Msaada wa kisheria kuwapata watoto baada ya kuhitilafiana na baba yao

olika

Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
25
Reaction score
60
Salaam wana jamvi,

Nahitaji msaada wa kisheria ama taratibu gani nifuate ili kuweza kupata haki ya kulea watoto wangu!

Story kwa ufupi iko hivi:

Mimi na mwanamke (34) nimeolewa ndoa ya kanisani, nimebahatika kupata watoto wawili (mkubwa miaka 4.7, mdogo miaka 2.5). Mimi na Mr tumekuwa kwenye migogoro isiyoisha kwa muda mrefu (ndoa ina miaka 6), na chanzo hasa ni mwenzangu hataki nifanye kazi, wala biashara yoyote, wala shughuli yoyote inayoniingizia kipato. Kwa muda wote huo nimekuwa mtulivu na kumsikiliza anachotaka ili tu amani iwepo, lakini haikuwezekana. Majukumu yake anatimiza kwa kusuasua, yaani ni mpaka awe na furaha ndipo atoe. Mkipishana kidogo anakususia kila kitu mpaka kutoa matumizi.

Kuna wakati ukimuomba fedha kwa ajili ya mahitaji ya nyumbani na watoto anakujibu vibaya, nanukuu: “Watoto sio wangu, watafutie baba yao” na “Sifanyi kazi kwa ajili ya matumbo yenu”. Hali hiyo na kauli hizo zimenifanya kuishi maisha ya kuogopa kumkwaza ili tu nipate mahitaji ya muhimu (chakula).

Ukimuomba mtaji wa biashara anadai nilee watoto bado wadogo.

Kutokana na changamoto hizo na maisha kuwa magumu, niliamua kutafuta kazi, maana nilifanikiwa kusomeshwa mpaka chuo kikuu, nina degree ya ………

Mwaka huu Mungu akajaalia nikapata kazi serikalini. Baada ya kumwambia nimepata kazi alichukia sana, ndipo akaamua kutorosha watoto. Sijui alipowapeleka na wala sijui wanaishi na nani. Ndugu zake hawanipi ushirikiano, wapo upande wa ndugu yao.

Mr amehama na nyumba na hapokei simu zangu kabisa. Ni miezi miwili imepita, lakini kuna maneno ya pembeni yalinifikia kwamba ili anipe watoto ni lazima niache kazi, vinginevyo sitawaona tena.

Hatua nilizofanikiwa kuchukua:
  1. Nilikwenda kutoa taarifa polisi kwenye dawati la jinsia.
  2. Nimejaribu kuongea na wakubwa zake ili angalau tukae kikao cha kusuluhisha kifamilia, lakini amekataa kuwekwa kikao mpaka siku nitakapokubali kuacha kazi.
Msaada ninaohitaji:
  • Nataka kujua process gani nifuate kisheria ili nipatiwe watoto wangu nilee mwenyewe, mpaka pale watakapofikia umri wa kuchukuliwa na baba yao.
  • Je, mgogoro huu hautaleta athari kwenye kazi yangu? Vipi kama ataenda kuniharibia ofisini ili niachishwe kazi?
  • Je, naweza kumueleza mkuu wangu wa kazi juu ya changamoto ninayopitia ili pia niweze kupata ruhusa wakati nitakapohitaji kufuatilia watoto?
Mimi kuacha kazi haiwezekani kutokana na mazingira niliyoishi, na pia mimi binafsi ninayo malengo yangu. Isitoshe nina wazazi wanaonitegemea.

Naombeni msaada tafadhali, siwezi kukaa kwa amani bila kujua mahali walipo watoto.

Ahsanteni.
 
Hivi mwanamke akiwa anajitafutia hata vi buku buku huwa ni jambo linalomkera sana mwanaume? Wanaume huwa wanainjoi kuona mtu unakua omba omba kwake mara akunyime....inaleta good feelings bila shaka 🤔

Pole kwa changamoto.
 
Kama vile unavyopenda watoto wakae kwako na yeye pia anapenda watoto wakae kwake, kama vile unavyohofia watoto labda watanyanyaswa na Mama wa kambo na yeye anahofia hivyohivyo kuwa watanyanyaswa na Baba wa kambo.

Kwanini unafikiri una haki zaidi ya kukaa na watoto kuliko yeye?
 
Ni jambo rahisi nenda ustawinwa jamii utaongozwa hatua kwa hatua
 
Watoto bado wadogo mkuu, sikatai yeye kukaa nao maana ni baba yao lakini kwanini hanipi nafasi ya kuzungumza nao wala kuwaona wala kujua tu mahali wanapoishi?. Pili namfahamu vizuri lengo la kuchukua watoto ni ili kunikomoa nikose utulivu niharibu kazi, sina hakika kama ana mapenzi na hao watoto maana ni mara kibao amewakataa na kususia kuwahudumia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…