Msaada wa mawazo: COVID19 inanirejesha nyumbani, baba naye hanitaki

Msaada wa mawazo: COVID19 inanirejesha nyumbani, baba naye hanitaki

kikoozi,
Suala la kumdai mzazi wako mpaka mkafikishana kwa mwenyekiti ni kumdhalilisha sana. Umeonekana huna nidhamu hata kidogo. Anachofanya baba yako yupo sahihi kwa umri huo ulionao hata uende kwa JPM, ataishia kukusweka ndani. Unawaza urithi muda huu, wewe unaweza ukawa muuaji...
 
kikoozi,
Mkuu kama jina lako lilivyo, kweli wewe ni kikohozi, mzee wako kaamua kukutafunia limao na tangawizi ili ujiongeze, wewe sio mtoto wa kukaa kwa wazazi, toka kajenge familia yako, tumia elimu yako hiyo kwani inaonekana hiyo degree haijakukomboa kifikra.
 
Mzee wako yupo sahihi kabisa. Akupige ni viboko. Kwanza unashabikia je CCM wakati huna hata ajira ya uhakika, pili miaka 37 unalilia kwenda kwenu. Mwanzako hapa miaka 23 nilikuwa siishi tena nyumbani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahah daah nimecheka sana
Mimi nadhani ungeripoti hili suala kwa hawa wana CCM "wenzio" mnaweza kuelewana! Ila nimecheka sana mkuu
Bia yetu
YEHODAYA
 
Pole sana mkuu ongea na huyu mwenzako.

 
kikoozi,
1. Umemkosea sana baba yako kwa kuingia naye kwenye ushabiki wa vyama. kumbuka wanaokichukia hicho chama kuna kidonda amepata nacho.

2. Miaka 37 bado unajiita mtoto na unataka kukaa kwa mzee wako. pole sana.

3. Ulipohama tu kwa mzee ulitakiwa urudi fasta uombe msamaha na siyo kusubiri matatizo ndo urudi.

4. Tafuta ndugu wa mzee waongee naye kuhusu kusamehewa. kiserikali unapaswa kuwa hata na wajukuu, hupaswi kukaa kwa mzee
 
kikoozi, Mzee wako hakukosea kuwaambia watu kwamba "hauna akili timamu" Period , mzee wako ukishamshitaki na akakulipa pesa yako yote, umri wako huo wa 37 ni aibu kuendelea kung'ang'ania tena kwa mzazi na hivi tena humuheshimu... Hatua za mzee kukupiga pini kwenda kwake ni nzuri, wewe nenda katafute kwako
 
Back
Top Bottom