Sa 7 mchana
JF-Expert Member
- Dec 30, 2018
- 5,214
- 10,276
Let me cut the bullshit and hit the point.
Leo nimepokea simu kutoka nyumbani, Napewa taarifa kuwa mdogo wangu wakiume amepata matatizo anapoteza fahamu.
Tatizo limeanza siku chache zilizopita( yani ijumaa ya tarehe 04.02.2022). Kijana aliondoka asubuhi sana kwenda shule, mashuhuda wanasema aliwahi sana siku hiyo isivyokawaida yake maana Kijana aliondoka sa kumi na Moja (11) alfajiri.
Mdogo wangu njiani alikutana na wenzie wawili na kufanya msafara uwe wa wanafunzi wa tatu.
Watatu hao walijongea mpaka shuleni. Baada ya kukaa kwa muda kidogo, dogo aliwaacha wenzie kuelekea chooni. Ila uko chooni dogo alikaa sana mpaka wenzie wakashuku kuwa kunakitu hakipo sawa, ikabidi waenda kumuangalia. Kufika uko dogo wakamkuta amedondoka chini hajitambui na ni kama amenyooka hivi.
Hivyo wakafanya utaratibu wa kumpeleka hospitali ila huko hakubahatika kupata nafuu wala kugundulika anatatizo lolote la kiafya ilihali dogo alikua bado hajitambui na amegangamara.
Siku hiyo hiyo ya Ijumaa ikabidi dogo apelekwe kwenye maombi kanisani.
Maombi yalifanya kuanza sa tatu asubuhi mpaka sa kumi na mbili jioni dogo akazinduka.
Jumamosi ya jana dogo siku nzima aliitumia kanisani (sabato). Ila kimbembe leo tena Jumapili, naambiwa dogo ameamka sa 11 alfajiri anajiandaa kuelekea shule, shuhuda dada wa kazi. Kumuuona vile akaenda kumshitua faza hausi. Dogo alivyokua "busted" pale pale kazima tena.
Duh ikawa ni noma sana, maombi yalifanyika na nyimbo, dogo akawa sawa. Dogo akaulizwa anakumbuka nini alivyoviona ama kuviishi muda mchache iliyopita. Dogo anasema alikua malaloni wanaofanya mazishi, anaulizwa mazishi ya nani hasemi.
Muda wa chakula cha mchana umefika dogo anasema ameshiba, eti ameshakula, anaulizwa umekula nini anasema kala nyama masibani. Watu duh!!!!
SASA NIMEKUJA KWAKO WANA JAMII FORUM.
Nakukaribisha utoe mchango wako wa mawazo ilituweze kumuundolea adha hii mdogo wetu mana hali ni mbaya japo siku ni chache. Ila pale anapokua amepoteza fahamu pia haja zote mdogo na kubwa hutoka bila kujizuia.
Ulishawahi kusikia kesi kama hii?
Je, mtu aliekubwa na hali hii alitibiwaje?
Am open kupokea kila aina ya tiba utakayoipendekeza iwe hospitali, ya kiimani au asili.
MCHANGO WAKE NI MUHIMU SANA KWA MDOGO WETU