Msaada wa kupata Pasi ya kusafiria

Msaada wa kupata Pasi ya kusafiria

Usitoe kitu wewe ni Mtanzania passport yako utapata sasa hivi unajaza Online harafu unapeleka viambatanisho vyako uhamiaji baada ya kulipia huko 30,000 kwa Control Number kiasi kingine utalipia baada ya ofisa uhamiaji kuzipitisha mimi sijawahi kufikiri kutoa Rushwa kwa mkwaju wa Nchi yangu na mkwaju napata tuu hapa nina fomu za watoto ntazipeleka wiki ijayo...
Ok mkuu Ahsante kwa muongozo. Sasa ningependa nijibiwe hayo maswali hapo.
Je ni lazima niandike Barua na kupeleka barua ya utambulisho wa Serikali za mtaa??
 
Ili kupata passport,unatakiwa uwe na.
1.cheti cha kuzaliwa.
2.cheti cha kuzaliwa cha mzazi mojawapo.
3.Kitambulisho cha Taifa.
4.kitambulisho cha Kazi Kwa watumishi wa umma.au barua ya utambulisho KUTOKA serekali za mitaa Kama hujaajiriwa.
5.barua ya maombi ya passport kama uko mkoani anapitisha kwa kamishna WA mkoa kwenda Kwa kamishna mkuu,anwani zao za posta unaweza kuzipata ofisini kwao.
6.uthibitisho wa safari ukionyesha nchi unauokwenda.
7.baada ya kuwa na vielelezo vyote utaanza kujaza form ya maombi online kupitia uhamiaji portal.kuna sehemu uta upload barua ya utambulisho na Cheti cha kuzaliwa.
Kama ombi limekamilika utapewa contral namba ya kulipia 20,000 ili uweze Ku print form.
Ukishaprint form utatafuta mashaidi waijaze na pia mwanasheria.
8.baada ya hapo utaenda ofisi za uhamiaji ukiwa na hiyo form na vielelezo nilivyotaja hapo juu,
9.Ombi litapitiwa kama hakuna dosari,litapitishwa,utalipia 130,000 Kwa kutumia control namba,alafu utakamilisha ombi Kwa kupiga picha pamoja na kuchukuliwa alama za vidole.
10.Baada ya hapo utasubiri Kwa mwezi mmoja passport kuwa tayari.
11.kama unaihitaji Kwa haraka na hauna baadhi ya vielelezo unaweza watumia vishoka,Ila utawalipa gharama za ziada.almost 100-200k.
 
Wakuu naombeni mwongozo wenu tafadhali, nilikua nafatilia pasi ya kusafiria (International Passport) kidogo nimekumbsna na vikwazo. Mimi niko mkoani huku (Chuganian)

Nimejaribu kuulizia uhamiaji wa hapa nimeelezwa niwe na..
  1. Cheti cha kuzaliwa (Ninacho)
  2. Namba za Nida (ninazo)
  3. Cheti cha kuzaliwa mzazi (Ninacho cha baba)
  4. Barua ya Serikali ya mtaa
  5. Barua mimi ya maombi ya Passport kwenda kwa afisa uhamiaji mkoa
Wamesema pia Nikishakamilisha vitu vitatumwa Dar ambapo itachukua kama mwezi hivi hadi kupata passport sasa naomba kuuliza kwq mliofuatilia passport kipindi cha hivi karibuni.
[emoji117]Barua ya Serikali za mtaa na baraua yangu ya kuomba passport ni Muhimu au ni huku tu wa mkoani ndio tunaambiwa hivo????
Kama ni lazima niandike barua ya kuomba he inakua katika lugha gani??? Na mfumo wa uandishi wake upoje????

Kwenye site ya uhamiaji wanasema uwe na ushahidi wa safari au ushahidi wa Shughuli anayofanya mwombaji. Je ushahidi huo ni upi?? Na unapatikanaje???

Kama kuna waliowahi kupata passport kutokea huku mkoani nilipo basi naombeni uzoefu wenu tafadhali.

Nawasilisha
Sasa hivi maombi ya passport unajaza online, ukishakamilisha kujaza, utapata control number then unalipia elfu 20, then utapakua form yako unaipeleka uhamiaji na document ulizozitaja hapo juu. Nakushauri leta dar, in two weeks unapata passport yako
 
Sina mwenyeji dar.. naomba uwe host wangu tafadhali.
Lakini je Barua ya mwaliko ni lazima kua nayo maana siendi kutembea tu kwa siku kadhaa
 
Ili kupata passport,unatakiwa uwe na.
1.cheti cha kuzaliwa.
2.cheti cha kuzaliwa cha mzazi mojawapo.
3.Kitambulisho cha Taifa.
4.kitambulisho cha Kazi Kwa watumishi wa umma.au barua ya utambulisho KUTOKA serekali za mitaa Kama hujaajiriwa.
5.barua ya maombi ya passport kama uko mkoani anapitisha kwa kamishna WA mkoa kwenda Kwa kamishna mkuu,anwani zao za posta unaweza kuzipata ofisini kwao.
6.uthibitisho wa safari ukionyesha nchi unauokwenda.
7.baada ya kuwa na vielelezo vyote utaanza kujaza form ya maombi online kupitia uhamiaji portal.kuna sehemu uta upload barua ya utambulisho na Cheti cha kuzaliwa.
Kama ombi limekamilika utapewa contral namba ya kulipia 20,000 ili uweze Ku print form.
Ukishaprint form utatafuta mashaidi waijaze na pia mwanasheria.
8.baada ya hapo utaenda ofisi za uhamiaji ukiwa na hiyo form na vielelezo nilivyotaja hapo juu,
9.Ombi litapitiwa kama hakuna dosari,litapitishwa,utalipia 130,000 Kwa kutumia control namba,alafu utakamilisha ombi Kwa kupiga picha pamoja na kuchukuliwa alama za vidole.
10.Baada ya hapo utasubiri Kwa mwezi mmoja passport kuwa tayari.
11.kama unaihitaji Kwa haraka na hauna baadhi ya vielelezo unaweza watumia vishoka,Ila utawalipa gharama za ziada.almost 100-200k.
Ahsante sana mkuu. Naomba kuuliza hizo process ni kwa watu waliopo mkoani tu?? Je nikienda dar hivyo vitu vyote vinatakiwa pia au ni mkoani pekee
 
Process ndo hizo hizo,tofauti ta DAR na mikoani ni kwamba Kwa DAR unaweza pata passport Ndani ya siku 2,tofauti na mkoani,sababu passport zote zinatengenezwa dar
 
Je ukiwa dar unatakiwa hizo barua utume kwa anuani au unazipeleka wewe mwenyewe pale makao makuu.
Je itahitajika pia kuandika barua ya mkono kwamba unaomba passport???
 
Je itahitajika pia kuandika barua ya mkono kwamba unaomba passport??

Je ukiwa dar unatakiwa hizo barua utume kwa anuani au unazipeleka wewe mwenyewe pale makao makuu.
Je itahitajika pia kuandika barua ya mkono kwamba unaomba passport???
Kwa DAR uko ofisi ya kamishna Kwa hiyo ni Moja Kwa Moja,barua ya maombi unaandika kivyovyote,Ila kama unataka shortcut,ukienda ofisi za uhamiaji,kurasini DAR,apo nje ya ofisi wapo watu maalum Kwa hizo Kazi,wewe na uwezo wako WA kubargain.
 
Ahsante sana Mkuu maelezo yako yamenifungua vya kutosha
 
Inatakiwa sahiv watu waache mambo ya kizaman maana namba ya nida ina taarifa sahihi za kila mtu had sehem aliyo zaliwa, hii biashara ya kutumana vyeti vya kuzaliwa hadi vya majirani mi naona si sawa nida inatosha kabsa, labda kama ni mkakati wanatafuta tu sehem yenye udhaifu ukiwa huna chet Cha mzazi waaze kukuvuta hela
 
Ok mkuu Ahsante kwa muongozo. Sasa ningependa nijibiwe hayo maswali hapo.
Je ni lazima niandike Barua na kupeleka barua ya utambulisho wa Serikali za mtaa??
Mkuu sasa hivi tunajaza kwenye mtandao jaza huko uki print ndio unapeleka hivyo vitu Uhamiaji kwani wana maswali ukishajaza na kulipia ni kusubiri passport yako hata wiki au wiki mbili mtu anakwambia nimetoa leo leo kwa laki tatu na safari sio ya leo maana yake nini sasa...
 
Sasa hivi maombi ya passport unajaza online, ukishakamilisha kujaza, utapata control number then unalipia elfu 20, then utapakua form yako unaipeleka uhamiaji na document ulizozitaja hapo juu. Nakushauri leta dar, in two weeks unapata passport yako
Hata mikoani zinatoka haraka tuu Mkuu mbona mnatishana wakati uhamiaji wapo mikoa yote na hiyo ndio kazi yao kila kukicha...
 
Back
Top Bottom