Msaada: Nyoka Mkali anazunguka Mazingira ya Nyumbani

Kwa mujibu wa maelezo yake nwanafunzi aligogwa kwenye kiatu mkuu..
 
Mwambie tu anitafute, mimi nakula nyoka na ninawawinda.
 
Pia amwage mbolea ya chumvichumvi.
Ila wawe makini, wasije wakamuua halafu wakaonekana kuwa wamemuua, maana nyoka ni nyara ya serikali kwa mujibu wa Kigwangara, au kama watamuua basi wasiwe na itikadi ya upinzani
Maana unaweza kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi
 
Mtoa mada sio kwamba Kuna ujumbe anaufikisha kupitia nyoka [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Mimi naonaga kwangu wa aina tatu wa kwanza ni wa kijani warefu na wa pili ni weusi wafupi pia na wa tatu ni silver flani hivi wanarangi kama tofali au cement nipo dar goba
wewe huko Goba kawaida kukutana na viumbe hivyo Kuna mwaka Kama sikosei 2018 chui alionekana huko huko kamanda hivi walimwona kweli maana hawakuleta update wana maliasili!
πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mimi naonaga kwangu wa aina tatu wa kwanza ni wa kijani warefu na wa pili ni weusi wafupi pia na wa tatu ni silver flani hivi wanarangi kama tofali au cement nipo dar goba
wewe huko Goba kawaida kukutana na viumbe hivyo Kuna mwaka Kama sikosei 2018 chui alionekana huko huko kamanda hivi walimwona kweli maana hawakuleta update wana maliasili!
πŸ˜‚πŸ˜‚
 
NENDA OFISI ZA MALIASILI WAAMBIE KUNA CHATU KAVAMIA ENEO LANGU. WATAKUJA KUMTOA KIRAHISI TU.
BAADA YA HAPO FYEKA ENEO LOTE KUZUNGUKA NYUMBA. ONDOA MAJANI NA MAUA YOTE KARIBU NA NYUMBA YAKO.
 
Sidhani kama ni kweli, mimi nilichoma juzi baada ya kuona nyoka chooni kwangu ila hakutoka hadi leo vinginevyo iwe alifia humo baada ya kuchoma maana hakuonekana kabisa.
Huwa wanatoka. Vinginevyo alizidiwa akafia hukohuko or kama choo kina upenyu alipita hukohuko.
 
Paka na kuku wote wananua nyoka lakini inategemea zaidi nani kamuwahi mwenzake na ukubwa wa nyoka. Kama nyoka ni mkubwa na sumu kali basi kuku na paka hawapindui. Kwa maelezo ya mtoa mada kama kweli kuna paka kauliwa na huyo nyoka basi huyo nyoka ni mkubwa na ana sumu kali kwa hiyo inahitajika tahadhari kubwa sana. Na mbaya zaidi kwa nyoka wakubwa kam hao huwa na makazi ya kudumu kwa hiyo huyo nyoka atakuwa na makazi yake hapo hapo jirani kwa hiyo anatoka anakula halafu anarudi kwenye makazi yake anatulia. Salama yenu ni kujua wapi ndio makazi yake ambalo ni jambo gumu sana kwenu.

Jaribuni kutumia njia zifuatazo ili kumfukza kwenye haya mazingira ya kwenu:-
1. Tafuta kampuni ya "fumigation" ya kueleweka ipulize madawa makali ndani ya nyumba na nje ya nyumba. Kama hamuwezi hizo gharama za kampuni basi mnaweza kununua oil chafu mkachanganya na dizeli kidogo mkamwaga kuzungua kwenye kuta za nyumba na pembeni ya kiwanja chenu (japo sio njia nzuri kwani inaharibu mazingira)
2. Punguzeni matawi ya miti juu zaidi ya uswa wa vichwa vyenu, maua (ikiwezekana ng'oeni kwa muda hali ikitulia mtapanda tena upya) na fyekeni majani yote kuzunguka mazingira ya nyumba zenu kwani nyoka hapendi kabisa sehemu zilizo wazi - kwa ufupi hapendi kuonekana kirahisi.
3. Chomeni matairi au taka za plastiki mara kwa mara nje ya nyumba zenu japo hii pia sio njia sahihi kimazingira.

Tahadhari za kuzingatia
1. Chukueni tahadhari sana mara mnapoona wanyama kama mbwa, paka, kuku, kanga n.k. wanapotoa milio isiyo ya kawaida au mkikuta wamekufa katika mazingira ya kutatanisha.
2. Mjitahidi sana muwe na "gumboot" na uzivae pale unapoingia kwenye mabanda ya kuku au kwenye bustani za mboga na maua. Unaweza kwenda mabanda ya kuku kutoa mayai kumbe nyoka naye kaingia kula mayai/kuku au unaweza kwenda kuchuma mboga za majani kumbe nyoka naye kaenda kula vyura/mijusi ndio hapo hatari ilipo.
3. Ukisikia ndani ya nyumba kuna kelele/sauti zisizo za kawaida kama unaishi maeneo yenye nyoka chukua tahadhari kwani mara nyingine nyoka huingia ndani kufuata panya au wanakuwa wameingia ndani kutafutwa hifadhi baada ya kufukuzwa na wababe wenzao huko nje ya nyumba
 
Nauliza tu. Tanzania hamna wahusika wa kusaka nyoka majumbani kama vile tunavoona kwenye National Geographic huko Ulaya. Maana inaonekana kuna mbinu na vifaa zinahitajika kwa ajili ya kutoa nyoka kama hao. Kuna watu wanawasomea hawa wadudu. Wanajua sifa zao, hatari zao n. K
 
Kama paka alimjeruhi huyo nyoka basi atakuwa keshakufa.

Kwa mujibu wa wataalamu, nyoka akijeruhiwa kiasi cha kutoka damu hawezi kuishi maana kadiri anavyotembea, kwa mwendo wake wa kujinyonga jeraha linazidi kuwa kubwa.

Vv
 
Nyoka kwa kuku hasogei labda wa kizungu, kuku anaua nyoka! Choma Tyre mwaga disel. Mmefanya kosa kubwa kuhama mmempa utulivu na nafasi ya kutafuta makazi yake vizuri.
Sio kweli mkuu, huyo atakuwa nyoka mdogo, nyoka aliyekomaa ana ngozi ngumu, tena nyoka wengine kuku ni chakula kwao.

Vv
 
Pia amwage mbolea ya chumvichumvi.

Ila wawe makini, wasije wakamuua halafu wakaonekana kuwa wamemuua, maana nyoka ni nyara ya serikali kwa mujibu wa Kigwangara, au kama watamuua basi wasiwe na itikadi ya upinzani.
Kama Ni nyara ya serikali watampeleka kwa kigwa akaishi nae kwake
 
Nyoka anayeweza kula kuku mzima ni Nyoka mkubwa sana
Jamii ya Chatu au Gaboon adder
 
Ndio maana sipendi bustani la maua, sana sana ya kijani karibu na makaazi karibu na mimi. Wadudu hao wanapenda sana. Choma tyre kila kona ya nyumba kwa nje, ikiwezekana chukua kipande kidogo cha tyre inayotoa Moshi na uiweke ndani ya ghetto kisha funga mlango kwa nje,moshi utapakae ndani. Hao kuku wajengee banda la kisasa tu, mchana unawaachia huru kwani pia nao ni wazuri kwa kupambana na vijoka vidogo(I've experienced it). Pia ukipata oil chafu, iwe ya pikipiki au gari, nyunyizia kwenye fence ya compound kote, sana sana entry points(mlangoni, nyuma au mbele). Hio miua ya kijana, kata kata yote (Green Mamba hupendelea hiyo mijana kujificha).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…