Msaada wa mawazo: COVID19 inanirejesha nyumbani, baba naye hanitaki

Msaada wa mawazo: COVID19 inanirejesha nyumbani, baba naye hanitaki

kikoozi,
Habari za uzima ndugu zangu, poleni sana na miangaiko ya hapa na pale, Mimi ni kijana mwenye miaka 37 kwa sasa elimu yangu ni degree miaka 37 unajiita kijana. Hiyo degree bro haijakusaidia kitu
 
Hasara ni hizo pesa na muda uliopoteza kusotea hiyo unayoita degree, ingekuwa kwa Ras Simba ungerudishiwa tu.

Kuhusu nyumbani, hapo ni kwa baba yako, komaa hapo hapo tena kuume kwa baba.
 
dah dunia inamambo ..kijana wa miaka 37 unalalamika baba amekufukuza ..yani hata aibu hauoni...

nenda kapambane na wewe ujenge nyumba yako acha kulia lia...
Hii ndio Africa bado tunasafari ndefu miaka 37 anapambana kukaa home, hajui kama hayupo kwenye group la watoto na amesoma hadi bachelor degree
 
Dingii hataki kumpokea mwanampotevu badala amchinjie hata jogoo kweli jamaa haupendwi
 
Sio kama nafurahia lakini ulikosa sana hekima kumdai mzee wako hiyo laki saba,na yeye angesema umlipe pesa zake wakati anakusomesha ungelipa

Alafu unawaza kuhusu mirathi,na hapo mzee lazima tu akuondoe kwenye mipango yake kwa sababu kashaona kabisa kuwa wewe kijana huna adabu
 
Kuhusu nidhamu tuliweke hilo pembeni kwanza, ulikosea sana kununua godoro na kupanga chumba cha umeme wakati tayari laki saba ilikuwa kama mtaji tosha wa kukutoa, miezi sita tu ingetosha kurudisha heshima.

Cc. Daktari wa Meno
 
Kadiri ulivyokiri kwenye post #4, hao viongozi wa kata wapo sahihi 100%.
Katika kukuelimisha tu:

1. Haki za mtoto zinakoma akifikisha miaka 18; vinginevyo awe mwanafunzi au MENTAL RETARDED.

2. Kuhusu kurithi au kunufaika na mali za wazazi; nzazi/wazazi ndio wenye maamuzi. Wakiamua kuandika mirathi kuwa wapewe yatima. It's OK!

3. Kama unakwenda ngazi za juu, andaa kabisa cheti kinachoonyesha hali yako ya akili: kuwa DISHI LAKO LIMEYUMBA.

4. Furahi kwa kuwa una baba mwenye akili sana. Anastahili kuwa mwenyekiti wa huo mtaa.
 
Ulisomea degree yako VETA ya mkoa gani? Labda tatizo lote linaanzia hapo
 
Wakati unaandika huu uzi labda umelewa yaani miaka 37 una kaa kwa baba na degee unayo.
Sawa unakaa kwa baba af unadai laki saba nakusepa
Nina chakukushauri ila sina muda.
 
Sometimes kwa sisi wazazi unaweza kujuta kuwa na Mitoto isiyo na akili, ni bora kupata NYANYA utaikatia kachumbali kuliko kuwa na Mtoto asiye na akili.
 
Baada ya siku 6 baba alinipatia pesa yangu yote laki 7, siku iyo iyo nikaondoka nyumbani na kwenda kupanga chumba cha umeme pamoja na kununua godoro niakaanza maisha ya kubangaiza tangu mwaka jana,

Nyie ndio mnafanya sisiemu iendelee kutawala nchi,

Ukapagawa na chumba cha umeme,, ukifikiria laki saba inaweza kutenga undugu wako na mzee wako
 
Back
Top Bottom