Msaada tafadhali - Kifungu cha 31(10) cha sheria ya kazi na mahusiano kazini kinanichanganya

ThnkingAloud

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2017
Posts
611
Reaction score
621
Kifungu cha Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini Sura 366, Toleo Rekebu 2019 kinasema hivi:

- 31(10) The pro rata amount of annual leave referred to in subsection (8) shall be calculated at the rate of one day’s basic wage for every 13 days the employee worked or was entitled to work.

Na kifungu cha 8 cha sheria hiyo hiyo kinasema hivi:

- 31(8) An employer shall pay an employee a pro rata amount for annual leave accrued-

(a) subject to the provisions of subsection (9), at the termination of employment; or

(b) at the expiry of each season in respect of an employee employed on a seasonal basis.

Kama basic salary ni shilingi 3,000,000 mfanyakazi atalipwa kiasi gani kama accrued leave ni siku 13? Je kama ni siku 28 atalipwa kiasi gani? Naona maluweluwe hapo.

Msaada tafadhali.
 
Kwa ushauri mzuri kama humu hutopata wa kujibu nenda TUCTA! au vyama vya wafanyakazi!
 
Cha kwanza, gawanya basic salary kwa siku 26 (normal working days) kupata wage yako ya siku moja ($)

Cha pili, kwa kila mwaka uliohudumu na kuutimiliza mwajiri anapaswa kukulipa 28 days of accrued leave

• Suppose umehudumu kwa miaka 6, maana yake ni 28 × 6 × wage yako ya siku ($)

• Suppose umetumikia kwa miaka 2, maana yake ni 28 × 2 × wage yako ya siku ($)

Hii ni kwa nchi ambayo sheria ya mahusiano na ajira kazini imeainisha accrued leave kwa mwaka kuwa ni siku 28, kwa nchi ambayo ni 13 au 14 au 21 nakadhalika unazidisha hivyohivyo kwa kuzingatia idadi ya siku
 
Tafsiri nyepesi ya accrued leave, ni idadi ya siku ambazo mtumishi hustahili kupata likizo ya siku moja kila anapozitimiliza au anapowajibika kuzitumikia, mfano; umenukuu kwa bongo accrued leave ni siku 13, maana yake kila utakapohudumu kwa muda wa siku 13 unastahili kupata likizo ya siku moja (1) ambayo hugeuzwa kuwa malipo ya kifuta jasho kwa wage yako ya siku
 
Hii umenichanganya zaidi mkuu. Ni kama unataka kusema Kiinua Mgongo [Severance Pay - Section 44(1)(e) R/W Section 42(1)] kama sijakosea. Hata hivyo kwa Kiinua Mgongo siku 28 hazitakiwi kuwa kwenye hiyo fomula badala yake ni siku 7.
 
Tafsiri nyepesi ya accrued leave, ni idadi ya siku ambazo mtumishi hustahili kupata likizo ya siku moja kila anapozitimiliza au anapowajibika kuzitumikia, mfano; umenukuu kwa bongo accrued leave ni siku 13, maana yake kila utakapohudumu kwa muda wa siku 13 unastahili kupata likizo ya siku moja (1) ambayo hugeuzwa kuwa malipo ya kifuta jasho kwa wage yako ya siku
Accrued leave ni siku za likizo ulizopata kwa muda uliofanya kazi kabla ya mzunguko wa miezi 12 kukamilika (Leave Cycle). Ukishakamilika na kuanza mzunguko mwingine wa miezi 12 haiitwi tena Accrued leave inaitwa leave carried-forward na accrued leave ni kwa mzunguko mpya wa miezi 12 ambao pia haujakamilika. Huu ndiyo uelewa wangu.
 
Back
Top Bottom