Msaada wa kisheria kuwapata watoto baada ya kuhitilafiana na baba yao

Msaada wa kisheria kuwapata watoto baada ya kuhitilafiana na baba yao

wanaume tuna taranta ya saikolojia...

mumeo ameshajua ukipata kazi na pesa utamsumbua...

baadhi ya wanawake mna ulimbukeni mkipata hivyo vitu viwili...

nakushauri achana na huyo mwanaume...

japo hakikisha mnakaa kikao ili upate haki ya access kwa watoto wenu...
 
Si umesema wapo kwa baba yao?

Tafuta mume olewa zaa wengine huku unaendelea kufuatilia hao wengine.

Ukienda ustawi wa jamii watakusaidia
Si umesema wapo kwa baba yao?

Tafuta mume olewa zaa wengine huku unaendelea kufuatilia hao wengine.

Ukienda ustawi wa jamii watakusaidia
aisee kumbe bi rahisi kuolewa na kuzaa wengine.
 
Watoto bado wadogo mkuu, sikatai yeye kukaa nao maana ni baba yao lakini kwanini hanipi nafasi ya kuzungumza nao wala kuwaona wala kujua tu mahali wanapoishi?. Pili namfahamu vizuri lengo la kuchukua watoto ni ili kunikomoa nikose utulivu niharibu kazi, sina hakika kama ana mapenzi na hao watoto maana ni mara kibao amewakataa na kususia kuwahudumia
Fata utaratibu Kafungue kesi ya talaka mahakama ya mwanzo au wilaya na ueleze sababu za msingi za kudai talaka ni zipi, labda ukatili, kutelekezwa, uzinzi, kutokuelewana kwa muda mrefu au sababu zingine.

Baada ya hapo mahakama itajaribu usuluhishi kupitia baraza la usuluhishi, ikiwa suluhu haitapatikana mahakama itasikiliza ushahidi wa ulichoshtaki na baadae itatoa hati ya talaka.

Masuala la mgawanyo wa mali au nani atabaki kulea watoto mahakama itaamua pia.

Ila hapa umeeleza malalamiko yako ya upande mmoja na siku zote anaesema peke yake ni mshindi, ikiwa na yeye anayo malalamiko yake ya msingi unaweza kunyimwa hao watoto na mahakama pia akaachiwa yeye kwa manufaa mapana ya mtoto.
 
Mimi kuacha kazi ni haiwezekani kutokana na mazingira niliyoishi na pia mimi binafsi ninayo malengo yangu isitoshe nina wazazi wanaonitegemea.
Pole dada yangu, ila tatizo lilianzia hapa, uliingia kwenye ndoa tayari ukiwa na msimamo wako kichwani na yeye akiwa na msimamo wake.
Inawezekana ulikubali kuwa utakuwa mama wa nyumbani ili kumridhisha jamaa na hatimaye mfunge ndoa, matokeo yake mmeingia kwenye ndoa na wewe ukaamua kuonyesha msimamo wako mpya.
Cha msingi mjulishe muajiri wako hayo unayopitia, then rudi dawati la jinsia na ikiwezekana fungua kesi.
NB: Msiingie kwenye ndoa kutokana na shinikizo la kijamii au rika, ukijua una misimamo yako iweke wazi mapema ili mkiamua kuingia huko kwenye ndoa msikumbane na mambo mapya sana. BTW kataa Ndoa.
 
Salaam wana jamvi,
Nahitaji msaada wa kisheria ama taratibu gani nifuate ili kuweza kupata haki ya kulea watoto wangu!

Story kwa ufupi iko hivi:
Mimi na mwanamke (34) nimeolewa ndoa ya kanisani, nimebahatika kupata watoto wawili ( mkubwa miaka 4.7, mdogo miaka 2.5). Mimi na Mr tumekua kwenye migogoro isiyoisha kwa muda mrefu ( ndoa ina miaka 6), na chanzo hasa mwenzangu hataki nifanye kazi wala biashara yoyote wala shughuli yoyote inayoniingizia kipato, kwa muda wote huo nimekua mtulivu na kumsikiliza anachotaka ili tu amani iwepo lakini haikuwezekana. Majukumu yake anatimiza kwa kusuasua yaani ni mpaka awe na furaha ndipo atoe, mkipishana kidogo anakususia kila kitu mpaka kutoa matumizi.
Kuna wakati ukimuomba fedha kwa ajili ya mahitaji ya nyumbani na watoto anakujibu vibaya nanukuu “ watoto sio wangu watafutie baba yao” na “ sifanyi kazi kwa ajili ya matumbo yenu”. Hali hiyo na kauli hizo zimenifanya kuishi maisha ya kuogopa kumkwaza ili tu nipate mahitaji ya muhimu( chakula ).
Ukimuomba mtaji wa biashara anadai nilee watoto bado wadogo.
Kutokana na changamoto hizo na maisha kuwa magumu niliamua kutafuta kazi maana nilifanikiwa kusomeshwa mpaka chuo kikuu nina degree ya ………
Mwaka huu Mungu akajaalia nikapata kazi serikalini, baada ya kumwambia nimepata kazi alichukia sana ndio akaamua kutorosha watoto sijui alipowapeleka na wala sijui wanaishi na nani, ndugu zake hawanipi ushirikiano wapo upande wa ndugu yao.
Mr amehama na nyumba na hapokei simu zangu kabisa ni miezi miwili imepita lakini kuna maneno ya pembeni yalinifikia kwamba ili anipe watoto ni lazima niache kazi vinginevyo sitawaona tena.
Hatua nilizofanikiwa kuchukua:
1. nilikwenda kutoa taarifa polisi kwenye dawati la jinsia.
2. Nimejaribu kuongea na wakubwa zake ili angalau tukae kikao cha kusuluhisha kifamilia lakini amekataa kuwekwa kikao mpaka siku nitakapokubali kuacha kazi.

Msaada ninaohitaji:
Nataka kujua process gani nifwate kisheria ili tu nipatiwe watoto wangu nilee mwenyewe mpaka pale watakapo fikia umri wa kuchukuliwa na baba yao.

Je, mgogoro huu hautaleta athari kwenye kazi yangu? Vipi kama ataenda kuniharibia ofisini ili niachishwe kazi?

Je naweza kumueleza mkuu wangu wa kazi juu ya changamoto ninayopitia ili pia niweze kupata ruhusa wakati nitakapohitaji kufuatilia watoto?

Mimi kuacha kazi ni haiwezekani kutokana na mazingira niliyoishi na pia mimi binafsi ninayo malengo yangu isitoshe nina wazazi wanaonitegemea.
Naombeni msaada tafadhali siwezi kukaa kwa amani bila kujua mahali walipo watoto
Ahsanteni
Rudi nyumbani ulee familia!
 
Je naweza kumueleza mkuu wangu wa kazi juu ya changamoto ninayopitia ili pia niweze kupata ruhusa wakati nitakapohitaji kufuatilia watoto?
- Maisha yako binafsi na changomoto unazopitia hupaswi kuzipeleka sehemu yakazi.
Je nini cha kufanya:
  • Fuata miongozo na taratibu za kupata ruhusu, zipo.
  • Andika barua ya kuomba ruhus (itakapo fika wakati), Ainisha muda wa ruhusa, kwenye sababu waweza andika "Matatizo ya kifamilia".
  • Wakuu wako watapokea barua,wataipitisha na utapewa release.
anakujibu vibaya nanukuu “ watoto sio wangu watafutie baba yao”
  • Tuseme ukweli: Hii kauli haiji kwa bahati mbaya, Kuna kila dalili ameona wazi kuwa watoto huenda si wake, kilichobakia yeye ni kuthibitisha kupitia DNA
  • Nadhani hapa kuna red flag kadhaa aliona toka kwako. sio bure, Narudia tena hii kauli huwa haiji kwa bahati Mbaya.
 
Hivi mwanamke akiwa anajitafutia hata vi buku buku huwa ni jambo linalomkera sana mwanaume? Wanaume huwa wanainjoi kuona mtu unakua omba omba kwake mara akunyime....inaleta good feelings bila shaka 🤔

Pole kwa changamoto.
Shida nyie viumbe hamjawahi kujua kudhibiti kiburi mpatapo kauwezo kidogo, tumesikia story ya upande mmoja tu, tungepata na ya upande wa pili we could judge better
 
Hivi mwanamke akiwa anajitafutia hata vi buku buku huwa ni jambo linalomkera sana mwanaume? Wanaume huwa wanainjoi kuona mtu unakua omba omba kwake mara akunyime....inaleta good feelings bila shaka 🤔

Pole kwa changamoto.
Shida nyie viumbe hamjawahi kujua kudhibiti kiburi mpatapo kauwezo kidogo, tumesikia story ya upande mmoja tu, tungepata na ya upande wa pili we could judge better
Pole dada yangu, ila tatizo lilianzia hapa, uliingia kwenye ndoa tayari ukiwa na msimamo wako kichwani na yeye akiwa na msimamo wake.
Inawezekana ulikubali kuwa utakuwa mama wa nyumbani ili kumridhisha jamaa na hatimaye mfunge ndoa, matokeo yake mmeingia kwenye ndoa na wewe ukaamua kuonyesha msimamo wako mpya.
Cha msingi mjulishe muajiri wako hayo unayopitia, then rudi dawati la jinsia na ikiwezekana fungua kesi.
NB: Msiingie kwenye ndoa kutokana na shinikizo la kijamii au rika, ukijua una misimamo yako iweke wazi mapema ili mkiamua kuingia huko kwenye ndoa msikumbane na mambo mapya sana. BTW kataa Ndoa.
Comment moja matata sana
 
Salaam wana jamvi,

Nahitaji msaada wa kisheria ama taratibu gani nifuate ili kuweza kupata haki ya kulea watoto wangu!

Story kwa ufupi iko hivi:

Mimi na mwanamke (34) nimeolewa ndoa ya kanisani, nimebahatika kupata watoto wawili (mkubwa miaka 4.7, mdogo miaka 2.5). Mimi na Mr tumekuwa kwenye migogoro isiyoisha kwa muda mrefu (ndoa ina miaka 6), na chanzo hasa ni mwenzangu hataki nifanye kazi, wala biashara yoyote, wala shughuli yoyote inayoniingizia kipato. Kwa muda wote huo nimekuwa mtulivu na kumsikiliza anachotaka ili tu amani iwepo, lakini haikuwezekana. Majukumu yake anatimiza kwa kusuasua, yaani ni mpaka awe na furaha ndipo atoe. Mkipishana kidogo anakususia kila kitu mpaka kutoa matumizi.

Kuna wakati ukimuomba fedha kwa ajili ya mahitaji ya nyumbani na watoto anakujibu vibaya, nanukuu: “Watoto sio wangu, watafutie baba yao” na “Sifanyi kazi kwa ajili ya matumbo yenu”. Hali hiyo na kauli hizo zimenifanya kuishi maisha ya kuogopa kumkwaza ili tu nipate mahitaji ya muhimu (chakula).

Ukimuomba mtaji wa biashara anadai nilee watoto bado wadogo.

Kutokana na changamoto hizo na maisha kuwa magumu, niliamua kutafuta kazi, maana nilifanikiwa kusomeshwa mpaka chuo kikuu, nina degree ya ………

Mwaka huu Mungu akajaalia nikapata kazi serikalini. Baada ya kumwambia nimepata kazi alichukia sana, ndipo akaamua kutorosha watoto. Sijui alipowapeleka na wala sijui wanaishi na nani. Ndugu zake hawanipi ushirikiano, wapo upande wa ndugu yao.

Mr amehama na nyumba na hapokei simu zangu kabisa. Ni miezi miwili imepita, lakini kuna maneno ya pembeni yalinifikia kwamba ili anipe watoto ni lazima niache kazi, vinginevyo sitawaona tena.

Hatua nilizofanikiwa kuchukua:
  1. Nilikwenda kutoa taarifa polisi kwenye dawati la jinsia.
  2. Nimejaribu kuongea na wakubwa zake ili angalau tukae kikao cha kusuluhisha kifamilia, lakini amekataa kuwekwa kikao mpaka siku nitakapokubali kuacha kazi.
Msaada ninaohitaji:
  • Nataka kujua process gani nifuate kisheria ili nipatiwe watoto wangu nilee mwenyewe, mpaka pale watakapofikia umri wa kuchukuliwa na baba yao.
  • Je, mgogoro huu hautaleta athari kwenye kazi yangu? Vipi kama ataenda kuniharibia ofisini ili niachishwe kazi?
  • Je, naweza kumueleza mkuu wangu wa kazi juu ya changamoto ninayopitia ili pia niweze kupata ruhusa wakati nitakapohitaji kufuatilia watoto?
Mimi kuacha kazi haiwezekani kutokana na mazingira niliyoishi, na pia mimi binafsi ninayo malengo yangu. Isitoshe nina wazazi wanaonitegemea.

Naombeni msaada tafadhali, siwezi kukaa kwa amani bila kujua mahali walipo watoto.

Ahsanteni.
Kwanza mshirikishe boss wako kisha nenda ustawi wa jamii.Otherwise mtafute advocate akusaidie.Usiache kazi
 
Fata utaratibu Kafungue kesi ya talaka mahakama ya mwanzo au wilaya na ueleze sababu za msingi za kudai talaka ni zipi, labda ukatili, kutelekezwa, uzinzi, kutokuelewana kwa muda mrefu au sababu zingine.

Baada ya hapo mahakama itajaribu usuluhishi kupitia baraza la usuluhishi, ikiwa suluhu haitapatikana mahakama itasikiliza ushahidi wa ulichoshtaki na baadae itatoa hati ya talaka.

Masuala la mgawanyo wa mali au nani atabaki kulea watoto mahakama itaamua pia.

Ila hapa umeeleza malalamiko yako ya upande mmoja na siku zote anaesema peke yake ni mshindi, ikiwa na yeye anayo malalamiko yake ya msingi unaweza kunyimwa hao watoto na mahakama pia akaachiwa yeye kwa manufaa mapana ya mtoto.
Yeye hajagusia mambo ya talqka.Kaongelea watoto ndo shida yake
 
Hivi mwanamke akiwa anajitafutia hata vi buku buku huwa ni jambo linalomkera sana mwanaume? Wanaume huwa wanainjoi kuona mtu unakua omba omba kwake mara akunyime....inaleta good feelings bila shaka 🤔

Pole kwa changamoto.
Halimkeri alichoniangusha mwanaume mwenzangu ni hataki mkewe afanye kazi huku kutoa matumizi na kumpendezesha mkewe hataki.

Kama hutaki mkeo aajiriwe na ana passion ya biashara mpe mtaji afanye biashara huyu jamaa ni mpumbavu sana
 

Kama inawezekana kama usiache Mwanaume akulelee watoto, wataenda kuteseka huko, hasa wa kike. Ni wanaume wachache wanaweza kusimamia maslahi ya watoto wao wakiwa na wanawake wengine au wenyewe.
 
Back
Top Bottom