Habarini ndugu Zangu, mwaka juzi nilikuja kuomba msaada hapa jukwaani wa kukosa uwezo wa kishiriki tendo la ndoa. Watu mbali mbali walijitolea kunielekeza matibabu na kunitia moyo, Mungu awabariki sana.
Mrejesho ni kwamba nilipata ahueni mashine ikaanza kusimama ila kwa kubeep. To cut the story nimetembea sehemu mbali mbali kutafuta matibabu, ikiwemo hospital wakasema Nina upungufu wa hormone ya testosterone. Hivyo wakanipa vidonge vya kumeza (Proviron) kwa mwezi 1. Unfortunately sijapata nafuu.
Nimekuja hapa kuomba msaada tatizo langu la kutosimamisha na kukosa hamu ya tendo la ndoa bado linanisumbua.
Kuna wakati navunjika moyo kutafuta matibabu maana nimetumia gharama kubwa sana tangu kuanza kwa hili tatizo. Hapa chini ni vipimo ambavyo nilipima na kupewa majibu kwamba hormone ya testosterone ipo chini.
Nimetumia dawa zao za sh 90,000 + 60,000 bila nafuu. Sina hamu na tendo la ndoa. Naombeni msaada ndugu Zangu.
View attachment 3291315