Msaada wa kimawazo

Msaada wa kimawazo

Habari yako mwana jf

Baba yangu alibahatika kuwa na mali nyingi sana na kwetu tumezaliwa wachache watu wa nne tu,

Sasa mzee ili kuondoka utata ameamua kugawa mali ingali yupo hai Mimi nimepata mgao wa nyumba ya kuishi pamoja na kiasi kama million 50

Kwa upane wa elimu nina degree ya agribusiness kutokea SUA
Pia binafsi sina background yoyote ya kufanya biashara maana mda mwingi nimetumia shuleni

Niliwaza hii pesa niiweke UTT baada ya kuisoma na kuifatilia Sana lakini changamoto inakuja nahofia usalama wa pesa yangu huko UTT hasa hasa kwenye nchi yetu hii ambayo kiongozi anaweza amua chochote mda wowote.

Naombeni ushauri je naweza anzia wapi katika uwekezaji.
Na je UTT ni salama mathalani kwa miaka 30 ijayo. Umri wangu ni miaka 25.

Pia ningeomba Kwa wenye kujua zaidi ni mkoa gani au eneo gani Tanzania ni zuri Kwa mtu mwenye mtaji kuanza biashara na biashara ipi inaweza kuwa na rejesho zuri.
Asanteni


Chukua million 20 weka UTT hizo risk nyingine unazoziwaza zipo kila mahali, then kwenye million 30 inayobaki chukua million 20 fungua ofisi ya wastani ya printing and branding.

Nunua large format ndogo moja, heat place ya kuchoma logos kwa Tshirst na vikombe pamoja na plotter if necessary. Now kampeni zinakuja so mabango na matshirt ya chama or vyama yataprintiwa sana hasa yale yenye sura za watu kwahiyo ukifanya marketing vizuri na ukawa unaenda outdoor kutafuta tenda utapiga pesa, and trust me hii biashara unaweza kustruggle miezi sita ya mwanzo coz ya ugeni wa ofisi ila baada ya hapo hautabaki kama ulivyo.

Hiyo million 10 nyingine itie bank kama akiba yako na matumizi ya hapa na pale... kila la heri young man.
 
Bhana usifute namba yangu, napenda wasap status zako zilivyo za moto afu kile kigauni cha jana ๐Ÿ”ฅ
Khaah ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ™Œ๐Ÿพ๐Ÿ™Œ๐Ÿพ๐Ÿ™Œ๐Ÿพ hujawah kua na akili,,mimi na magauni wap na wapi
 
Back
Top Bottom