Msaada wa mawazo: COVID19 inanirejesha nyumbani, baba naye hanitaki

Msaada wa mawazo: COVID19 inanirejesha nyumbani, baba naye hanitaki

😂😂nilihisi mimi tu ndo naona huu uzi kama mzaa!

Uwezo wa kupangilia matukio na uandishi unaonesha wazi mleta mada yuko timamu na hana shida na mzazi wake na sio mwanachama wa ccm, zaidi ni mwanachama cha CDM.
eti zaidi atakuwa CDM
😂😂😂😂
 
Unawaza mirathi wakati mwenye Mali yupo hai. Nadhani kata hawakukosea observation yao. Ukianza kufa wewe?

Wewe si ulishaondoka mkakubaliana na sharti la mzee akupe laki 7 yako Kisha upotee mazima na ukapokea ukajiona kidume ukaondoka vipi Tena?

Acha kujilazimisha kuwa wewe ni mtoto, wewe ni kubwa zima unatakiwa uwe na kwako na familia yako. Hiyo nyumba na hizo mali Ni za baba yako na hukumsaidia hata thumni kununua huna haki yoyote. Anaweza akaamua kuandika wosia hata akifa Mali zake wapewe mbwa wa barabarani usipate hata kijiko cha chai na usifanye kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila uyu jamaa anaeza akawa anajaribu kupima jf ni wangap wanaish kwa kujtgmea pia anatak kupima y watu wanasaport lockdown hum je wanaish kwa kujtgmea?
 
Imenichukua Muda mrefu sana kuelewa ni kwanini huwa wengi JamiiForums wanaamua kujibu comments za ajabu. Ila kwa sasa nimesha anza kuelewa!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
KWa akili hizi za wanaccm mzee anahaki yakuwa dictator maana ukisikili ushauri wa akili hizi unauza nchi!
 
kikoozi,
Suala la kumdai mzazi wako mpaka mkafikishana kwa mwenyekiti ni kumdhalilisha sana. Umeonekana huna nidhamu hata kidogo. Anachofanya baba yako yupo sahihi kwa umri huo ulionao hata uende kwa JPM, ataishia kukusweka ndani. Unawaza urithi muda huu, wewe unaweza ukawa muuaji...
Huyu inaelekea angepata Mali angemnyanyasa sana Baba yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huwezi amini nimeandika comments na kufuta zaidi ya mara 20 kisha mwisho kabisa nikajiuliza.
ikiwa mimi ambae nilioteza wazazi ote nikiwa na 16 years tu na urihi ulibakia ni kitanda na kijakabati cha mlango mmoja,nimefikaje hapa nilipo at 27 years bila ya msaada wa wazazi wala support,nikiwazaga hivi huwa nainua mikono juu na kusema alhadulilah rabil alamin.

Sijui unayoyapitia but kwa umri wako wew siyo wa kuyandika haya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za uzima ndugu zangu, poleni sana na miangaiko ya hapa na pale, Mimi ni kijana mwenye miaka 37 kwa sasa elimu yangu ni degree, kama mnakumbuka nilishawai kuja na uzi wa baba yangu mzazi wa kunizaa kunitimua nyumbani kisa eti mimi ni mwanachama wa chama cha mapinduzi kisa cha kunifukuza ni kumshawishi yeye nae ajiunge kwenye chama cha mapinduzi (CCM)

Baada ya kunitaka niondoke kwake nilimuomba anirudishie pesa yangu niliokuwa nimemuazima kipindi nasoma chuo shilingi laki 7, aligoma kunipa mwanzoni ila baadae nilienda kwa mwenyekiti wa serikali za mtaa ili kuendelea kupigania haki yangu

Baba aliitwa serikali za mtaa, na alikubali kutoa pesa yangu kwa sharti moja tu, kama atanipa pesa yangu nisije kuonekana pale nyumbani, niame kabisa na nisije kukanyaga, mbaya zaidi alitoa maneno makali kabisa ya kusema kuwa niende kwa hao ccm ambao wananipa kiburi wakanipe nyumba ya kukaa (wakati anaongea maneno ayo mbele ya mwenyekiti wa serikali za mtaa ambaye ni mwenyekiti pia wa serikali za mtaa) nilisikitika sana wakuu.

Baada ya siku 6 baba alinipatia pesa yangu yote laki 7, siku hiyo hiyo nikaondoka nyumbani na kwenda kupanga chumba cha umeme pamoja na kununua godoro niakaanza maisha ya kubangaiza tangu mwaka jana,

Tatizo linaanzia hapa
Kodi yangu ilikuwa inamalizika mwezi wa nne tarehe 30, na sehemu tulipokuwa tunafanya kazi kama kibarua nilipunguzwa na kiwanda baada ya kuona uzalishaji umepungua kutokana na hili janga la corona, kwa hiyo tangu mwezi wa 3 nipo tu nyumbani sina kazi wala kibarua, baba mwenye nyumba alinieleza mapema kama naendelea na chumba au basi atafute mpangaji mwingine, nilimueleza kuwa atafute tu mpangaji maana sina pesa hata senti,

Mwisho wa mwezi uliopita nikatakiwa kuondoka pale nilipokuwa nakaa, nikampigia simu mzee wangu kumwelewesha kuwa pale ni kwetu natakaiwa kurudi kama mtoto maana sina pa kwenda, baba alipokea simu na baada ya kujua ni mimi akakata simu, Mimi nikabeba vitu vyangu nikaenda navyo palepale nyumbani, nimeshangaa sana mzee ananizuia nisiingie nyumbani. baba yangu mzazi amediliki kuniambia mimi sio mwanae mimi ni kibaka tu

Mpaka imefikia hatua ya kumweka mtu mlangoni ahakikishe kuwa hakuna mtu ambaye afahamiki kuingia pale ndani nikiwemo mimi, nilienda kwa mwenyekiti wa serikali za mtaa jana, akaniambia pale ni nyumbani na mzazi hapaswi kumfukuza mtoto katika kipindi kama hiki cha janga ili zito,

Mwenyekiti akaniambia ili huyu mzee asirudie iki kitendo cha kunifukuza inatakiwa niende kwenye ngazi ya kata, leo nimeenda kwenye kata na kuwaeleza mkasa mzima nimeshangaa sana yaani viongozi wa kata wanasema mimi inawezekana sina akili timamu, hapo akili ikanijia moja kwa moja mzee ameshatoa hongo kwenye ngazi ya kata ili nisiipate haki yangu kama mtoto, nimepanga kesho kwenda kwenye ngazi ya juu zaidi ya kuipigania haki yagu kama mtoto nirejee nikae pale nyumbani mpaka ili gonjwa litakapopita, kitu kingine naona kabisa hata kwenye ulithi kuna hati hati nikadhurumiwa na huyu baba,

Naombeni ushauri wenu wakuu.
Niende ngazi gani au nitumie njia gani huyu mzee asininyanyase kwenye nyumba nikiwa kama mtoto wake?
Na pia kama itatokea mirathi niwepo pasipo kupunjwa?
WE PUMBV SAAAANA, iaka 37 unang, ang, ania kukaa kwa baba yako, miaka 37 bado unavizia ulithi. Si utafute vyako. Amekizaa, bado amekusomesha, na laki saba amekupa, bdo unataka ukae bure. Tubu kwa huyo babako pmbv wewe
 
Back
Top Bottom