Msaada: Nina presha 162/103 umri wangu miaka 33. Je, nianze dawa au nibadilishe lifestyle?

Sasa mbona unamwambia aishushe mpk 140 hapo hapo asiiache ifike 130
BP ina presentiwa hivi SBP/DBP
Kwa mfano 140/90
DBP maana yake Diastolic Blood Pressure na kwa mfano huo ni 90
SBO maana yake Sytolic Blood Pressure na kwa mfano huo ni 140

DBP kupanda kwa DBP kuna mahusiano na kuwa na Bad outcome but not in all cases
 
Cheki sugar maana Presha na Sugar ni mtu na mpwa wake !!
 
Ukifata huu ushauri hatojuta
 
SBP ikiwa imakaa kwenye 142 na DBP 82 VIPI hapo unaweza kuwa na hofukuwa pressure iko juu?
 
Wakuu habari zenu,

Kama nimevoandika hapo juu nimepima presha Leo na presha yangu ni kama hiyo nlioandika Ila sikuwahi kuwa na presha. Sasa wakuu ushauri wenu nianze dawa au nianze lishe ya kuacha wanga na sukari?
Kwanza wewe unahisi Nini mwilini mwako mkuu
1.Kama ulipima Mara TU baada ya kufika Hapo ulipopimia kipimo majibu hayo SI sahihi
2.Kama ulipima ukiwa na njaa majibu hayo SI sahihi
3.UZITO WAKO NI KG NGAPI?
 
Juzi usiku nlipika chapati za Maji nliweka sukari Na chumvi nikala nlivomaliza nikashushia Na Pepsi nikaenda kulala usiku kwenye SAA 9 nliharisha Sana tangu Muda Huo mpaka Sasa najisikia Vibaya nkilala nahisi kama Moyo unaelemewa nakosa pumzi pia nahisi kama kitu kina nichoki shingoni
 
mrembo ulitakiwa ule matunda ulale unaona sasa yatakukuta mengi zaidi
 
Wakuu habari zenu,

Kama nimevoandika hapo juu nimepima presha Leo na presha yangu ni kama hiyo nlioandika Ila sikuwahi kuwa na presha. Sasa wakuu ushauri wenu nianze dawa au nianze lishe ya kuacha wanga na sukari?
Mimi kama muathirika wa shinikizo la damu kwa miaka arobaini sasa na kutibiwa JKCI na kufanyiwa vipimo vyote na shinikizo langu ni chini ya yako natumia dawa Kila siku miongo mitatu sasa.
BP ya juu hailetwi na lifestyle pekee huenda kama mimi nilivyo ni hitilafu kwenye moyo.
USHAURI: Nenda hospital kafanye vipimo vyote hasa vya ECHO na umeme wa moyo pia Chunga lifestyle yako haswa pombe.
 
Hivi presha nayo huwa ya kurithi
 
hiyo pressure kwa wewe siyo labda mtu mwenye miaka 60 kwenda juu
 
Acha wanga na sukari kabisa , anza kwenda gym lift weight, piga aerobics ndani ya miezi 3 utajihisi kama kijana wa miaka 23
Nina miezi 6 leo bila kutumia sukari. Nafanya steps aerobics nyumbani aisee hata enzi za ujana sikuwa hivi. Sitii sukari kwenye chai, sinywi tena soda, keki wala ice cream. Wala asali. Nimepunguza ubwabwa na ugali. Nakamata mdudu na nyama choma nasindikiza na wine glass moja. Makunyanzi ya uso kwisha. Ninashangaa hata siamini. My belly fats zimepungua dramatically. Weka bundle halafu bofya hapa

View: https://youtu.be/-si1MZD5MFE?si=7wX1kOfQABtfRSG4
 
Pole Sana Ni vyakula Gani unakula kumaintain afya yako
 
Kinywaji chako ni Nini hasa Mkuu.... breakfast yako lunch Na dinner zikoje
 
Acha sukari na Kila kinywaji cha sukari utakuja kunishukuru humu.


Niliacha kula sukari tangu mwaka 2017 nimeshuhudia mabadiriko makubwa sana kiafaya. Makubwa mno!


Punguza uoga fanya maamuzi magumu. Acha kula Bidhaa kula Vyakula. Bidhaa ni mavyakula yenye kemikali kama Coca-cola, chocolate n.k na vyakula ni Vitu fresh kama viazi , mohogo n.k
 
Elimu ya Lishe ni muhimu sana sana sana!


Hivi usiku unawezaje kula CHAPATI na Pepsi MLS 375 yenye masukari vijiko 10. Yani unakula mawanga na masukari Tena usiku. Hapo lazima upate likitambi. Ulale kama unakimbizwa au upate maluwe luwe.


Piga chini sukari kula kiafya.
 
Safi sana mkuu , Huwa nawashangaa watu wanamcheka Dr Janabi eti wanashindwa kuacha kula sukari.

Sukari ya kiwandani ni Jini inasababisha matatizo mengi sana sana Kwa Binadamu ni vile watu tumeshaingia kwenye chain kutoka ni ngumu.

Mtu akiacha kula sukari ndani ya mwezi mmoja ataona mabadiriko mengi sana sana. Kubwa zaidi ukiacha sukari ni Moja ya njia za Anti-aging. Utaonekana kama hukui kumbe umri unaenda.

Leo unakuta mtu anakunywa soda Kila siku na keki na mavyakula mengine ya sukari. Mtu anakuwa na miaka 25 ila anaonekana kama ana miaka 60. Hatari sana!

Mimi tangu mwaka 2017 sijawahi kuweka sukari mdomoni kwangu! Sina kitambi.


Tangu mwaka 2017 sijawahi kunywa hata hiyo chai ya asubuhi sijui. Na nimeshasahau kama watu Huwa wanakula asubuhi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…