Msaada usafiri kutoka Morogoro kwenda Butiama

Msaada usafiri kutoka Morogoro kwenda Butiama

Ili ufike mapema zaidi, epuka kupanda magari yanayopitia mwanza, yanachelewa zaidi.

In this case, magari ya Kampuni ya Kapricon ndo yanapita route hii na yanafika mapema zaidi kule. So wewe utakubali kulala Musoma ili kukicha ndo uende huko butiama kwa kutokea musoma, maana usiku huo ukiteremkia njiani, hutapata usafiri wa kwenda butiama.
Senseless!

Atafute magari yanayofika haraka halafu unamwambia atatakiwa kulala stendi mpaka asubuhi yake, sasa maharaka ya njiani ya nini? Jifunze logic!
 
Falcon , Happy Nation,Kapricon

Hizo Zinatoka Dar Es Salaam ~Musoma Moja Kwa Moja

Ukiwa Morogoro Zipo Abood, Nyahunge, Ally's Lakini Mwisho Mwanza
 
Yes, panda gari ya Moro ... Musoma, zinafika usiku sana na hali ya ugeni itakuwia ugumu kufika chuoni.

Ushauri
Nenda hadi Musoma mjini, pakikucha ulizia magari yanayoenda Buhemba(haya yanapita kwenye geti kabisa la Mwl Nyerere Un), au panda magari yanayoenda Butiama then shukia Butuguri then daka boda anakupeleka chuoni chap
Uliyeanzisha thread, jibu la swali lako liko hapa.

Thread closed.
 
Senseless!

Atafute magari yanayofika haraka halafu atatakiwa kulala stendi mpaka asubuhi yake, sasa maharaka ya njiani ya nini? Jifunze logic!
Hide your senselessness!

Umejuaje hana watu wa kumpokea? Na ningekuwa nakurupuka kama wewe unadhani ningemwambia hizo options za kufika mapema na kuchelewa?
 
Yes, panda gari ya Moro ... Musoma, zinafika usiku sana na hali ya ugeni itakuwia ugumu kufika chuoni.

Ushauri
Nenda hadi Musoma mjini, pakikucha ulizia magari yanayoenda Buhemba(haya yanapita kwenye geti kabisa la Mwl Nyerere Un), au panda magari yanayoenda Butiama then shukia Butuguri then daka boda anakupeleka chuoni chap
Asante sana mkuu, shukrani sana
 
Unakwenda kijiji cha Butiama kwa Nyerere yalipo makao makuu ya wilaya?

Kama ndio, uliza basi zuri linalokwenda Tarime utashuka Kyabakari, pale kuna tax na Bodaboda uamuzi ni wako utapelekwa Butiama.

Unapotokea Mwanza mabasi hayapiti Butiama hivyo ni lazima ushuke hapo Kyabakari ndio upande Bodaboda au tax nauli ya kawaida tu watakupeleka hapo Butiama.

Route ni Morogoro, Dodoma, Singida, Igunga, Nzega, Shinyanga, Mwanza to Musoma.
Siku hizi kuna magari yanatokea Mwanza kwenda Buhemba kupitia Butiama.
 
Kwahiyo sisi wa Busegwe Sasa hivi unashuka barazani tu?
Hazipiti Buswege. Zinakatiza bypass ya Kiabakari Butiama center kwenda Buhemba.

Kama huyo anaenda Chuoni maana yake ni Buswege, aidha ashuke Butiama center au Makutano apande gari ndogo.
 
WADAU NINGEPENDA NITOE SHUKRANI KWA WOTE MLIOJITOKEZA KUNIELEKEZA MAWAZO YENU WOTE YAKO HELPFUL KWANGU.

NASHUKURU SANA🙏
 
Hazipiti Buswege. Zinakatiza bypass ya Kiabakari Butiama center kwenda Buhemba.

Kama huyo anaenda Chuoni maana yake ni Buswege, aidha ashuke Butiama center au Makutano apande gari ndogo.
Huyo tayari ameshapata option hapa Sasa nijibu Mimi, kama unapitia Butiama utafikaje Buhemba bila kupitia Busegwe?

Yani dalada litoke Buguruni kwenda kariakoo si lazima lipite Ilala?
 
Kipo Butiama kama alivyoeleza.Anaweza kufika hapo Makutano na kupata usafiri unaopita katikati kuiacha njia ya Mwanza na kuelekea Butiama moja kwa moja.Au akaendelea kutoka Makutano na kuelekea hadi Nyamisisye.Halafu atafute usafiri kwenda moja kwa moja Butiama kupitia Nyankanga.Hapo vipi?
Na wewe ni product ya Mara land
 
Unaweza kunielekeza straight natokea MOROGORO napanda bus la kwenda wapi nashukia wapi na naelekea wapi Ili kufika hapo butiama, just short and clear boss wangu fanya hivyo asee.
Msome Synod ameeleza njia nyepesi.Asante.
 
Huyo tayari ameshapata option hapa Sasa nijibu Mimi, kama unapitia Butiama utafikaje Buhemba bila kupitia Busegwe?

Yani dalada litoke Buguruni kwenda kariakoo si lazima lipite Ilala?
Ukiwa unatokea wapi?

Kama unatokea Musoma Mjini unaweza kupita Busegwe pia.
 
Hivi wadau kwani inawezekana, ukakata ticket gari ya kutoka DAR kwenda MUSOMA, halafu ukaisubiria itoke Dar Ili uje kuipanda ikifika Morogoro ?

Maana wengine kusafiri comfortably inabidi upate seat namba mbili, tukipanda za mbali bhas ni full kizungu zungu na kutapika njiani. So hiyo huduma inasaidia kusecure seat unayoitaka. Vipi hiyo inawezekana wadau ?
 
Inawezekana, zungumza na wenye mabus.
 
Hide your senselessness!

Umejuaje hana watu wa kumpokea? Na ningekuwa nakurupuka kama wewe unadhani ningemwambia hizo options za kufika mapema na kuchelewa?

angekuwa na watu wa kumpokea wangeshamweleza wapi pa kumpokea na anafikaje hapo pa kumpokelea kutoka Morogoro. Use your noodles.

Eti atafute magari yanayokwenda fasta ili awahi kulala stendi! You need a frontal lobe transplant.
 
Back
Top Bottom