Msaada tafadhali,Kipato cha binti cha mtoa nduki jamaa..!

Sasa Canta wewe mwenyewe mtazamo kuhusu mapenzi/ngono ndio huo hapo (wa mwanaume kuwa anafaidi) halafu unashangaa jamaa kuchapa mwendo............Trust me bado tuna safari ndefu ya kurekebisha mfumo wa watu kufikiri.
Dah, nakweli,
Yani hata sijui ianzie wapi na ni lini tutafika,
Mpaka huwa najiuliza hv mwanaume wa aina hii huwa anataka nn hasa kwa mwanamke?
 
i wanted to ask the same mkuu ... nashangaa canty anatetea vitu vingine ambavyo havipo katika uzi ... mfano amejuaje tabia za huyu dada??
Ni mtu wangu karibu sn,
Na kila nilichoandika ni cha ukweli huwezi amini,
Na pamoja na huyu binti kubahatika kupata kazi nzuri na inayomlipa vizuri wala sio aina ya mabinti wa mjini wachakaramu kutokana na malezi aliyolelewa!
Ndio maana namtetea sn kuhusu tabia yake,i know her.
 
Labda amewahi kuonywa na watu wazima juu ya wanawake wenye fweza au amewahi shuhudia kidume akiwa humiliated kisa mali...ila binafsi nina mifano halisi mingi nyie bamtu yani mkipata gape hasira unazimalizia kwa mmeo nakwambia

ukiona mwanamke anapesa kuliko mwanamme na ana mnyanyasa mme wake tafuta mchawi ni nani lakini kama mwanaume atasimamia jukumu lake la uanaume katika familia, kumuheshimu mke wake na watoto mwanamke hata akiwa na hela kama Bill Gate atamuhemishu. lakini kama ulikuwa unamnyanyasa na kumtupia vijimaneno nyumbani huonekani ukirudi usiku ni matusi, hamkai pamoja kudiscuss family matters am telling u, huyo mwanamke akiwa na pesa atakunyanyasa mpk uone rangi zote. otherwise nimeona nyumba nyingi tu ikiwemo ya wazazi wangu mama ana kipato kuliko baba lakini heshima iko mbele kwa kuwa mwanamme ana play part yake. sio mtoto anakuomba hela ya nguo unamjibu nenda kwa mama yaani hapo hata mtoto atakudharau. lakini kama unamawasiliano vizuri na mkeo na huna kipato hata mtoto akiomba hela utamwambia subiri tudiscuss mama yako then tutakupa. hayo ni mawazo yangu
 
nimesoma uzi huu nikakumbuka mbali sana....hali hii iliwahi kunikumba mimi ila mimi sikufanya kama huyu bwana alivyofanya....mi baada ya kujua kuwa mwenzangu yuko juu sana kwa kweli ilibidi nijiongeze namna ya kufikiria na namna ya kuongea kipato......bila kumwambia wala nini nilianza kuchakalika sana a kilichorahisisha ni kwamba nilikuwa natumia usafiri wake..kwa kuwa tulikuwa tunakaa mikoa miwili tofauti...nilihakikisha kila akija anakuta maendeleo flan....nakumbuka alikuja mda flani akakuta nafuga kuku wengi sana na nimeajili mtu wa kuwahudumia akafurahi sana.....mimi kimya.....
akaja wakati mwingine nimenunua shamba na nikampeleka kwenda kuliona...kule shamba nikawa nafuga ng'ombe wa kisasa nako nikaweka mtu.....kwa kuwa tayari nilikuwa na kibanda cha kuishi nikaenda bank nikachukua mkopo wa maana..nikaenda iringa nikaaanza kusafirisha mbao naleta dar buguruni....mtaji ukakua nilifanya kazi ile kwa miezi kama 6...hakika nilipata faida kubwa sana......wakati nafanya yote haya mwenzangu nae alikuwa nashughuli zake(mabotique 3, saluni 4 zote ziko dar) nashughuli kibao na nyumba moja kapangisha......
baada ya kujiridhisha nae na kwa kuwa alikuwa na mawazo chanya kwangu nikaridhika nae sana......baada ya miaka miwili nikamvika pete na tukaunganisha mali zote aliochuma yeye na mimi ....baadae nikasafiri nikaenda kuongeza shule kidogo huko italy huku yeye akisimamia miradi yangu na yake ujenzi wa nyumba yangu na mwaka jana tar 8 september tulifunga ndoa na ndoa yetu tulifungia italy na ni kati ya ndoa zilizofungwa na baba ntakatifu Benedict wa 16......sasa tupo katika nyumba niliyojenga mimi tunaishi, nyumba alizojenga yeye wakati yuko alone zimepangishwa zote na tunaishi salama na maisha yanakwenda vizuri sana....namshukuru Mungu mama blanca alinipa changamoto nyingi sana juu ya maisha ..

kikuwa nilichokuwa nawaza ni kwamba huyu anawezaje na kwa nini mimi nishindwe!!!? na hakika kwa kiasi nilicho nacho nakwa maisha tunayoishi namshukuru Mungu....

huyu kijana mwenzangu aliyekimbia hana changamoto..hataki kujifunza na mvivu wa kujishughulisha ndo wale wanaosubiri mishahara ya kila mwezi pasipo kujishughulisha.....unakimbia mwaanamke kisa ana kipato kukuzidi?!!!
 
tuambie tu kama ulishampa mzigo halafu jamaa akachpa lapa ... lo
Haaa haaa haaaa!
Wala sio mm bwana,
Ingekuwa mie wala nisingelia lia,huyu jamaa ni kivulana tu sio type yangu kbs,
Mie ningemshukuru,na kumpa mwanaume nafasi lol!
 
haya kwa hiyo tukae mkao wa kuendelea kusubiri ...

wewe kama wewe ulimshauri vipi suala lake??
Mie nimemwambia aachane naye huyo jamaa ana tabia za kitoto,
Ila ndio hivyo hataki ushauri wa kuachana anataka ashuriwe namna ya kurudiana naye!
 
kama huyo jamaa amekimbia kisa uwezo wa mali wa huyo binti basi ni mjinga sana...ila kama ameota tatizo lingine kwa binti mwenyewe personaly nje ya mali zake hapo naweza kuelewa....
 
Mie nimemwambia aachane naye huyo jamaa ana tabia za kitoto,
Ila ndio hivyo hataki ushauri wa kuachana anataka ashuriwe namna ya kurudiana naye!

haha angalia mwisho wa siku utapewa kazi zaidi
 
nimesoma uzi huu nikakumbuka mbali sana....hali hii iliwahi kunikumba mimi ila mimi sikufanya kama huyu bwana alivyofanya....mi baada ya kujua kuwa mwenzangu yuko juu sana kwa kweli ilibidi nijiongeze namna ya kufikiria na namna ya kuongea kipato......bila kumwambia wala nini nilianza kuchakalika sana a kilichorahisisha ni kwamba nilikuwa natumia usafiri wake..kwa kuwa tulikuwa tunakaa mikoa miwili tofauti...nilihakikisha kila akija anakuta maendeleo flan....nakumbuka alikuja mda flani akakuta nafuga kuku wengi sana na nimeajili mtu wa kuwahudumia akafurahi sana.....mimi kimya.....
akaja wakati mwingine nimenunua shamba na nikampeleka kwenda kuliona...kule shamba nikawa nafuga ng'ombe wa kisasa nako nikaweka mtu.....kwa kuwa tayari nilikuwa na kibanda cha kuishi nikaenda bank nikachukua mkopo wa maana..nikaenda iringa nikaaanza kusafirisha mbao naleta dar buguruni....mtaji ukakua nilifanya kazi ile kwa miezi kama 6...hakika nilipata faida kubwa sana......wakati nafanya yote haya mwenzangu nae alikuwa nashughuli zake(mabotique 3, saluni 4 zote ziko dar) nashughuli kibao na nyumba moja kapangisha......
baada ya kujiridhisha nae na kwa kuwa alikuwa na mawazo chanya kwangu nikaridhika nae sana......baada ya miaka miwili nikamvika pete na tukaunganisha mali zote aliochuma yeye na mimi ....baadae nikasafiri nikaenda kuongeza shule kidogo huko italy huku yeye akisimamia miradi yangu na yake ujenzi wa nyumba yangu na mwaka jana tar 8 september tulifunga ndoa na ndoa yetu tulifungia italy na ni kati ya ndoa zilizofungwa na baba ntakatifu Benedict wa 16......sasa tupo katika nyumba niliyojenga mimi tunaishi, nyumba alizojenga yeye wakati yuko alone zimepangishwa zote na tunaishi salama na maisha yanakwenda vizuri sana....namshukuru Mungu mama blanca alinipa changamoto nyingi sana juu ya maisha ..

kikuwa nilichokuwa nawaza ni kwamba huyu anawezaje na kwa nini mimi nishindwe!!!? na hakika kwa kiasi nilicho nacho nakwa maisha tunayoishi namshukuru Mungu....

huyu kijana mwenzangu aliyekimbia hana changamoto..hataki kujifunza na mvivu wa kujishughulisha ndo wale wanaosubiri mishahara ya kila mwezi pasipo kujishughulisha.....unakimbia mwaanamke kisa ana kipato kukuzidi?!!!
Hongera sana mkuu,
Ww ni mwanaume na huyu ni mvulana ndio maana amekimbia!
Mungu awape maisha marefu na yenye furaha!
 
Mie nimemwambia aachane naye huyo jamaa ana tabia za kitoto,
Ila ndio hivyo hataki ushauri wa kuachana anataka ashuriwe namna ya kurudiana naye!

ningekuwa namfahamu huyo jamaa ningelimsaidia kimawazo sana ila basi tu ..canty msaidie mwenzio arudiane na mtu wake...
 
haha angalia mwisho wa siku utapewa kazi zaidi
Kazi gani,mie nimemwambia sina ushauri zaidi ya huo!
Ya nn tugombane, kilichobaki nampa moyo tu labda jamaa atabadili mawazo.
 
"we ndio mwanaume bana, mwanamke hawezi kukuzidi kipato". Hizi kauli zao wanazoambiana zitawaponza wengi. Nawahurumia sana wanaozichukua kama zilivo na kuzimeza nzima nzima, ndo hao sasa! Kuweni reasonable bana sio mnaishi tu kwa mazoea, things are changing sio kama zamani ambapo tulizuiliwa hata kumiliki ardhi!! Huyo dada atumie ndugu/rafiki yeyote wa huyo "mkaka muoga" kupata ramani yake na ratiba then amuibukie, sometimes unajisacrifice kwa ajili ya ukipendacho lol!!! Ila kama ni wewe cantie nambie nikusindikize........just a joke, lol.......hahahahahaaaa
 
kwa hiyo unaamini atafuata ushauri wako??? lakini unaweza kuwa mtu wa kati kumuunganisha kwa alisiye muoga

vipi jeny anaendeleaje???
 
"we ndio mwanaume bana, mwanamke hawezi kukuzidi kipato". Hizi kauli zao wanazoambiana zitawaponza wengi. Nawahurumia sana wanaozichukua kama zilivo na kuzimeza nzima nzima, ndo hao sasa! Kuweni reasonable bana sio mnaishi tu kwa mazoea, things are changing sio kama zamani ambapo tulizuiliwa hata kumiliki ardhi!! Huyo dada atumie ndugu/rafiki yeyote wa huyo "mkaka muoga" kupata ramani yake na ratiba then amuibukie, sometimes unajisacrifice kwa ajili ya ukipendacho lol!!! Ila kama ni wewe cantie nambie nikusindikize........just a joke, lol.......hahahahahaaaa

umekuja hatimaye lol
 
Back
Top Bottom