Msaada wa mawazo juu ya biashara ya photo studio & photo printing services

Hii biashara inakua nzuri hasa maeneo ya karibu na shule, vyuo au makazi ya watu na ofisini.

yah ni kweli nafikiri muhimu kupata msimamizi mzuri...vipi una uzoefu nayo ndugu?
 
Hapana sina uzoefu nayo lakin kwa maelezo ya wadau huko juu inaweza fanyika vizuri tu. Ili mradi uwe na msimamizi mzuri.
 
JE ZILE CAMERA ZA KUSHOOT KWENYE SHEREHE ZINAAPATIKANAJE NA JE LENSI YAKE IKOJE?

NA KAMERA ZA KUSHOOT LABDA MOVIE, KWAYA, AU CHOCHOTE KILE ZIKO AINA GANI NA ZIPI NZURI KWA SHUGHULI HIZO? NISAIDIENI WADAU WANAOJUA HAPA
 

MKUU UMEMALIZA KILA KITU...TUPIAMO MAWASILIANO YAKO UPANDE WA PM ILI NIKUTANE NA WEWE NA KUJADILI KWA KINA JUU YA UENDESHAJI ILI NIANZE UWEKEZAJI.
 
JE ZILE CAMERA ZA KUSHOOT KWENYE SHEREHE ZINAAPATIKANAJE NA JE LENSI YAKE IKOJE?

NA KAMERA ZA KUSHOOT LABDA MOVIE, KWAYA, AU CHOCHOTE KILE ZIKO AINA GANI NA ZIPI NZURI KWA SHUGHULI HIZO? NISAIDIENI WADAU WANAOJUA HAPA

Ukipata canon 600 d itasaidia au kama bajeti yako ipo vizuri unaweza kununua canon 5d mark3
 
Uko vizuri
 

Hii ni kama photo point pale mlimani city?
 
Kama kuna wataalam wa kupiga picha aina zote;
Aina gani ya camera ni nzuri kwenye sanaa hii?
Bei yake ikoje
Jinsi ya kuiendesha biashara hii
 
asante mkuu nimekuelewa sana
 
Wakuu habari zenu,
Nimeamua kudaka fursa ya kupiga picha za kisasa ambazo zimepata umaarufu mkubwa hasa kutokana na wimbi la ongezeko kubwa la matumizi ya mitandao ya kijamii na maendeleo ya teknolojia.

Nimenunua nyenzo kadhaa za kazi yangu tarajiwa kama vile computer kwa ajili ya photo editing na bajeti ipo kwa ajili ya vifaa vinginevyo.
Kwa wataalamu na wazoefu wa kazi hizo humu ndani, naomba msaada wa ushauri ninunue camera gani ambayo itafaa zaidi kwa bajeti ya laki 8 na nusu [iwe ni DSLR] kwa ajili ya upigaji picha.

Pia naomba kufahamishwa program nzuri za photoshop za kutumia kwa ajili ya photo editing. Na Kama kuna mtu anauza DSLR camera nzuri na kwa bei tajwa hapo juu tunaweza kufanya biashara.
Natanguliza ahsante kwa michango yenu.
NB: mimi sio pro photographer, bado najifunza...
 
Camera nzuri kwa bajeti ya laki nane?? Hebu kua serious kidogo mkuu.
Nimejaribu kuangalia mtandaoni nimeona entry level DSLR ambazo hazizidi dola 450 hivyo Naamini hata ikiwa used mwaka 1 kwa bei hiyo(850k) naweza bahatika hapa bongo .

Ni kwa kuanzia tuu mkuu mambo yakikaa vyema nitachukua camera nzuri na ya kisasa zaidi.
 
wabongo wengi hawana ufahamu sana na DSLR zipo kupatana bei hizo japo hutapata mpya kabisa na model ya karibuni ila utapata. kuwa makini na hao jamaa ambao hawana namba za Tz ni matapeli,

search keyword hizi dslr, nikon, canon, utazipata tu

pia angalia uwezekano wa kuagizishia nje kwa budget hio unapata dslr nzuri tu, zipo za around dola 400
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…