Msaada wa Mawazo kwa wenye uzoefu wa kununua na kuuza mchele wa Jumla nataka nijiajiri mtoto wa kike

Hiyo ni good adea. Mchele safi mzuri unapatikana kyela. Kwa dar hii biashara inaweza kukutoa. Nakushauri kwa kuongezea uwe sehemu ya changanyikeni,hapo utauza rejareja na jumla.

A. Mchele kwa sasa kilo 20 mzuri ni 26,000
C. Wasafirishaji wapo sehemu husika,wala hutapata tabu (magari ni mengi kuna madalali hapo)
D. Mizani kama hamjazidisha uzito hilo halitawapa shida
E. Hakuna gharama za kukusanya ksbb utafika mashineni utawakuta wauzaji na wanunuzi wengine watakuongoza tu kuijua hii biashara

=kwa kuongezea kipindi kizuri cha kuanza hii biashara ni sasa ksbb ndio kipindi cha mavuno,hivyo gharama inakuwa chini,kwa unaeanza anza ni vizuri kuanza kuzoea mazingira sasa.


Sent from my SM-C9000 using JamiiForums mobile app
 
Naomba mnitoe matongotongo ndugu zangu. Mchele unapakwaje mafuta? Ni mafuta ya aina gani wanapaka? Duniani kote wanafanya hili zoezi au ni exclusive kwa Bongo tu?
Hhaa hujawahi ona mkuu? Wanakokovoa utakuta madumu ya mafuta kibao...unawaka hatari...nadhan ni tz tu
 
Nadhan mie nishazoea super Kyela..nimeuacha. .nw natoka nao kahamaaa...! Upo upo tu yaani
 
Man nakubakiana na wewe sehemu zote ila nakukataa kwenye bei ya nanunuzi maana mi nakiduka changu cha mchele nanunua kawe mpa kwa sh.1300,na nauza 1400 ama1500 ukimpanga kwa 1700 atapiga nao picha maana huo wa 1700 kwa sehemu za jumla kama kawe tunauita mchele wa kula baba apitie masoko vizuri
 
Faida za mcheke hazijawahi kubadilika kilo ya mchele ikakupa zaidi ya 300 ni 100,120,150 na 200 ikipanda na zali la mental ndo unakutana na 300 hapo lazima ufanye sherehe ila kurudisha hela yako bila kupata faida ni jambo kawaida na kwa wanaoonza wengi wanapigaga chini kwa kukosa timing ya business na wateja ikiwemo location ya kuuzia maana kuna watu wanachagua wale mchele wa kutoka wapi hapo ndo huchelewi kumpata mchawi wako kuwa anakuloga biashara haziendi mara chuma ulete

Acha kabisa ukiwa na mtaji unatakiwa kuwa na roho ngumu hatar uvumilivu huku matapeli wanakuwinda kwa style zote wakuingize king
 


Ukiwa na mtaji mdogo ile hela ya mtaji itarudi bila kifaida...mfano..unaenda mashine unachukua kilo 20!.ukiweka na usafiri imekula kwako! Na Kama una mzunguko mdogo wa wateja🥴🥴! Kilo 20zitumie week mhhhh🤸
Mchele ukitaka ukulipe weka wa Bei 3tofauti...ubebane!

Kitu ambacho kinalipa no 1kwenye hayo maduka Mie niliona ni mafuta ya taa na sigara inafatia vinywaji! Mengine mbwembwe!
 
Reactions: amu
Mkuu, huwa nafikiri hyo biashara ni nyepesi kumbe sivyo.. kukaanga na kupaka mafuta tani kadhaa si mchezo. Kumbe ile harufu huwa ni bandia?!
Hii ya kukaanga sijawahi kuisikia.... Mchele ukishaukaanga si ndio umeshaupika hapo sasa
 
Naomba mnitoe matongotongo ndugu zangu. Mchele unapakwaje mafuta? Ni mafuta ya aina gani wanapaka? Duniani kote wanafanya hili zoezi au ni exclusive kwa Bongo tu?
Mafuta ya kupikia haya ya kawaida. Ila ni vema ukatumia ambayo hayana harufu kama Korie au sunflower but sio ya alizeti maana yale yanakuwa na kile kiharufu cha mafuta ya alizeti.

Mafuta yanatumika kuzuia mchele usiharibike kama unakwenda kuwekwa store kwa mida mrefu, mfano mwaka mzima. Kwa maana mchele huwa unapotoka mashineni huwa unakuwa na vumbi fulani hivi jeupe la kawaida ambalo hutokana na zile fujo za kuukoboa mpunga.

So kama utakwenda kugifadhiwa hivyo hivyo kwa zaidi ya miezi kumi na mbili yaani mwaka kuna uwezekano ukaharibika especially maeneo ya chini ya mfuko sehemu mfuko utakuwa umelazwa au kupandishiwa na mwingine kutokana na ujoto utakaotokea na unyevunyevu. Huwa mchele unatengeneza fungus fulani hivi kama funza weupe......
 
Kama sehemu nyingine duniani hawatumii njia hii basi inaonyesha jinsi tulivyo nyuma. Nchi zinazolima mchele kwa wingi wanauza mchele mzuri sana hivyo kama na wao hawapaki mafuta basi ni ajabu.
 
Kuweka utambulisho kuwa wewe ni mtoto wa kike kuna add value gani kwenye Tangazo lako la Biashara!
 
Mkuu alizeti na Sunflower ! ulikua unamaanisha nini!
 
Ndio uwezo wako wa kufikiri unapoishia. Ujinga na upeo finyu ulio nao ni vema ukabaki nao na sio vema kuwaambukiza wengine..! Ulivyo tapeli wewe unadhani kila mtu ni tapeli kama wewe?
Funguka hapa hapa, DM kuna upigaji.
Tiririka hapa watu wakuweke sawa.
 
Kama sehemu nyingine duniani hawatumii njia hii basi inaonyesha jinsi tulivyo nyuma. Nchi zinazolima mchele kwa wingi wanauza mchele mzuri sana hivyo kama na wao hawapaki mafuta basi ni ajabu.
Inawezekana sio ajabu, ila ni teknolojia yetu mpya. Ambayo na wao hawaijui wanaweza kuja kujidunzia kwetu. Cha msingi hii teknolojia isiwe na madhara.
 
Nataka kuchangia kidogo kuhusiana na hii baishara ya mchele niliyowahi kufanya kipindi cha 2017&2018..

Kwanza kabla ya kufata mzigo hakikisha kuwa una mtaji wa kutosha,soko lako lipoje na umewalenga wateja wa sampuli gani.baada ya kuyafahamu hayo ndo unaanza kuingia kwenye biashara yenyewe.

Pili, baada ya kufanya maamuzi ya kufanya hiyo biashara,nakushauri ufate mzigo wewe mwenyewe na usimuagizie mtu kuna upigaji lakini unaweza ukapoteza msingi kwa yule aliyekuagizia kukimbia na mtaji wako.

Nadhani kuna baadhi ya wachangia wameeleza vizuri kuhusu hiyo biashara,lakini na mimi naomba nielezee uzoefu na changamoto za biashara hii...kuna aina mbili za kuweza kupata mchele, njia ya kwanza kwa mfano muda huu maeneo ya ifakara,kilombero wapo kwenye mavuno kwahiyo unaweza kwenda mashambani kwa ajili ya KULENGA MPUNGA(kufikicha mpunga kwa kutumia mikono)..maana yake unakwenda kununua mpunga moja kwa moja toka kwa wakulima,kipindi nafanya hii biashara tulikuwa tunanunua gunia la debe kumi kwa shilingi 80000 lakini pia inategemea na msimu ukiwa mzuri kwa maana ya maeneo mengine mpunga umepatikana kwa wingi bei ya debe la mpunga hushuka..

Hii njia ni nzuri lakini inachangamoto zake kwa maana ili uweze kuyafanya hayo yote lazima uwe na mwenyeji wa kuweza kuku link na wakulima, kumpoza mwenyeji lakini pia hii njia hutumia mikono kwa ajili ya kufikichia mpunga ili uweze kujua mpunga huu nikiupeleka mashineni unaweza kutoka vizuri/vibaya..unaweza ukakuta umeufikicha mpunga na kutoka vizuri lakini ukija kukoboa mchele hutoka vibaya mwishowe usipate ulichokitarajia kupata/ukapata kwa % ndogo.

Njia hii inachangamoto nyingi nimefupisha ziwezi kuzitaja zote,maana kuna usafiri kutoka shambani,viroba,kamba, wabebaji, turubui la kuanikia mpunga n.k

Kuna njia nyingine ambayo ni nzuri kwa sababu inaokoa muda na kufanya biashara kuwa rahisi kabisa.. KUKINGA MPUNGA.njia hii mnunuzi utembelea mashine kwa ajili kutafuta mchele uliokobolewa kutoka kwa madalali au wakulima wanaotaka kuuza mchele huo. Hapa kuna makubaliano baina ya mnunuzi na mkulima/dalali baada ya kukobolewa hapo mashineni,inategemea na aina ya mchele, kuna super,middle na mavulavula kipindi nanua mie supa ilikuwa inauzwa 1400-1300 kwa kilo, middle 1100-1250,na vula vula 1000 kwa kilo ila hapa inategemea na bargaining power yako.

Njia hii changamoto zake ni chache,mfano kuzungukia mashine zote za eneo husika(Muda) kwa ajili ya kupata mchele mzuri,lakini pia pindi utakaponunua mzigo kwenye mashine tofauti kuna gharama za kubeba aidha kwa piki piki au baiskeli ama mkokoteni,lakini usiweze pia kupata mzigo kwa wakati inategemea na unataka mzigo kiasi gani, lakini pia kuna kuangaliana usoni sana haswa kwa watu wanaotoka maeneo ya kilombero,ifakara,mgeta ,mlimba,kuna siku nilikinga mchele na kufikiana muafaka na muuzaji/mkulima lakini kutokana na kuwa mgeni yule mwenye mashine aliweza kuupata ule mzigo malikauli lakini mimi mwenye cash niliishia kutumbua macho na kushikwa na butwaa hiyo ilikuwa maeneo ya kijiji cha Mwaya-Mang'ula na changamoto zingine ni ndogo ndogo,mfano malazi,chakula

Baada ya kupata huo mchele kuna vitu vifuatavyo vinahitajika...Viroba kuhifadhia mchele kiroba =shs700/800,Mafuta kwa ajili kung'arishia mchele wako,mimi nilikuwa natumia mawese na mafuta ya kula ya kawaida nilikuwa natumia Chupa mbili kwa mafuta ya kawaida na mawese nusu chupa kwa tani 1(kg1000),kamba, ushuru wa mazao 30 kwa kilo(3000/kg100) usafiri shs 70 kwa kilo(7000/kg100) wabebaji shs 500/kg 100 kama utahitaji kugrade mchele pamoja na kupaka mafuta tulikuwa tunachajiwa shs 20/kg1 (2000/kg100) nahisi ni hivyo

Nilichogundua kwa walaji wa Dar wanapenda sana kununua michele iliyonyooka ikiwa inang'aa kwa hiyo hakikisha unalifikia soko lako vizuri kwa kuangalia mahitaji ya wateja wako. Naendelea kukushauri kuwa makini unapotaka kununua mchele kutoka kwa wakulima/madalali hakikisha mchele unaonunua ni mzuri maana hata ukitaka kuja ku ugrade unakuwa hupati chenga nyingi,jitahidi kununua mchele ulio supper na middle ambao hutokana na mbegu ndefu kama mfano mbawa mbili,sengo ila inategema unapochiukulia mchele wako ili upate kitu kizuri.

Biashara haina hasara lakini pia haina faida kivile maana wengi wetu tunafikra za kupata kwa kufanya tu kitu kwa mara moja.....Nakushauri ndugu,kwenye biashara walenge mama ntile, shule za nasari, wenye maduka madogo madogo lakini pia kama Una store jaribu kushusha bei kw a wateja wanaoanza kununua kuanzia kg 10 ,itakusaidia ku retain wateja wako na kutengeneza network kwa wateja wengine ..mfano mchele ulikuwa unauza 1700 unaweza kufanya discount ya shs 50 kwa kila kilo ili kumvutia mteja wako.
 
Vipi ule mchele uliokatika katika hatuwezi kusema mbaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…