Msaada wa haraka unahitajika kuhusu ujauzito wangu

Msaada wa haraka unahitajika kuhusu ujauzito wangu

Poleni na mihangaiko ya mchana kutwa

Ndugu Madaktari wa JF na wadau wote wa afya naomba msaada wenu.

Mimi ni mama mjamzito mimba yangu ina wiki 35.

Katika umri huu nimepima utra sound mtoto ana uzito wa kilo 2. 71kg

Swali langu kitu gani naweza kufanya kwa muda huu mchache uliobaki kuongeza uzito wa mtoto .

Maana Dr ananiambia kwa uzito huu ni hatarishi kwangu na mtoto pia

Naombeni ushauri wenu.

Ahsanteni
Utajifungua mtoto wa kiume nakuombea heri ujifungue salama
 
Mrejesho
Nimefanikiwa kujifungua salama kabisa ingawaje kwa operation nilikua (obstructed labour)
Mtoto ametoka na kilo 3.5Kg
Shukrani zangu za dhati kabisa kwa wote mlitumia muda wenu kunipa ushauri wa kitaalam na ushauri kutokana na experience
 
UNataka kuongeza Uzito wa mtoto kwenye Ujauzito wa wiki 35 Ambao ni 2.71 kg?

Uzito Normal kwa mtoto Wa week ya 35 Huwa ni 2.3kg mpaka 2.5 kg..

Nilifikiri Ungeanza kufanya jitihada za kupunguza Lishe unayokula ili usijifungue Big Baby??

Daktari aliyekushauri kwamba Kilo za mtoto Chache kwa umri wake maybe ali overlook..

Hizo kilo ziko sawa na zimepita Uzito wa Normal ya Mtoto..
So Kuwa na amani kabisa
Dr nashukuru nilifuata ushauri huu na Alhamdulillah nilipunguza baadhi ya protein na ndio katoka na 3.5kg

Ubarikiwe sana
 
Back
Top Bottom