Ukisoma comments za members wengi hapa wamekusihi kuhusu kuzingatia lishe.
Inaonekana huli vizuri (mlo Kamili) ama umekuwa mvivu sana wa kula
Kwa kuwa upo mwishoni kuelekea kujifungua, almost wiki 3 ama 4 zijazo jitahidi kuboresha ratiba yako ya Kula bila kusahau muda mrefu wa Kulala.
Kwa Wazazi wajao, ni vyema mkajifunza kuwahi kufanya check up za mara Kwa mara ikiwemo kuangalia maendeleo ya mimba zenu Kwa wakati (Utra-sound)
Waambieni Waume/wapenzi wenu watenge fedha kwaajili ya kula yako hasa milo kamili kwaajili ya Afya Bora kwako kama Mama pamoja na mtoto aliye tumboni.
Sio vibaya kama Mume, kumtengea Mkeo/Mpenzi wako order maalumu ya Maini Kila Siku kwenye mlo wake (almost shilingi 200,000) Kwa Mwezi.
Maini ni muhimu sana Kwa Mama Mjamzito