavazi.


Kila la kheri Mkuu
 
una nia na malengo mazuri sana hata kama si wewe...

Nimeona apo juu, kwa uchache, ushauri mzuri sana wangwana wa JF wameuporomosha....

A serious human being akiaamua kuuchukua ushauri huo na kuufanyia kazi, anatoboa vizuri sana within short, middle and long period of time...

Hiyo hela sio kidogo, ukiamua ukanunua na ukafungasha mathalani karanga za mia1, mia2 na mia5, ukaongeza na peremende, pipi, sigara na bigG kwa kuanzia, mbona umejipatia ajira yako mwenyewe tayari..

Lakini pia ukafungasha maji ya mia mia, maarufu maji ya kandoro, tunayabwia sana humu kwenye vijiwe vya boda daladala, kahawa na sokoni. Wateja wapo, soko lipo kwa uwekezaji mtaji kama huo ulonao.

Lakini mwingine ameshauri wekeza kwenye nguo za ndani za kike na kiume mathalani chupi, socks , boxer, singland, tyty, sidiria n.k .Aise huku maofisini maofsaa wanapitanazo mbaya sana. Hawana muda kwenda madukani. Lakini pia mtaani zinauzika sana na haziozi...

So,
kwa uwekezaji wa mtaji huo, unaweza kufanya dogo likawa kubwa. Likakufurahisha na kukunufaisha wewe na wengine pia.

Cha muhimu zaidi ni kua na nia thabiti na uthubutu wa kuamua na kutenda.
Nakutakia kila la Kheri.
Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi...
 
Mtaji hautoshi kaka angu. Vifaa vyenyewe huna 40k hupati, eneo la kukaangia je?

Nilipoanza kusoma hiki kifungu, moyoni nilijiambia naweza kukusaidia kuongeza mtaji...

We ni zaidi ya Motivational Speaker

Conclusion yako ikaniondolea hiyo huruma ya mwanzo...

Anyway kila la kheri, Mungu akusaidie ufanikiwe...
 
Thanks 🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…