olika
Member
- Mar 30, 2020
- 25
- 60
Salaam wana jamvi,
Nahitaji msaada wa kisheria ama taratibu gani nifuate ili kuweza kupata haki ya kulea watoto wangu!
Story kwa ufupi iko hivi:
Mimi na mwanamke (34) nimeolewa ndoa ya kanisani, nimebahatika kupata watoto wawili (mkubwa miaka 4.7, mdogo miaka 2.5). Mimi na Mr tumekuwa kwenye migogoro isiyoisha kwa muda mrefu (ndoa ina miaka 6), na chanzo hasa ni mwenzangu hataki nifanye kazi, wala biashara yoyote, wala shughuli yoyote inayoniingizia kipato. Kwa muda wote huo nimekuwa mtulivu na kumsikiliza anachotaka ili tu amani iwepo, lakini haikuwezekana. Majukumu yake anatimiza kwa kusuasua, yaani ni mpaka awe na furaha ndipo atoe. Mkipishana kidogo anakususia kila kitu mpaka kutoa matumizi.
Kuna wakati ukimuomba fedha kwa ajili ya mahitaji ya nyumbani na watoto anakujibu vibaya, nanukuu: “Watoto sio wangu, watafutie baba yao” na “Sifanyi kazi kwa ajili ya matumbo yenu”. Hali hiyo na kauli hizo zimenifanya kuishi maisha ya kuogopa kumkwaza ili tu nipate mahitaji ya muhimu (chakula).
Ukimuomba mtaji wa biashara anadai nilee watoto bado wadogo.
Kutokana na changamoto hizo na maisha kuwa magumu, niliamua kutafuta kazi, maana nilifanikiwa kusomeshwa mpaka chuo kikuu, nina degree ya ………
Mwaka huu Mungu akajaalia nikapata kazi serikalini. Baada ya kumwambia nimepata kazi alichukia sana, ndipo akaamua kutorosha watoto. Sijui alipowapeleka na wala sijui wanaishi na nani. Ndugu zake hawanipi ushirikiano, wapo upande wa ndugu yao.
Mr amehama na nyumba na hapokei simu zangu kabisa. Ni miezi miwili imepita, lakini kuna maneno ya pembeni yalinifikia kwamba ili anipe watoto ni lazima niache kazi, vinginevyo sitawaona tena.
Hatua nilizofanikiwa kuchukua:
Naombeni msaada tafadhali, siwezi kukaa kwa amani bila kujua mahali walipo watoto.
Ahsanteni.

- Nilikwenda kutoa taarifa polisi kwenye dawati la jinsia.
- Nimejaribu kuongea na wakubwa zake ili angalau tukae kikao cha kusuluhisha kifamilia, lakini amekataa kuwekwa kikao mpaka siku nitakapokubali kuacha kazi.
- Nataka kujua process gani nifuate kisheria ili nipatiwe watoto wangu nilee mwenyewe, mpaka pale watakapofikia umri wa kuchukuliwa na baba yao.
- Je, mgogoro huu hautaleta athari kwenye kazi yangu? Vipi kama ataenda kuniharibia ofisini ili niachishwe kazi?
- Je, naweza kumueleza mkuu wangu wa kazi juu ya changamoto ninayopitia ili pia niweze kupata ruhusa wakati nitakapohitaji kufuatilia watoto?